My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, October 23, 2012

Hon. Philipo Augustino Mulugo, Dep Minister of Education and Vocational Training

Hon. Philipo Augustino Mulugo -- Deputy Minister of Education and Vocational Training, Tanzania, speaking on Education for Employment, Developing Skills for Vocation at the Innovation Africa Summit - 5th-7th October 2012 at the Westin Hotel, Cape Town, South Africa. Supported by the Government of South Africa and co-hosted by AfricanBrains and the University of the Western Cape. 
 

Watoto wauawa kwenye mapigano Sudan



Eneo la milimani Kordofan Kusini

Jeshi la Sudan limesema watato wawili wameuawa kufuatia mashambulio mapya ya mabomu yaliyotekelezwa na waasi katika mji mkuu wa jimbo la Kordofan ya Kusini.
Msemaji wa jeshi la nchini hiyo amesema kuwa raia wanane walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo mjini Kadugli.
Kundi la waasi wa SPLM-North nchini Sudan limesema lilikuwa likijibu mashambulio ya siku kadhaa yaliyotekelezwa dhidi yao na wanajeshi wa serikali
Umoja wa mataifa unakadiria kuwa maelfu ya watu wamehama makwao na wengine wengi kuathirika kutokana na mapigano hayo katika eneo la Kordofan ya Kusini, tangu uasi huo ulipoanza mwaka uliopita wakati Sudan Kusini ilijapatia uhuru wake.

Kesi dhidi ya E. Kemboi yatupilliwa mbali Kenya



Mwanariadha Ezekiel Kemboi

Kesi ambayo bingwa wa Olimpiki wa Kenya, Ezekiel Kemboi alishtakiwa kwa kumshambulia Ann Njeri Otieno mjini Eldoret Mkoani Rift Valley mwezi wa Julai mwaka huu, imetupiliwa mbali na mahakama mjini humo
Kulingana na hakimu wa mahakama ya Eldoret Francis Kyambia mlalamishi Njeri amekubali kesi hiyo waimalize nje ya korti.
Anne Njeri Otieno alidai kuwa mwanaridaha huyo alimshambulia alipokataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye mwishoni mwa mwezi Juni .
Lakini kabla ya kesi hiyo kusikilizwa tena, Bi Njeri Otieno aliambia mahakama kuwa alimua kumwodolea mashtaka Kemboi.
Bwana Kemboi, anayefanya kazi katika idara ya polisi daima amekuwa akikanusha madai hayo
Hakimu alimwachilia kwa dhahama ya dola 230 mwanariadha huyo mwishomi mwa mwezi Juni na kumruhusu ashiriki michezo ya Olimpiki mjini London ambako alishinda medali yake ya pili ya dhahabu.

Ann Njeri Otieno

Bi Njeri aliwaambia waandishi wa habari kuwa alifutilia mbali kesi hiyo kwa sababu anataka kuendelea na maisha yake.
Njeri alikuwa amemshtaki Kemboi kwa kumshambulia na kisu nje ya nyumba yao iliyoko mtaa wa West Indies mjini Eldoret akiwa ndani ya gari lake. Lakini Kemboi alidai ni Njeri ndiye aliyemshambulia akiwa na watu wanne.
Hatimaye Kemboi, ambaye hufurahisha mashabiki sana kwa densi yake murwa kila anapoibuka mshindi uwanjani, alisafiri hadi London na timu ya Kenya na kushinda dhahabu mbio za mita elfu tatu kuruka viunzi na maji.

