My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, October 19, 2012

HALI BADO TETE MITAA YA KARIAKOO: MABOMU YAZIDI KURINDIMA


 
Hili lilikuwa tangazo kwa ajili ya maandamano ya leo.
 
Magari ya Jeshi la Wananchi yakipita katika mitaa ya Kariakoo kuwataarifu wananchi kutawanyika eneo hilo.
Baada ya baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kutawanywa kwa mabomu na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia hapo awali, kwa sasa waumini hao wanajipanga kuvamia kituo cha polisi mtaa wa Msimbazi wakiwa katika makundi makundi mikononi wakiwa na mawe na wakiimba nyimbo. Awali magari ya Jeshi la Wananchi yalipita mitaa ya Kariakoo yakiwa na wanajeshi waliokuwa wakiamuru wananchi kutawanyika lakini hali inaonekana kubadilika maana kwa sasa waumini hao wanajikusanya upya kutimiza azma yao ya kuandamana mara baada ya kumaliza swala ya saa 10 katika msikiti wa Idrissa uliopo Kariakoo. Baadhi ya madai ya waumini hao ni KUKAMATWA SHEIKH PONDA, KUTOONEKANA KWA SHEIKH FARIDI WA ZANZIBAR NA KUKOJELEWA QURAN.

KARIAKOO DAR LEO HAKUNA MSONGAMANO WA WATU

FFU wakizunguka maeneo ya Kariakoo leo huku  wakitumia kipaza  sauti  kuwataka  wananchi wote  kurejea majumbani kwao
Hili ni eneo la Msimbazi ambalo kwa kawaida  huwa  kuna msongamano mkubwa wa  watu
Eneo la mzunguko  wa Kariakoo ambalo jiupe kama unavyoliona hapa
Hapa  sio maduka  yamefungwa  muda  umepita ama  wahusika  wamefiwa hapana ni baada ya vurugu  kutokea
Hii ni kariakoo sio biashara  mbaya ni usalama hakuna
                                       ingekuwa  vipi kama kariakoo  kila  siku  kungekuwa  hivi?

Tukio  hilo   la kukosa  watu kabisa  eneo hilo kama  picha  zinazoonyesha  limetokea  leo kutokana na vurugu  kubwa  vilizoibuka  toka majira ya mchana eneo hilo vurugu  zilizohusisha  jeshi la  polisi  kikosi  cha  kutuliza ghasia (FFU) na badhi  ya  waumini  wa dini ya kiislam ambao  wanashinikiza wenzao ambao  wanashikiliwa  kwa  tuhuma  za  kufanya  vurugu na  kupora mali  wakati  wa vurugu  za waumini  wa  dini  hiyo katika  eneo la Mbagala .
Vurugu  hizo ambazo  chanzo chake ni  watoto  kugombana na mmoja kati ya  watoto hao  wawili ambaye ni mkristo kukojolea  Msaafu  jambo  lilozua vurugu na hata  waislam kuandamana na  kuchoma makanisa .
Hivyo  kutokana na utata  huo  leo mkuu  w  mkoa  wa Dar es Salaam na kamanda  wa  polisi kamnda maalum ya Dar walionya kutokuwepo kwa maandamano  ila bado  watu sita wafuasi wa Sheikh Ponda waliokua wakiandamana kwenda Ikulu kabla ya  kukamatwa na  polisi  na  ndipo  vurugu  zilipoanza.
Wakati  vurugu  hizo  zikianza  eneo la Kariakoo  na maeneo mbali mbali ya jiji maduka na benk  zote  zilifungwa pamoja na  wananchi kutawanywa  kuondoka  maeneo hayo .
Mtandao  huu  umeshuhudia wananchi  wakitawanywa na  waliopo ndani kama ni  zaidi ya  watano  walikuwa  wakitolewa kwa  virungu huku baadhi ya  wananchi  wakijeruhiwa kwa  kukimbia vurugu na wengine kwa kupigwa na polisi na mgambo  wa  jiji.
Vipo taarifa  ambazo bado  kuthibitishwa kuwa  watu kadhaa  wamejeruhiwa  vibaya na  mali mbali mbali   ikiwemo  pikipiki  mmoja kuchomwa  moto .
Hadi mwandishi  wa mtandao huu anaondoka  eneo hilo la Kariakoo tayari magari ya wanajeshi  wa JWTZ yalikuwa  yakifika  eneo hilo  huku polisi  wakitawanywa katika misikiti mbali mbali  kuthibiti hali hiyo.
Baadhi ya  wananchi  wamemwomba  Rais Jakaya  Kikwete  kusitisha  safari  zake za nje na  kuingilia kati  kurejesha amani na utulivu nchini huku baadhi  wakidai  kuwa kitendo  kinachofanywa na  waislam hao ni  kuiharibia  dini  hiyo kwa  waumini  wake kukosa imani kwa  wananchi pindi  wanapoomba nafasi mbali mbali za uongozi  hivyo  kumwomba  kiongozi  wa waislam nchini  kutoa tamko dhidi ya haya  yanayoendelea  ili kurejesha imani kwa  watanzania.
Uchunguzi  wa mtandao  huu pia umebaini  kuwa  vurugu  hizo  zinachochew  zaidi na polisi na mgambo ambao  wamekuwa  wakiwapiga  wananchi hata  wasio na hatia na baadhi ya askari  wakizunguka maeneo mbali mbali na kuwatoa  nje  watu  waliojificha ndani ya nyumba na maduka yao bila  kuangalia na muumini wa  dini ya kiislam ama mkristo na  kuwakamata .
Moja kati ya maswali ambayo  polisi  wanapaswa  kujibia ni pamoja  na hili kuwa maandamano ya  waislam  ,wakristo wanakamatwa na  kupigwa kwa sababu  zipi? Pili kwa  waislam  kwanini wanafanya maandamano kwa jambo ambalo  lipo tayari mahakamani  ?
Mungu  ibariki Tanzania ,Mungu  wabariki  viongozi  wa Tanzania na Mungu wabariki waumini  wa  dini  zote  ili  kuifanya Tanzania  kubaki kuwa nchi ya Amani.

No comments:

Post a Comment

New