My Web

Emmanuel

CONTACT

Saturday, December 31, 2011

Dhana hizi zinawaharibia wanawake kimapenzi 4

Wiki hii tunaendelea na sehemu nyingine ya mada yetu ya dhana zinazowaharibia wanawake kimapenzi ikiwa ni mwendelezo wa pale tulipoishia wiki iliyopita.

Ukiacha mateso ya Janette baada ya kutoswa na Mully aliporudi mara ya pili, Jambo la kuzingatia ni jinsi alivyomtenda boyfriend wake aliyekuwa anamhudumia na kwenda kuangukia kwa mwanaume ambaye ni mume wa mtu. Hakutafakari mwenye faida kwake ni nani, leo anahangaika.

Aina ya wanawake kama Janette ndiyo wanaosababisha wanaume watambe mitaani wakitoa maneno ya kebehi kwamba wanawake wote mwalimu wao ni kipofu. Hakutambua jema wala hakujua kwenye maisha haya anahitaji nini.

Mtu anayejihusisha kimapenzi na mume au mke wa mtu, maana yake hajui kesho yake ni nini.

Mully ni mmoja wa waathirika, wapo wanaume wengi waliotendwa na wapenzi wao ambao waliwalea na kutumia fedha nyingi kuwasomesha. Mambo yao yalipokaa sawa na kupata kazi, wakasahau walipotoka na kuanzisha uhusiano na wengine. Kipya kinyemi, mume aliyemsomesha akatupwa mbali.

Janette na wengine wenye tabia za namna hiyo ni mwendelezo wa dhana zinazowaharibia wanawake kimapenzi. Wanatakiwa wajirekebishe ili mambo yakae sawa. Wasiwaponze wengine wenye tabia safi, wenye akili hai za kulea familia yenye mafanikio tele.

Ipo dhana nyingine kuwa mwanamke akipendwa sana, hujenga kiburi na matokeo yake humdharau mwanaume anayeonesha mahaba ya ndani kabisa. Kwamba anaweza kumgeuza mwanaume punda kwa sababu tu anajua anampenda.

Hachukulii upendo ni tunu, yeye anaubeba kama fimbo ya kuchapia.

Nimeshakutana na watu kadhaa, wananieleza matatizo yao na jinsi walivyoshauriwa na watu mbalimbali. Mathalan, mtu mke wake anamsumbua, anamueleza mshauri kila kitu kinachozunguka mgogoro ndani ya familia yake. Mwisho katika kushauriwa anaambiwa: “Tatizo, umemuonesha mkeo unampenda sana.”

Je, kumuonesha mtu kuwa unampenda ndiyo igeuke adhabu kwako? Ni wazi kuwa mapenzi ya siku hizi, yanatawaliwa na nguvu kubwa ya shetani ndiyo maana tafsiri yake inakosewa. Ukweli wa mapenzi ni kuwa wawili wanaoamua kupendana ni lazima upendo wao uwe wa ndani ya nyoyo zao na waudhihirishe kwa vitendo.

Ni mateso kujilazimisha kuficha mapenzi, eti unahofia ukimuonesha atajua na atakufanyia vitimbi. Kufanya hivyo ni mateso, bora kutopenda kabisa. Inatupasa kupendana bila kuwa na shaka yoyote ndani. Kila mtu ausikilize moyo wake namna unavyomuongoza na atende pasipo kuhofia kuitwa Bushoke.

Wakati nashauri kwa watu kuruhusu nyoyo zao ziwaongoze katika kudhihirisha mapenzi yao bila kuogopa jinsi watakavyochukuliwa na jamii, ni vema nikatoa angalizo kwa wale wanaooneshwa mapenzi, kuheshimu hisia za wenzao. Maisha ya sasa, kupata mtu anayekupenda, anayekujali na kukuheshimu kwa dhati, ni bahati.

