My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, October 17, 2012

Polisi wa Kenya wajeruhiwa vibaya



Polisi waliwahi kunasa mabomu na maguruneti ambayo Al Shabaab walikuwa wananuia kutumia kwa mashambulizi Kenya

Takriban polisi kumi wa Kenya wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi la guruneti
Maafisa hao wa polisi walikuwa wanasaka nyumba moja mjini Mombasa, pwani mwa Kenya ambako walipata silaha ikiwemo bunduki aina ya AK-47 na maguruneti mawili.
Msemaji wa polisi alidokeza kuwa wanamgambo wa Al-Shabab huenda walihusika na shambulizi hilo.
Kenya kwa muda sasa imakumbwa na misururu ya mashambulizi ya maguruneti, tangu wanajeshi wake walipoingia Somalia kupambana na wanamgambo wa Al Shabaab mwaka jana.

Mkuu wa Polisi mkoani humo, Aggrey Adoli,aliambia waandishi wa habari kuwa washukiwa watatu wa kigaidi waliuawa katika makabaliano kati yao na polisi baada ya shambulizi hilo.

Washukiwa wa Al-Shabab wametekeleza mashambulizi kadhaa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita eneo la Pwani ambalo ni maarufu kwa watalii.

Wanajeshi wa Kenya nao wamekuwa vitani kuondoa kundi la Al Shabaab kutoka katika ngome yao kubwa na ya mwisho ambayo ni Kismayo kwa ushirikiano na wanajeshi wa Muungano wa Afrika tangu Oktoba mwaka jana, jambo ambalo walifanikisha mwanzoni mwa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment

New