Mafuta yanayoibwa Nigeria huishia ulaya



Eneo la Niger Delta ndilo linazalisha mafuta mengi ya Nigeria

Wateja wakubwa wa mapipa laki mia moja na themanini ya mafuta yanayoibwa kutoka nchini Nigeria wako katika nchi za Kusini Mashariki mwa Ulaya pamoja na Singapore, kulingana na wanaharakati.
Mwanasiasa kutoka jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta, Patrick Dele Cole, amesema kuwa asilimia tisini ya mafuta yanayoibwa yanasafirishwa kwenda nje ya nchi kinyume na sheria.
Amezindua kampeini yenye kauli mbiu ''Komesha wizi'' ili kumaliza visa vya wizi wa mafuta.
Nigeria ni mojawapo ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi ingawa idadi kubwa ya wananchi wake wanaishi kwa umaskini
Kampeini hiyo inalenga kuzichunguza meli hizo kwa satelite na kubaini pesa zinazotokana na uuzaji huo zinakokwenda.
''Unapoanza kuuliza maswali, na kuanza kuangazia swala hili, utakuwa umesuluhisha zaidi ya asilimia hamsini ya matatizo kuhusiana na wizi wa mafuta.'' alisema bwana Dele Cole, mwanadiplomasia mkongwe na mshauri wa zamani wa rais.
''Nadhani ni mumimu kutoa onyo kwa wale matajiri kwamba siku yao ya kuwajibika itafika''
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa sekta nzima ya mafuta nchini humo inakumbwa na ufisadi,
Wanasiasa wengi wanahusika na wizi huo anasema Will, huku sehemu ya mapato ya mafuta hayo yakitumiwa kununua kura na kufadhili kampeini zao.
Jeshi la Nigeria linapaswa kusitisha visa vya wizi wa mafuta lakini wao huchukua hongo ili kutofuatialia visa hivyo

Friday, October 19, 2012

hali ilivyokuwa leo



.
Taarifa kutoka http://networkedblogs.com/DFxGK zimeamplfy kwamba hizi picha ni za watu sita wafuasi wa Sheikh Ponda waliokua wakiandamana kwenda Ikulu WATU sita waliokuwa na nia ya  kuandamana kuelekea Ikulu lakini imeshindikana baada ya polisi kuwakamata.
Waandishi wa habari ambao wapo karibu na Ikulu wamesema hawa watu walifika mmoja mmoja kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati ambapo pia waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha.
.
.
.
.

Wanajeshi kutoka JWTZ.

HALI BADO TETE MITAA YA KARIAKOO: MABOMU YAZIDI KURINDIMA


 
Hili lilikuwa tangazo kwa ajili ya maandamano ya leo.
 
Magari ya Jeshi la Wananchi yakipita katika mitaa ya Kariakoo kuwataarifu wananchi kutawanyika eneo hilo.
Baada ya baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kutawanywa kwa mabomu na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia hapo awali, kwa sasa waumini hao wanajipanga kuvamia kituo cha polisi mtaa wa Msimbazi wakiwa katika makundi makundi mikononi wakiwa na mawe na wakiimba nyimbo. Awali magari ya Jeshi la Wananchi yalipita mitaa ya Kariakoo yakiwa na wanajeshi waliokuwa wakiamuru wananchi kutawanyika lakini hali inaonekana kubadilika maana kwa sasa waumini hao wanajikusanya upya kutimiza azma yao ya kuandamana mara baada ya kumaliza swala ya saa 10 katika msikiti wa Idrissa uliopo Kariakoo. Baadhi ya madai ya waumini hao ni KUKAMATWA SHEIKH PONDA, KUTOONEKANA KWA SHEIKH FARIDI WA ZANZIBAR NA KUKOJELEWA QURAN.

KARIAKOO DAR LEO HAKUNA MSONGAMANO WA WATU

FFU wakizunguka maeneo ya Kariakoo leo huku  wakitumia kipaza  sauti  kuwataka  wananchi wote  kurejea majumbani kwao
Hili ni eneo la Msimbazi ambalo kwa kawaida  huwa  kuna msongamano mkubwa wa  watu
Eneo la mzunguko  wa Kariakoo ambalo jiupe kama unavyoliona hapa
Hapa  sio maduka  yamefungwa  muda  umepita ama  wahusika  wamefiwa hapana ni baada ya vurugu  kutokea
Hii ni kariakoo sio biashara  mbaya ni usalama hakuna
                                       ingekuwa  vipi kama kariakoo  kila  siku  kungekuwa  hivi?