Ukigundua ni bahati, basi ni vizuri kuitunza kwelikweli, vinginevyo unaweza kuichezea, ukaipoteza, matokeo yake ni kujuta baadaye. Usimfanye mwenzi wako ashindwe kukuonesha penzi la dhati. Mpe uhuru na amani juu yako. Mpokee vizuri, zungumza naye kwa lugha tamu ili ajisikie kuwa nawe.
Ni vipi mwenzio kwa mapenzi aamue kukununulia zawadi aliyoona inafaa, wewe kwa sababu unamdharau kutokana na jinsi anavyokupenda kupitiliza, unaitazama kwa nyodo kisha unapotezea. Husemi hata asante. Inawezekana inakuvutia lakini hutaki tu kumuonesha kwa sababu unamuona katuni, kisa anakupenda kupitiliza.
Mwenzio ametulia, anaona akutoe ‘auti’, mwende sehemu mkapate chakula cha jioni. Hisia zako za dharau juu yake, iliyotokana na mtazamo kuwa anakupenda mpaka kero, unaamua kukataa bila sababu: “Sitaki tu kwenda, acha nipumzike nyumbani.”

Dar LIve

Na Luqman Maloto
Baada ya tafsiri iliyotawala muda mrefu kuwa Wilaya ya Temeke, ipo nyuma katika mambo ya burudani ndani ya Jiji la Dar es Salaam, sasa hivi imekuwa tofauti kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa ukumbi mkubwa wa kisasa wenye hadhi ya kimataifa unaoitwa Dar Live.
Ukumbi huo ambao ni wa kwanza kuwahi kutokea ndani ya Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla, umejengwa eneo la Mbagala, Zakhem, wilayani Temeke.
Dar Live, umejengwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd ambayo imejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi katika sekta ya habari na uandaaji wa matamasha makubwa kama vile, Mfalme wa Rhymes, Champions Day na mengineyo, bila kusahau lile la kuhamasisha uzalendo kwa Watanzania lililofanyika hivi karibuni.
Akiutambulisha ukumbi huo kwa waandishi wa habari juzi, Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, alisema kuwa Dar Live ni ukumbi wa aina yake, utakaojishughulisha na utoaji wa huduma za matamasha ya muziki, disko, sherehe za harusi, michezo ya watoto, mikutano na vinywaji.
Alisema, ukumbi huo ni fahari ya Mbagala na Temeke yote, hivyo aliwataka wakazi wa eneo hilo kuanza kujivunia, kwani sasa watakuwa wanapata burudani ya uhakika nyumbani, tofauti na mwanzo walipokuwa wanalazimika kufunga safari hadi Wilaya za Kinondoni na Ilala.
“Pamoja na uwepo wa vifaa vya huduma za michezo ya watoto, kingine ni kwamba Dar Live tumefunga jukwaa kubwa la kisasa la kudumu. Jukwaa ambalo linakidhi mahitaji ya shoo yoyote ya kimataifa.
“Jukwaa limekamilika, lina taa za kutosha, sound (muziki) yenye ujazo mkubwa. Siyo kama kumbi nyingine ambazo hulazimika kukodi majukwaa na muziki. Dar Live imekamilika kila idara. Pamoja na yote hayo, pia kuna bwawa la kuogelea,” alisema Mrisho.

WANAMUZIKI WAKUBWA KUPAMBA UZINDUZI
Mrisho alisema kuwa Dar Live utazinduliwa Januari Mosi, 2012, kuanzia saa 4:00 asubuhi na sherehe za uzinduzi zitakamilika saa 6:00 usiku.
Alisema, kufanikisha uzinduzi huo, wanamuziki wakubwa nchini, watafanya shoo kubwa, itakayoendana na hadhi ya ukumbi wenyewe.
Aliwataja wanamuziki watakaotumbuiza siku hiyo kuwa ni Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’ na Kundi lake la Wanaume Halisi, mkongwe Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Kundi la Gangwe Mob likiongozwa na Haroun Kahena ‘Inspector’ pamoja na vijana chipukizi wakali wa Kundi la JNY Unit.
Aliongeza, kwa upande wa dansi, Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, ikiongozwa na Ali Choki ‘Mzee wa Farasi’ itafanya kazi nzuri ikiwatumia rapa Saulo John ‘Ferguson’, wanenguaji Aisha Mbegu ‘Madinda’, Hassan Musa ‘Nyamwela’ na wengine wengi.
Kwa upande wa burudani ya Taarab, Mrisho alisema kuwa Kundi la Jahazi Modern Taaarab, likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf, litasababisha mirindimo ya Pwani.
Mrisho alitaja viingilio vya siku hiyo kuwa ni shilingi 10,000 kwa VIP, kawaida ni shilingi 5,000 na shilingi 1,000 kwa watoto.
“Watoto wao watafurahia uzinduzi kuanzia asubuhi mpaka saa 12:00 jioni, watu wazima wao kazi kwao kusherehekea matunda ya Dar Live mwanzo mwisho,” alisema Mrisho.
Kuna la ziada? Mbagala wapewe nini wakati wao kesho ndiyo Alfa na Omega?

