My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, March 13, 2013

Moshi mweusi Vatican, Bado hajapatikana Papa




Moshi mweusi Vatican
Moshi mweusi umetokea kwenye dari la hekalu ya Sistine mjini Roma, kumaanisha kuwa makadinali walioko ndani ya hekalu wameshindwa kuafikiana juu ya Papa mpya anayetarajiwa kuchaguliwa.
Moshi mweupe utaashiria kupatikana kiongozi mpya wa kanisa Katoliki la Roma.
Makadinali hao wanatarajiwa kupiga kura mara nne kwa siku hadi pale thuluthi mbili ya makadinali wote watakapoafikiana juu ya Papa mpya.
Walipiga kura yao ya kwanza ambayo haikuleta maafikiano hapo usiku wa Jumanne. Yeyote atakayeteuliwa kuliongoza kanisa hilo katoliki anakabiliwa na wakati mgumu, ambapo kanisa limezongwa na kashfa mbali mbali pamoja na migawanyiko ya ndani.
Papa aliyeondoka Benedikt wa Kumi na sita aliwashangaza wengi alipotangaza kujiuzulu wadhifa huo miaka minane tu tangu kuchaguliwa. Yeye ndiye Papa wa kwanza kujiuzulu katika miaka 600 ya historia ya kanisa hilo.
Alitoa sababu kuwa amezeeka na afya yake imedhoofika kwa hivyo haoni kuwa anaweza kutekeleza wajibu wake kikamilifu kama Papa wa kanisa


 
Moshi mweusi umetokea kwenye dari la hekalu ya Sistine mjini Roma, 
hii inamaanisha kuwa makadinali walioko ndani ya hekalu wameshindwa kuafikiana juu ya Papa mpya anayetarajiwa kuchaguliwa.
Moshi mweupe utaashiria kupatikana kiongozi mpya wa kanisa Katoliki la Roma.
Makadinali hao wanatarajiwa kupiga kura mara nne kwa siku hadi pale theluthi mbili ya makadinali wote watakapoafikiana juu ya Papa mpya.
Walipiga kura yao ya kwanza ambayo haikuleta maafikiano jana usiku wa Jumanne. Yeyote atakayeteuliwa kuliongoza kanisa hilo katoliki anakabiliwa na wakati mgumu, ambapo kanisa limesongwa na kashfa mbali mbali pamoja na migawanyiko ya ndani.
Papa aliyeondoka Benedikt wa Kumi na sita aliwashangaza wengi alipotangaza kujiuzulu wadhifa huo, Alitoa sababu kuwa amezeeka na afya yake imedhoofika kwa hivyo haoni kuwa anaweza kutekeleza wajibu wake kikamilifu kama Papa wa kanisa

Thursday, March 7, 2013

CORD wadai kuna hujuma kwenye uchaguzi Kenya



Idadi kubwa ya wakenya walipiga kutrra ambayo hadi sasa wangali kujua matokeo ya urais
Mgombea mwenza wa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, amesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha kuwa kuna hujuma dhidi yao katika dhughuli ya kuhesabu kura inayoendelea katika ukumbi wa Bomas, na kwamba shughuli hiyo inastahili kusitishwa.
Hata hivyo alisema kuwa haina maana kuwa wanaitisha maandamano.
Shughuli ya kuhesabu kura ingali inaendelea ingawa kwa mwendo wa kinyonga baada ya tume hiyo kutupilia mbali mitambo yake ya kuhesabu kura baada ya kugoma.
Uhuru Kenyatta angali anaongoza kwa idadi ya kura za wagombea wa urais akiwa na kura 2,660,379 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliye na kura 1,996,181 lakini matokeo rasmi yatajulikana tu mwishoni mwa juma.
Taharuki imetanda na kuna hali ya wasiwasi kwani tume ya uchaguzi haijatangaza matokeo ya urais zaidi ya masaa arobaini na nane tangu wakenya kupiga kura.
Muungano wa CORD umesema kuwa unatafakari hatua za kuchukua baada ya kudai hujuma katika shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura za urais.
Shughuli hiyo imekumbwa na utata hasa baada ya mitambo ya kuhesabu kura ya tume ya uchaguzi kukumbwa na hitilafu.
Hatua hii imelazimu tume hiyo kuanza kuhesabu kura upya katika kitovu cha kupokea matokeo ya kura za urais kwenye ukumbi wa Bomas viungani wa mji wa Nairobi.
Kalonzo Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa Raila Odinga, amehutubia waandishi wa habari mjini Nairobi na kusema kuwa muungano wa CORD, unataka shughuli hiyo ya kuhesabu kura za urais kusitishwa mara moja na kuanzishwa upya wakitumia stakabadhi kutoka kwa makarani wa kura jambao ambalo linafanywa kwa sasa
Musyoka vile vile amesema kuwa muungano huo una tashwishi kuhusu baadhi ya matokeo wakisema sio ya kweli kwa kuwa hayawiani na yale waliyoyaleta maajenti wao.
Aliendelea kwa kusema kuwa baadhi ya matokeo yako juu kuliko idadi ya wapiga kura katika baadhi ya maeneo ambako kura zilipigwa.
Musyoka amesisitiza kuwa tatizo hilo limetokana na kugoma kwa mitambo ya kupiga kura na pia kuanza upya kwa shughuli ya kuhesabu kura kwa kutumia mfumo wa zamani.
Musyoka alisema kuwa tume ya uchaguzi inastahili kutumia mitambo ya elektroniki kuhesabu kura kama inavyoagiza katiba ya nnchi, huku akiongeza kuwa muungano huo ungali unatafakari hatua za kuchukua ingawa kwa kufuata sheria.
Moja ya hatua inazotafakari kuchukua ni kwenda mahakamani kuitaka mahakama kusimamisha shughuli ya kuhesabu kura na kuanza tena.

New