Tukio  hilo   la kukosa  watu kabisa  eneo hilo kama  picha  zinazoonyesha  limetokea  leo kutokana na vurugu  kubwa  vilizoibuka  toka majira ya mchana eneo hilo vurugu  zilizohusisha  jeshi la  polisi  kikosi  cha  kutuliza ghasia (FFU) na badhi  ya  waumini  wa dini ya kiislam ambao  wanashinikiza wenzao ambao  wanashikiliwa  kwa  tuhuma  za  kufanya  vurugu na  kupora mali  wakati  wa vurugu  za waumini  wa  dini  hiyo katika  eneo la Mbagala .
Vurugu  hizo ambazo  chanzo chake ni  watoto  kugombana na mmoja kati ya  watoto hao  wawili ambaye ni mkristo kukojolea  Msaafu  jambo  lilozua vurugu na hata  waislam kuandamana na  kuchoma makanisa .
Hivyo  kutokana na utata  huo  leo mkuu  w  mkoa  wa Dar es Salaam na kamanda  wa  polisi kamnda maalum ya Dar walionya kutokuwepo kwa maandamano  ila bado  watu sita wafuasi wa Sheikh Ponda waliokua wakiandamana kwenda Ikulu kabla ya  kukamatwa na  polisi  na  ndipo  vurugu  zilipoanza.
Wakati  vurugu  hizo  zikianza  eneo la Kariakoo  na maeneo mbali mbali ya jiji maduka na benk  zote  zilifungwa pamoja na  wananchi kutawanywa  kuondoka  maeneo hayo .
Mtandao  huu  umeshuhudia wananchi  wakitawanywa na  waliopo ndani kama ni  zaidi ya  watano  walikuwa  wakitolewa kwa  virungu huku baadhi ya  wananchi  wakijeruhiwa kwa  kukimbia vurugu na wengine kwa kupigwa na polisi na mgambo  wa  jiji.
Vipo taarifa  ambazo bado  kuthibitishwa kuwa  watu kadhaa  wamejeruhiwa  vibaya na  mali mbali mbali   ikiwemo  pikipiki  mmoja kuchomwa  moto .
Hadi mwandishi  wa mtandao huu anaondoka  eneo hilo la Kariakoo tayari magari ya wanajeshi  wa JWTZ yalikuwa  yakifika  eneo hilo  huku polisi  wakitawanywa katika misikiti mbali mbali  kuthibiti hali hiyo.
Baadhi ya  wananchi  wamemwomba  Rais Jakaya  Kikwete  kusitisha  safari  zake za nje na  kuingilia kati  kurejesha amani na utulivu nchini huku baadhi  wakidai  kuwa kitendo  kinachofanywa na  waislam hao ni  kuiharibia  dini  hiyo kwa  waumini  wake kukosa imani kwa  wananchi pindi  wanapoomba nafasi mbali mbali za uongozi  hivyo  kumwomba  kiongozi  wa waislam nchini  kutoa tamko dhidi ya haya  yanayoendelea  ili kurejesha imani kwa  watanzania.
Uchunguzi  wa mtandao  huu pia umebaini  kuwa  vurugu  hizo  zinachochew  zaidi na polisi na mgambo ambao  wamekuwa  wakiwapiga  wananchi hata  wasio na hatia na baadhi ya askari  wakizunguka maeneo mbali mbali na kuwatoa  nje  watu  waliojificha ndani ya nyumba na maduka yao bila  kuangalia na muumini wa  dini ya kiislam ama mkristo na  kuwakamata .
Moja kati ya maswali ambayo  polisi  wanapaswa  kujibia ni pamoja  na hili kuwa maandamano ya  waislam  ,wakristo wanakamatwa na  kupigwa kwa sababu  zipi? Pili kwa  waislam  kwanini wanafanya maandamano kwa jambo ambalo  lipo tayari mahakamani  ?
Mungu  ibariki Tanzania ,Mungu  wabariki  viongozi  wa Tanzania na Mungu wabariki waumini  wa  dini  zote  ili  kuifanya Tanzania  kubaki kuwa nchi ya Amani.

DAR ES SALAAM HALI MBAYA


Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba kuna vurugu zinaendelea maeneo ya Kariakoo ambapo baadhi ya Waislamu wanaandamana kuelekea Kidongo Chekundu na polisi wanatumia mabomu ya machozi kuzuia maandamano hayo. Hali imekuwa tete na polisi wamelazimika kutumia helkopta kuzuia vurugu hizo ambazo zinahatarisha amani jijini Dar es Salaam

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WATANZANIA NCHINI UINGEREZA‏

Mh waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Watanzania waishio 
nchini Uingereza (hawapo pichani).
 
JUMANNE tarehe 16.10.12 Mh Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Kayanza Peter Pinda alipata fursa ya pekee ya kukutana na baadhi ya Watanzania waishio nchini Uingereza katika ofisi za Ubalozi wetu zilizopo hapa jijini London ili kuongea, kufahamiana nao na kuwapa taarifa kamili kuhusu hali ya nchi Kiuchumi, Kisiasa, Kiusalama, Kimaendeleo na changamoto mbalimbali zinazozikabili taifa letu.…
 
Mh waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Watanzania  
waishio nchini Uingereza (hawapo pichani).