wolper ala Kristmasi kitandani

Na Erick Evarist

Sura ya mauzo kunako Bongo Movie, Jacqueline Wolper amejikuta akila Sikukuu ya Krismasi kitandani baada ya kushindwa kujikinga na ‘anopheles’ mdudu anayeambukiza ugonjwa wa Malaria.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu na nyota huyo zinasema Wolper alibanwa na homa hiyo kiasi cha kushindwa kutoka nje hivyo kuisikia sikukuu kwenye redio tu.

“Duh! Jamani shosti ‘angu ameshindwa ku-enjoy sikukuu na hivi ninavyomjua anapenda kujiachia, lo!” alisema rafiki wa karibu wa Wolper.

Akizungumza kwa tabu kwa njia ya simu na paparazi wetu, Wolper alikiri ‘kupigwa’ na malaria siku hiyo na kudai kwa sasa hajambo, anaendelea vizuri baada ya kutumia dozi.

“Kwa sasa naendelea vizuri kwa kweli, namshukuru Mungu, lakini nilikuwa hoi sikukuu yote hii,” alisema Wolper.

Diamondi

Na Luqman Maloto

Ushamba wa mapenzi alionao dogo ‘mgonjwa’ wa warembo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ (pichani), umekwenda hatua mbaya zaidi, alichokifanya Uingereza hivi karibuni, kimeshusha thamani yake kutoka geji hafifu hadi sifuri.

Akiwa Uingereza, Diamond alibwabwaja maneno ‘mbofumbofu’ ambayo siyo tu kwamba yalimfanya azomewe jukwaani, bali pia yaliwadhalilisha warembo wenye majina makubwa Bongo, Wema Sepetu na Jokate Mwegelo.

Inadaiwa kuwa Diamond akiwa katikati ya shoo kwenye ukumbi mmoja jijini London, alisimamisha muziki halafu akawaambia mashabiki waliohudhuria, wamchagulie mpenzi wa maisha yake, kati ya Wema na Jokate.

Madai yanaanikwa kwamba kitendo hicho, kiliwakera mashabiki ambao walilipuka na kumzomea, huku wengi wakimponda kwa kumwita limbukeni wa mapenzi, anayetumia umaarufu wake vibaya kuwachezea warembo.

Mashabiki mbalimbali wametoa maoni kwamba kauli ya Diamond kuwa hamjui mpenzi wake kati ya Wema na Jokate, inatosha kuchangamsha ubongo wa warembo hao ili wajivue gamba mapema na endapo wataendelea naye, basi nao wataonekana ni sifuri.

Dongo hilo la mashabiki, linanogesha kama siyo kusherehesha msemo kuwa mia halali kitanda kimoja na nunge, siku zote ziro huchangia shuka na sifuri kwa sababu ndiyo wanaofanana kuanzia thamani mpaka umbile.

Kwa upande mwingine, kauli ya Diamond imeibua mjadala mkubwa kwenye mitandao mbalimbali, huku kipande cha video, kinachomuonesha ‘dogo huyo mpenda sifa’ akibwabwaja jukwaani kikisambazwa kwa fujo kupitia intaneti na kuchangiwa maoni ya kufuru.

Kuweka pamoja maelfu ya maoni yaliyotumwa, wachangiaji wamemwita Diamond ni mchafuzi wa watoto wa kike, hana mapenzi ya kweli, gusa unate, mkuki popote na mengineyo ambayo hayana tafsiri nzuri kwa ‘dogo huyo’ aliyekulia Tandale, Dar.
Promota mmoja wa Uingereza (jina tunalo), aliliambia gazeti hili kuwa alipanga kumpa shoo tatu Diamond katika majiji ya Leads, Swansea na Leiceste lakini aliahirisha baada ya kuona amewachafua mashabiki na hakubaliki tena.

NI TUSI KUBWA KWA WEMA
Oktoba 2, 2011, Diamond kwa utashi wake, bila kulazimishwa, alijishaua kumvisha pete ya uchumba, Wema ambaye ni staa wa filamu mwenye taji la Miss Tanzania 2006-07.

