My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, February 12, 2013

Mjadala wa kwanza wa urais Kenya



Mjadala wa kwanza kati ya wagombea wa urais kuwahi kufanyika Kenya ulifanyika Jumatatu usiku kati ya wagombea 8 wanaowania wadhifa huo.
Ingawa wagombea wote walishiriki kwenye mjadala huo, kura ya maoni inaonyesha kuwa kinyang'anyiro kitakuwa kikali kati ya Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta na waziri mkuu Raila Odinga.
Akihutubia wakati wa mjadala huo Bwana Kenyatta, alisema kuwa ukabila umekuwa donda sugu ambalo limekumba nchi nzima kwa muda mrefu.
Zaidi ya watu elfu moja waliuawa wakati wa ghasia za kikabila baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007 uliokumbwa na utata.
Kenyatta anakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC, baada ya kuhusishwa na ghasia hizo. Mgombea mwenza wake William Ruto pia anatakiwa na mahakama hiyo kwa kuhusika na ghasia hizo.
Wakenya walikusanyika kwenye vituo mbali mbali kushuhudia mjadala huo. Hoja kuu kwenye mjadala huo ilikuwa swala la ICC ambalo wagombea wengine walitaka Uhuru kuelezea atakavyoongoza nchi ikiwa atapatikana na hatia kwa makosa anayokabiliwa nayo.
Kenyatta alisema kuwa haoni kama kesi yake katika mahakama ya ICC haitaathiri kwa vyovyote atakavyoongoza nchi ikiwa atashinda uchaguzi huo.
Lakini mpinzani wake mkuu Raila Odinga, alipuuza hilo akisema kuwa Uhuru atakuwa na wakati mgumu kuongoza nchi kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Skype wakati kesi yake ikisikilizwa Hague.
Wagombea wote walizungumzia swala la ukabila wakisema ni moja ya changamoto kubwa katika uongozi wa nchi kwani tatizo hilo limekita mizizi.

HATIMAYE TANZANIA YASHINDA VIVUTIO VITATU MAAJABU SABA YA ASILI AFRIKA, NI MLIMA KILIMANJARO, NGORONGORO CRATES NA MBUGA YA SERENGETI‏


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro 
Crates  muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders 
Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza 
maajabu saba ya asili ya Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye 
Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba 
hafla hiyo kamavinavyoonekana.
Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa 
wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki akisalimiana na 
Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa, Kushoto ni Mh Shah 
kutoka Mafia na mmoja wa wajumbe wa bodi ya Utalii TTB.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo 
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua 
juu juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza 
mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye 
hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya 
Seven Natural Wonders Bw. Philip Imler.
Tanzania imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii 
ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama 
ya Serengeti, hafla hiyo imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa 
ni pamoja na Mabalozi, Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la 
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka 
Mataifa mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki. Katika picha kulia 
ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja 
wa wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzaniaakiwa 
katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria pia.
Mbunge Mh. James Lembeli akisalimiana na Bw. Mike Teyrol walipokutana 
katika hafla hiyo.
Mwanamuziki Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza wakati wa 
utoaji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bi Devitha Mdachi akiwa pamoja 
na maafisa wengine wa bodi hiyo wakipokea wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza jambo 
na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na 
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi katikati ni 
msaidizi wake Bw. Miskanji.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji 
wa tuzo hizo za Seven Natural Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia 
ni Magesa Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa 
Utalii kutoka nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka 
Taasisi ya Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi 
Khamis Kagasheki.
Mkurugenzi wa Hifadhi za taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiwasikiliza 
wabunge waliohudhuria katika hafla hiyo kulia ni Deo Filikunjombe na 
kushoto ni David Kafulila.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii 
Dk. Aloyce Nzuki wakati alipowasili kwenye hoteli ya Maount Meru kwa 
ajili ya utoaji tuzo hizo.
Mama Tunu Pinda wa pili kutoka kushoto akiwa katika hafla hiyo, kulia ni 
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk Aloyce Nzuki na katikati 
 ni Lynn Imler kutoka Seven Natural Wonders.
Mabalozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia 
ni Balozi Mutinda Mutiso Balozi wa Kenya Nchini Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge 
wa jimbo la Arusha Mjini Bw. Godbless Lema  kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB)  Dk. Aloyce Nzuki 
akiongea katika hafla hiyo.
Bw Allan Kijazi kushpto akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crates
 Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi  katika hafla hiyo,
 kushoto ni Philip Imler wa Seven Natural Wonders.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiongea 
katika hafla hiyo.
muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders 
Bw.Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.
Tuzo ya mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo 
kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.



Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii 
akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya 
Mount Meru jijini Arusha.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana 
kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
 Balozi wa Kenya nchini Tanzania akizungumza na Balozi Charles Sanga
 Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB na Mkurugenzi wa bodi 
hiyo Dk. Aloyce Nzuki wakati wa hafla hiyo.

New