JUMANNE tarehe 16.10.12 Mh Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Kayanza Peter Pinda alipata fursa ya pekee ya kukutana na baadhi ya Watanzania waishio nchini Uingereza katika ofisi za Ubalozi wetu zilizopo hapa jijini London ili kuongea, kufahamiana nao na kuwapa taarifa kamili kuhusu hali ya nchi Kiuchumi, Kisiasa, Kiusalama, Kimaendeleo na changamoto mbalimbali zinazozikabili taifa letu.
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifananua jambo wakati alipokutana na baadhi ya Watanzania waishio nchini Uingereza katika ofisi za Ubalozi zilizopo jijini London juzi.

Mh Waziri Mkuu alieambatana na mkewe mama Tunu Pinda walipokelewa rasmi na Mh Balozi wetu Peter Kallaghe, wafanyakazi pamoja na maofisa kutoka ngazi mbalimbali katika Ubalozi wetu. Kabla ya kuanza hotuba yake Mh Balozi alichukua fursa hii kuwakaribisha na kuwashukuru watanzania wote ambao waliojitokeza kuja kumsikiliza na kumsalimia Mh Waziri Mkuu.

Wednesday, October 17, 2012

Polisi wa Kenya wajeruhiwa vibaya



Polisi waliwahi kunasa mabomu na maguruneti ambayo Al Shabaab walikuwa wananuia kutumia kwa mashambulizi Kenya

Takriban polisi kumi wa Kenya wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi la guruneti
Maafisa hao wa polisi walikuwa wanasaka nyumba moja mjini Mombasa, pwani mwa Kenya ambako walipata silaha ikiwemo bunduki aina ya AK-47 na maguruneti mawili.
Msemaji wa polisi alidokeza kuwa wanamgambo wa Al-Shabab huenda walihusika na shambulizi hilo.
Kenya kwa muda sasa imakumbwa na misururu ya mashambulizi ya maguruneti, tangu wanajeshi wake walipoingia Somalia kupambana na wanamgambo wa Al Shabaab mwaka jana.

Mkuu wa Polisi mkoani humo, Aggrey Adoli,aliambia waandishi wa habari kuwa washukiwa watatu wa kigaidi waliuawa katika makabaliano kati yao na polisi baada ya shambulizi hilo.

Washukiwa wa Al-Shabab wametekeleza mashambulizi kadhaa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita eneo la Pwani ambalo ni maarufu kwa watalii.

Wanajeshi wa Kenya nao wamekuwa vitani kuondoa kundi la Al Shabaab kutoka katika ngome yao kubwa na ya mwisho ambayo ni Kismayo kwa ushirikiano na wanajeshi wa Muungano wa Afrika tangu Oktoba mwaka jana, jambo ambalo walifanikisha mwanzoni mwa mwezi huu.

Rais Obama na Mitt Romney watoana jasho



Barack Obama na Mit Ronmney wamemenyana katika mjadala wa pili wa kempeini za uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao
Rais Barack Obama na mshindani wake wa Republican,Mitt Romney, wametoana jasho katika mdahalo wa pili kwenye kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani.
Wawili hao walikabiliana mbele ya wapiga kura ambao bado hawajaamua nani watakaye mpigia kura kwenye uchaguzi huo mwezi ujao.
Walizungumzia sera ya kodi, ajira na nishati kila mmoja akijaribu kumtia dosari mwenziye wakati wakielezea watakavyofanikisha sera zao kuhusu maswala hayo.
Walikosoana mara kwa mara huku wakati mmoja Rais Barack Obama akimtuhumu Romney kwa kusema uongo.
Mpiga kura mmoja ambaye angali kuamua mgombea atakayemchagua, alisema kuwa hali ya ubishani kati ya wawili hao haikutoa taswira nzuri kuwahusu.
Mdahalo huu ni wa pili huku wagombea hao wakisubiri mdahalo mmoja na wa mwisho siku ya Jumatatu kabla ya uchaguzi kufanyika baadaye mwezi ujao.
Mhariri wa BBC wa maswala ya Amerika ya Kaskazini, anasema kuwa baada ya mjadala wa mapema leo asubuhi, Barack Obama ameweza kujiimarisha tena kwa wapiga kura kwani alionekana kuibuka mshindi.
Katika majibizano makali kuhusu mauaji ya balozi wa Marekani nchini Libya, bwana Romney alisema kuwa tukio hilo lilifedhehesha sera ya Obama katika eneo la Mashariki ya kati.
Naye Obama alisisitiza kuwa atafanya kila awezalo kuwakamata washukiwa wa mauaji hayo.