Diamond, alimvalisha pete Wema na kuahidi kufunga naye ndoa katika tukio kubwa la shoo ya siku yake ya kuzaliwa, iliyochukua nafasi ndani ya New Maisha Club, Masaki, Dar es Salaam.

Wakati Diamond anautangazia ulimwengu kuwa Wema ndiye mke wake mtarajiwa, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili 2006-07, alikuwepo.

Kwa mujibu wa watoa maoni, tusi kwa Wema ni kuwa kumbe alivishwa pete kanyaboya isiyo na mapenzi ya moyoni, kama ni mpira, basi alipangwa kikosi cha kwanza kwa ajili ya kumshikia nafasi mchezaji mwenye namba yake.

UKWELI NI UPI?
Jokate anaendelea kusisitiza kwamba hajawahi kukwea kitandani na Diamond, isipokuwa yupo karibu na ‘bwa mdogo’ huyo mpenda wa’mama kwa ajili ya kazi tu.

Wema anadai anao ushahidi kuwa Jokate kaanguka dhambini, wakati huo huo Diamond naye anajichetua ili aonekane kidume cha mbegu kwa kuomba mashabiki wamchagulie anayefaa.

HESHIMA YA JOKATE
Kabla ya tukio hilo, Jokate ni mrembo maarufu ambaye heshima yake kwenye jamii ilikuwa juu kutokana na jinsi alivyoendesha mtindo wa maisha yake.

Tathmini inaonesha kuwa tangu alivyoanza kuhusishwa kutoka kimapenzi na Diamond, heshima yake imepungua, huku watu wengi wanaompenda wakisema kwamba mrembo huyo ameingia ‘chaka’.

Kitendo cha Diamond kumuweka mezani na Wema, kisha kumchezesha bahati nasibu kama atashinda au la, kimezidi kuporomosha heshima ya Jokate.

Mrembo huyo ambaye amekuwa akifanya kazi nyingi za harakati, ameshauriwa kuwa hadhi yake ni kubwa, hivyo haipendezi kugombania sadakalawe na Wema ili kumpata Diamond.

KUTOKA RISASI
Wema na Jokate, kama kuna makosa ambayo mmefanya ni wakati wenu kujisahihisha. Mungu amewajaalia vipaji na nyota za umaarufu, haivutii mkatumiwa bila heshima mithili ya vitanda vya nyumba za kulala wageni.

Maisha yenu ni mazuri endapo mtaamua kushika yenye faida. Kwa Diamond, vema akajikosoa, umri wake ni mdogo, kwa hiyo anatakiwa kuzingatia kwamba anaweza kuzunguka mabucha nyama ni ileile. Akidanganywa na ujana, fainali uzeeni.

Kasheshe BBM

Na Mwandishi Wetu

Ujio wa mtandao mpya wa kijamii kupitia simu za mkononi aina ya BlackBerry almaarufu BBM, sasa umezua kasheshe miongoni mwa mastaa wa Bongo waliojisajili kwenye huduma hiyo.

Kasha la upekuzi wa gazeti hili limesheheni habari mbichi za hivi karibuni kuwa, chokochoko, ugomvi na kumalizana kistaa, shetani wake ni meseji za umbeya zinazotundikwa na wadau wa mtandao huo.

UNATAKA KUJUA ZAIDI?
Habari zisizokuwa na chenga kutoka kwa baadhi ya wanachama wa BBM zinafafanua hivi: “Mtandao huu unawachonganisha sana mastaa na hasa akina dada, utakuta mtu anakutungia jambo na kuliweka kwenye ukurasa wake, lengo likiwa ni kukuharibia.

“Wanaosoma posti hiyo ya umbeya wanaamini, wanaanza kukutukana au kukudhalilisha, matokeo yake ni kuwekeana bifu zisozokuwa na msingi,” alisema Jane Abbas, mtumiaji wa BBM ambaye pia ni mwigizaji chipukizi.

VIONJO VYA MESEJI ZA BBM
Hakuna ubishi kwa sababu, timu ya Gazeti la Risasi mchanganyiko imeshuhudia baadhi ya meseji za vijembe vya baadhi ya mastaa zikisomeka: “Msanii maarufu hawezi kuishi Manzese (eneo moja jijini Dar). Usipende kuiga tembo we mwanamke. Mzuri atakuwa yeye?”

Inaelezwa kuwa maneno yenye sura hiyo huwa ni sawa na dongo gizani, atakayelia na kujibu kwa jazba ujue ujumbe umemgusa na kutoka hapo mtafutano wa kitemi huanza safari zake.

HITIMISHO
Mbali na matumizi hayo mabaya ya mtandao huo, wapo baadhi ya watu ambao hutumia BBM kuhabarishana ishu za kijamii na hivyo ‘kuwakipu bize’ muda mwingi. Mfano ni picha za ukurasa wa mbele ambazo mastaa walipigwa siku moja wakati Irene Uwoya akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa yaani birthday.

Tuesday, December 20, 2011

Babu miaka 7 jela

Na Makongoro Oging’

Mchungaji Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’ wa Samunge, Loliondo, Arusha, atapanda kizimbani kukabili kesi za madai na jinai, hii ni kwa mujibu wa wakili maarufu, Mabere Nyaucho Marando.

Wakili huyo alisema, endapo mahakama itamkuta na hatia ya kutenda jinai, Babu Ambi, anaweza kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka saba jela.

Marando alisema, kesi ya jinai ambayo Babu Ambi anafunguliwa ni ile ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kwamba aliwahadaa watu kuwa dawa yake inatibu, wakati hakuna mtumiaji aliyepona.

Aliongeza kuwa kesi ya madai, inafunguliwa kwa sababu anatakiwa alipe fidia za watu waliopoteza maisha na wote waliosafiri kutokana sehemu mbalimbali wakitumia gharama kubwa kwa dawa isiyotibu.

Marando alifafanua, Babu Ambi, anaweza kukumbana na kifungo hicho endapo atakutwa na hatia kutokana na sheria ya jinai namba 302.

“Nipo makini na suala hili, hawezi kupona, nitasimamia kesi na tutamfunga,” alisema Marando na kuongeza:

“Nina taarifa nyingi kuhusu watu waliokufa, hakuna aliyepona.

Mazingira ya kisheria, yanatoa picha rahisi kuwa Babu atakutwa na hatia.”

Kutokana na msimamo huo, Marando aliwataka wale wote waliotibiwa na Babu Ambi lakini hawakupona, waende kwake kwa sababu amedhamiria kuisimamia kesi hiyo.

“Kiukweli babu aliwadanganya watu kuwa anatibu magonjwa sugu, lakini watu walipokwenda na kupata kikombe, hawakupona, na hawezi kuthibitisha mahakamani kuwa dawa yake imethibitishwa na serikali kuwa inatibu magonjwa aliyoyasema,” alisema Marando.

Aliongeza kuwa yupo tayari kuandaa kesi hizo na ndugu wote waliokunywa dawa na hawakupona, wanaweza kwenda kwake ili wakusanye ushahidi wa kutosha.

“Ni jambo linaloumiza, nitasimamia kesi hiyo na nitahakikisha anafungwa si chini ya miaka saba kama sheria inavyosema...ama zake ama zetu, alisababisha wagonjwa wa Ukimwi kuacha kutumia ARV, wengine wakatoroka hospitalini kwenda kwake na wengi wamepoteza maisha,” alisema Marando.

Wakili huyo aliigeukia serikali na kuilaumu kwa kumruhusu Babu kuwapa dawa watu wakati ikijua kuwa ilikuwa haijafanyiwa majaribio ya kitaalamu kujua kuwa kama inatibu au la.

Alisema anaweza kumfungulia kesi ya madai mchungaji huyo kwa kuwa wagonjwa wengi waliuza mali au kuchukua akiba zao na kusafiri hadi Samunge wakijua kuwa watapona baada ya kunywa dawa yake.

“Badala ya kupona wengi walifariki dunia huku wengine wakibaki masikini na hawajapona kutokana na udanganyifu mkubwa uliofanywa na Babu huyo na sasa hawawezi tena kupata mali nyingine,” alisema Marando.

Mwanasheria mwingine, Dk. Ngali Maita alipohojiwa kwa simu alisema atakuwa tayari kumsaidia mawazo ya kisheria Marando ikiwa atahitajika kwa kile alichodai, Babu alidanganya watu kuhusu tiba ya kikombe.