Rwanda inatoa amri kwa M23, yasema UN


Kiongozi wa kisiasa wa M23 Jean Marie Runiga

Waziri wa ulinzi nchini Rwanda, ametuhumiwa kwa kuamuru uasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa ripoti ya wataalamu wa Umoja wa mataifa.
Ripoti hiyo ya kisiri, iliyofichuliwa na shirika la habari la Reuters, inasema kuwa Uganda pia inaunga mkono waasi wa M23 ambao wamekuwa wakipigana na jeshi la DRC tangu mwezi Aprili.
Ripoti hii inakuja baada ya ripoti nyingine ya Umoja wa Mataifa kutolewa mwezi Juni ambayo ilituhumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi hao
Lakini Rwanda na Uganda zimekuwa zikikna madai ya kuunga mkono waasi wa M23.
Duru zinasema kuwa katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, Rwanda imeunga mkono makundi ya waasi Mashariki mwa Congo, kama njia moja ya kupiga vita waasi wa kihutu waliokimbilia eneo hilo baada ya mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Baadhi wanatuhumu Rwanda kwa kutumia waasi kupigana vita vyake dhidi ya DRC , nchi ambayo ina utajiri mkubwa wa madini na eneo zima la Maziwa Makuu.
Taarifa za hivi punde za wataalamu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa zinatoa maelezo zaidi kuhusu Rwanda kujihusisha na vita vya DRC.
Maelfu ya watu wameachwa bila makao kufuatia mapigano Mashariki mwa DRC

Wataalamu hao wanasema kuwa waasi wa M23 wanapokea amri za moja kwa moja kutoka kwa mkuu wa majeshi ya Rwanda, Generali Charles Kayonga, " ambaye naye anafuata amri za waziri wa ulinzi Generali James Kabarebe.
Wataalamu hao pia wanasema kuwa Rwanda imekuwa ikitoa silaha kwa waasi hao na kuweka mikakati ya kusajili waasi zaidi ili kuliganya kundi hilo kuwa kubwa.
Maelfu ya watu nchini DRC wamepoteza makao yao kufuatia vita hivyo kati ya waasi na wanajeshi wa Rwanda.
Ripoti hiyo iliyoonwa na shirika la habari la Reuters inasema kuwa wanajeshi wa Rwanda na Uganda wamesaidia waasi wa M23 kupanua harakati zao katika eneo la Mashariki mwa DRC.

Tuesday, October 16, 2012

Gary Neville urges Manchester United's Wayne Rooney to adapt to stay at the top




Wayne Rooney: Gary Neville has challenged the England star to reinvent himself to stay at the top
Wayne Rooney: Gary Neville has challenged the England star to reinvent himself to stay at the top

Gary Neville has challenged Wayne Rooney to reinvent himself to stay at the top as he moves into the second decade of his career.
Rooney burst onto the domestic season 10 years ago when his winner for Everton against Arsenal made him the youngest player to score in the Premier League.
The Manchester United striker will win his 78th England cap against Poland but England coach and Sky Sports pundit Neville urged him to keep improving, citing the pragmatic approach of his evergreen club team-mates, Paul Scholes and Ryan Giggs.
"The last couple of weeks, coming back from injury, I've seen a lean, fit, hungry Rooney," Neville said.
"He looks like he is up for the next challenge in his career, to maintain his position at Manchester United.
"At the age of 26 you always have to think there's more to come. You can't get to the age of 26 and think 'My best years have gone'. He has to challenge himself.

"He has great examples of players who have continued to do that in Paul Scholes and Ryan Giggs.
"Giggs has gone from a flying, out-and-out left-winger to someone who now plays off the front, inside-left and central midfield.
"Scholes was a goal-scoring midfielder, off-the-front number player when he started playing as a 16-year-old. Now he's a holding midfielder who controls the game.
"Rooney is still a centre-forward, but he'll adapt over this next 10 years to continue to become someone who's thought of in the same way as those two players."