“Ni kitu kibaya sana alifanya Babu wa Loliondo, amesababisha maafa makubwa kwa jamii na mbaya zaidi hadi sasa uchunguzi wa dawa yake upo gizani, serikali haisemi chochote licha ya kuahidi wananchi kuwa watataarifiwa… hii ni mbaya na ni hatari,” alisema Dk. Ngali.

WAGANGA WA DAR
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Waganga wa Tiba Asilia jijini Dar es Salaam, Maneno Tamba alisema alishangazwa sana na serikali kumruhusu Babu kufanya tiba bila kufuata sheria ya tiba asili ya mwaka 2002.

“Sifa za kutibu kiasili zimebainishwa na sheria, kwamba pamoja na sheria nyingine mtoa dawa ni lazima awe chini ya mganga wa jadi kwa miaka mitatu ndipo anaweza kusajiliwa.

Je, Babu alisajiliwa? Inafaa ashitakiwe,” alisema Tamba.

TAMOPHA
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (Tamopha), Julius Kaaya alilithibitishia gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita alipohojiwa kwa njia ya simu kuwa, wanachama wake 14 waliopelekwa kwa Babu kutibiwa kwa majaribio, hakuna hata mmoja aliyepona.

ALICHOSEMA BABU
Babu wa Loliondo alijipatia umaarufu mapema mwaka huu baada ya kutangaza kwamba amezungumza na Mungu kwenye ndoto na kumuonesha dawa inayoitwa Mugariga inayotibu Ukimwi, Kisukari, Moyo, Kifafa na magonjwa mengine sugu.

Mchungaji Masapila alisema dawa yake ambayo ni dozi ya kikombe kimoja ilikuwa na gharama ya shilingi 500, hali iliyofanya maelfu ya watu wakiwemo mawaziri, wabunge na wafanyabiashara kwenda kwake huku wakitumia magari na wengine kukodi helikopta.

Hivi sasa idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa huko ni ndogo sana na Babu anadai hali hiyo imetokana na kupigwa vita na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa jadi.


SAkata la ukosefu wa Mafuta Dar

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye foleni ya mafuta katika Kituo cha Mafuta cha Bamaga, Mwenge jijini.

Jamaa huyu anaonekana akilalamika akiwa kwenye foleni hiyo.

Baadhi ya madumu ya kuchukulia mafuta yakiwa yamepangwa kwenye foleni na wateja, tayari kwa kutiwa mafuta iwapo yatapati.…

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye foleni ya mafuta katika Kituo cha Mafuta cha Bamaga, Mwenge jijini.
Jamaa huyu anaonekana akilalamika akiwa kwenye foleni hiyo.
Baadhi ya madumu ya kuchukulia mafuta yakiwa yamepangwa kwenye foleni na wateja, tayari kwa kutiwa mafuta iwapo yatapati.
Magari yakiwa kwenye msululu wa kugoja kujaziwa mafuta.

SAKATA la kuadimika kwa nishati ya mafuta nchini limeibuka tena leo, ambapo wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameendelea kuhangaika kutafuta nishati hiyo bila mafanikio.

Tatizo hilo linazidi kuipaka matope Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), kufuatia kutoweka wazi tatizo linalosababisha upatikanaji wa mafuta katika vituo mbalimbali.

Baadhi ya wateja wa nishati ya mafuta ya petroli na dizeli leo wamelalamikia utaratibu wa vituo vya mafuta kuendelea kugoma kuwauzima nishati hiyo kwa madai ya kwisha katika vituo vyao.

“Inanikela sana hali ni mbaya maana nimetafuta mafuta tangu asubuhi sijapata, na nikiangalia sababu hata sielewi, nini kinachowafanya Ewura kutosema tatizo kwetu wateja wao ili tusisumbuke?” alihoji mkazi mmoja huku mwingine naye akilalamika kuwa:

“ Hawa Ewura hawafai kabisa, yaani leo wamenifanya kutoenda kazini kwa ajili ya kuhangaika huku na kule kutafuta mafuta, huwezi kuamini, gari limenizimikia Sinza Mugabe na sasa niko hapa kituo cha mafuta Bamaga tangu saa tatu asubuhi na mafuta sijapata, wauzaji wanatuyeyusha tu.” Alisema mkazi huyo.


WEMA ana kidole Gundu

Na Mwandishi Wetu

Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu ametajwa kuwa na kidole chenye gundu.

Kidole cha Wema kinachotajwa kuwa na gundu ni kile cha pete kwa maelezo kuwa kila akivalishwa pete ya uchumba hufarakana ndani ya muda mfupi.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Wema huwa na bahati ya kung’ara kwenye uhusiano wa kawaida lakini uchumba ni mzito.

Ripoti ya uchunguzi huo inanyevua kuwa wanaume watatu ambao Wema amewahi kuvaa pete zao za uchumba, wote alitibuana nao muda mfupi baada kumvalisha madini kwenye kidole.

Katika safari ya mapenzi, Wema ameshavaa pete za wanaume watatu, mjasiriamali, Jumbe Yusuf, mwanamuziki wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel Mbwana ‘Charlz Baba’ na mwana-Bongo Fleva, Naseeb…

Na Mwandishi Wetu

Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu ametajwa kuwa na kidole chenye gundu.

Kidole cha Wema kinachotajwa kuwa na gundu ni kile cha pete kwa maelezo kuwa kila akivalishwa pete ya uchumba hufarakana ndani ya muda mfupi.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Wema huwa na bahati ya kung’ara kwenye uhusiano wa kawaida lakini uchumba ni mzito.

Ripoti ya uchunguzi huo inanyevua kuwa wanaume watatu ambao Wema amewahi kuvaa pete zao za uchumba, wote alitibuana nao muda mfupi baada kumvalisha madini kwenye kidole.

Katika safari ya mapenzi, Wema ameshavaa pete za wanaume watatu, mjasiriamali, Jumbe Yusuf, mwanamuziki wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel Mbwana ‘Charlz Baba’ na mwana-Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’.

JUMBE
Wema alipoanza mahaba na Jumbe, ikawa patashika. Nchi nzima ikatambua kwamba mtoto huyo wa Balozi Isaac Abraham Sepetu, yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na kijana wa Kingazija, Jumbe.

Kumbukumbu zinafunua kuwa kutokana na kukolea kimapenzi, wakaishi pamoja Tabata, Dar es Salaam.

Data zinaonesha kuwa baada ya kuishi kwa muda mrefu kidogo, huku wakiitana mke na mume, waliamua kuvuka hatua moja kwa Jumbe kumvisha pete ya uchumba Wema.

Hata hivyo, pete hiyo haikuwa na matunda, kwani baada ya mwezi mmoja, waliachana.

CHARLZ BABA
Wema alipoachana na Jumbe, alijirusha kwa muda na Mkurugenzi wa Hartmann Production, Hartmann Mbilinyi kabla ya kutua kwa Charlz ambaye aling’ara naye kiasi kwamba zikaibuka taarifa kuwa watafunga ndoa.

Kuthibitisha upendo wake, Charlz alimvalisha pete ya uchumba ambayo iliibua matokeo mabaya pia, kwani muda mfupi baadaye Wema alikwenda Marekani na akiwa huko alivunja uhusiano na mwana Twanga Pepeta huyo, aliporudi nchini alitua moja kwa moja kwenye mikono ya Diamond.

DIAMOND
Walikuwa kama watoto, wakijifungia ndani wanapiga mapicha ya denda na mapozi mbalimbali ya kimahaba.

Dhahiri, ilionekana wanaendana, kwa hiyo kilichosubiriwa ikawa ndoa. Kukaribisha hatua hiyo, Diamond aliitumia siku yake ya kuzaliwa kumvalisha pete Wema ndani ya New Maisha Club.

Kama kawaida, balaa likafuata baada ya pete, kwani wiki moja na nusu baadaye, Diamond alitangaza kuachana na Wema kwa madai kwamba ni mvivu kwenye kazi za nyumbani, vile vile hampendi mama yake.

Pamoja na Wema kuomba msamaha na kurudiana kwa shinikizo la mama wa Diamond, imeonekana ‘bwa mdogo’ huyo alishaamua kuangalia mbele, kwani hivi karibuni yameibuka madai kwamba yupo katika uhusiano wa kimapenzi na Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006-07, Jokate Mwegelo.

WEMA
Katika maelezo yake kuhusu kuachana na wanaume wake, alisema kuwa jamii humuona ni malaya lakini ukweli ni kwamba hujitahidi kuvumilia na anapoinua mikono maana yake ameshindwa kwa njia zote.

Hii inamaanisha kuwa Wema anaamini matatizo yapo kwa wanaume wake ambao huwavumilia mno lakini mwisho hushindikana.


New