Wafungwa 100 watoroka jela nchini Libya



Walinzi wa magereza nchini Libya
Maafisa wa Libya wanasema kuwa mewatia nguvuni wafungwa 60 kati ya mia moja na ishirini na wawili waliokuwa wametoroka jela katika mji mkuu Tripoli .
Maafisa sasa wanadhibiti magereza kadhaa , likiwemo gereza la Al-Jadaida lililo maalum kwa wahalifu wa kawaida .
Zaidi ya wafungwa 100 walitoroka kutoka jela la Al-Judaida mjini Tripoli.
Wafungwa hao wanasemekana kuwa raia wa nchi mbali mbali na maafisa wanasema kuwa takriban watu 60 wamekamatwa.
Haijulikani ni vipi wafungwa hao walifanikiwa kutoroka jela.
Al-Judaida ni mojawapo ya jela kubwa zaidi mjini Tripoli. Mashirika ya kutetea haki za binadamu wanatuhumu maafisa wa magereza kwa kuwatesa wafungwa.
Tukio hilo la wafungwa kutoroka, linajiri chini ya wiki moja kabla ya kuadhimishwa mwaka mmoja tangu kuuawa kwa kanali Gaddafi.
Kiongozi wa jeshi la Libya, Khaled al-Sharif, aliambia BBC kuwa kati ya wafungwa 120 ambao walitoroka , nusu yao wamekamatwa.
Aliongeza kuwa baadhi ya wafungwa hao walikuwa wahamiaji haramu wa kiafrika, na wengine walikuwa raia wa Libya waliofungwa kwa makosa ya uhalifu.
Hali inayozingira tukio hilo ni tete kwa sasa na maafisa wanasema kuwa uchunguzi unafanywa kwa sasa.
Idara ya ulinzi wa ndani imeweka vizuizi barabarani katika eneo hilo kujaribu kuwasaka wale waliotoroka.
Ulinzi umedhibitiwa katika magereza hayo.

Saturday, October 13, 2012

UN yataka kuona mpango kuhusu Mali

Mataifa ya Afrika Magharibi yanajitayarisha kukamilisha mipango yao ya kuingilia kijeshi nchini Mali, kuwaondoa wapiganaji wa Kiislamu walioteka zaidi ya nusu ya nchi hiyo kufuatia jaribio la kupindua serikali mwezi Machi.
Wapiganaji wa Mali
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kupewa maelezo kamili ya mpango huo katika siku 45 zijazo, ili kuamua kama itatoa idhini au la.
Lakini hadi sasa ni mataifa machache tu ya Afrika Magharibi ambayo yamejitolea kutoa wanajeshi kwa kikosi hicho.
Baadae juma hili, Umoja wa Mataiafa, wakuu wa Ulaya na Umoja wa Afrika watajumuika na wawaikilishi wa Mali mjini Bamako, kujaribu kutafuta mkakati imara wa kuingia Mali kijeshi.

Mkuu wa mashtaka Misri akaidi rais

Mkuu wa mashtaka wa Misri, AbdalMajid Mahmoud, amerejea ofisini na ulinzi mkali na hivo kukaidi amri ya Rais Mohamed Morsi ya kumtoa kazini.
Mkuu wa mashtaka wa Misri
Rais Morsi alijaribu kumtoa kazini mkuu wa mashtaka siku ya Alkhamisi baada ya afisa huyo kuwafutia mashtaka maafisa zaidi ya 40 watiifu kwa rais wa zamani, Hosni Mubarak, ambao walishtakiwa kwa kuongoza mashambulio dhidi ya waandamanaji wakati wa mapinduzi ya mwaka jana.
Mkuu wa mashtaka na wafuasi wake wanasema rais hana madaraka hayo.
Kuachiliwa kwa washtakiwa hao kulizusha maandamano ya ghasia katika medani ya Tahrir mjini Cairo Ijumaa, ambapo watu zaidi ya mia moja walijeruhiwa kwenye maandamano makubwa kabisa dhidi ya rais tangu kushika madaraka mwezi wa Juni.
Mkuu wa mashtaka, Abdel Maguid Mahmoud, alirudi ofisini mwake huku amezungukwa na walinzi na mamia ya mahakimu na mawaikili.
Alitaka kuonesha uhuru wake baada ya Rais Morsi kujaribu kumtoa kazini, kwa kumteua kuwa balozi wa Misri Vatikani.
Inaarifiwa kuwa majaji kadha walitishia kujiuzulu piya.
Tena mkuu wa mashtaka alikwenda kwenye mkutano na mmoja kati ya ma-naibu wa rais kujaribu kuzimua mambo.
Wakati wa serikali ya zamani kulikuwa na malalamiko mengi kuwa mahakimu na maafisa wa mashtaka wakishawishiwa na serikali.
Sasa, chini ya serikali mpya, wanajaribu sana kuonesha uhuru wao.
Hichi kisa kimeleta aibu kwa rais - na tayari kuna ishara kuwa anajaribu kubadilisha uamuzi wake wa kumtoa kazini mkuu wa mashtaka.

Wednesday, October 10, 2012

Mtetezi wa elimu Pakistan anusurika kifo



Malala Yousafzai,

Madaktari nchini Pakistan wamefanikiwa kutoa risasi kichwani mwa msichana wa miaka 14 mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Malala Yousafzai.
Hii ni baada ya msichana huyo kushambuliwa kwa kupigwa risasi hapo jana alipokuwa akitoka shuleni Kaskazini Magharibu mwa eneo la Swat.
Taarifa kutoka kwa madakatari wake zinaeleza kuwa hali ya msichana huyo iko shwari kwa sasa.
Malala alituzwa tuzo la nobel kutokana na juhudi zake za kupigania haki ya elimu kwa wasichana wa Taliban ambao kwa mujibu wa desturi za kitaliban haswa katika eneo la Swat walikuwa hawaruhisiwi kupata elimu
Ndugu yake aliambia BBC kuwa, madaktari,wangali wanatafakari ikiwa wampeleke nje kwa matibabu zaidi.
Kundi la Taliban lilisema lilihusika na shambulizi hilo.
Malala Yousafzai aliandika kitabu cha kumbukumbu zake binafsi kwa niaba ya BBC miaka mitatu iliyopita wakati eneo la Swat lilikuwa linadhibitiwa na kundi laTaliban.
Wanasiasa nchini Pakistan, walilaani shambulizi hilo huku Marekani ikilitaja kama kitendo cha uoga

Rais wa Kenya atibua njama ya wabunge



Kero la wananchi wa Kenya kwa wabunge wao
Rais wa Kenya Mwai Kibaki, amekataa kuidhinisha mipango ya wabunge wa taifa hilo kujipatia kitita kikubwa cha pesa kama marupurupu ya kuhudumu kama wabunge.
Wabunge hao walipanga kujilipa dola alfu mia moja na kumi kila mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Lakini bwana Kibaki amesema kuwa hatua hiyo inakiuka katiba na haiwezi kutekelezwa wakati ambapo walimu pamoja na madaktari nchini Kenya wamekuwa wakigoma kudai nyongeza ya mishahara.
Waandamanaji waliojawa na ghadhabu nchini Kenya walijitokeza hapo jana kulaani hatua ya wabunge hao kutaka kujilipa mamilioni ya pesa kama pesa za ziada wakati bunge litakapofunga vikao vyake kwa maandalizi ya uchaguzi mwaka ujao.
Waliwataja wabunge hao kama fisi wenye ulafi.
Wabunge wa Kenya ni baadhi ya wale wanaopokea mishahara mikubwa sana barani Afrika , wakipokea takriban dola elfu 10,000 kama mshahara kila mwezi.
Malipo hayo ya ziada ya dola 110,000 kwa kila mmoja walitaka yalipwe wakati watakapofunga vikao vyao kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2013.
Wadadisi wanasema kuwa wananchi wangetozwa kodi zaidi ili kugharamia malipo hayo ya dola milioni 23.
Hatua hii imewakasirisha watu wengi, hasa ikizingatiwa kuwa inakuja baada tu ya migomo katika sekta ya umma ambapo madaktari, walimu na hata wahadhiri wa vyuo vikuu walisusia kazi wakidai nyongeza ya mishahara.
Mswaada huo ulipitishwa siku ya Alhamisi ikiwa sehemu ya mabadiliko yaliyofanyiwa mswaada wa fedha bungeni.
Mnamo mwezi Septemba, shule za umma zilifungwa kwa wiki tatu wakati walimu walipogoma wakidai nyongeza ya mishahara na huku madaktari nao wakitaka mazingira bora ya kazi.

New