My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, November 28, 2011

kupandisha posho za wabunge ni ukuchaa

Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.

Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.

Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hili.

Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za vikao. Popote ninapohudhuria vikao huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho. Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu. Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?

Tazama nchi hii, juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.

Tanzania inaagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine.

Ipo siku Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao.

http://zittokabwe.wordpress.com/

Kilichotokea Dodoma kwenye vikao vya CCM - Tafsiri yangu

Ndugu zangu
Waafrika sisi tu mahodari sana wa kufunga safari, lakini, huwa hatupangi safari. Kuna tofauti ya kufunga safari na kupanga safari. Kuna tofauti pia ya kuwa na mipango na mikakati na kuwa na mipango na mikakati sahihi.
Mara nyingi wenye kupanga safari zao, na hata kuwa na mipango na mikakati sahihi hufanikiwa zaidi. Na ndivyo ilivyo kwenye siasa.

Kule Dodoma tumeshuhudia ’ Vita vya wenyewe kwa wenyewe’ ndani ya CCM. Inahusu safari ya kuelekea 2015, na si kitu kingine. Kule Dodoma CCM hawakutoka WaMOJA . Wametoka kwenye mapande makubwa mawili na mafungu mengine madogo madogo.

Na CCM ya sasa ina makundi, walau hili wamekiri rasmi CCM wenyewe. Na kwenye kuelekea 2015 tunayaona makundi makubwa mawili; lile linaloongozwa na Edward Lowassa na la akina Samwel Sitta. Kule Dodoma tumeushudia mnyukano wa wazi wa makundi haya yakiwahusisha pia vijana wa chama hicho.

Yote haya yanatoa fursa kwa upinzani kufanya vizuri kama itatumia vema fursa hii ya Wana- CCM wanaonyukana wenyewe kwa wenyewe. Huu ni wakati kwa Wapinzani kuwaonyesha Watanzania kuwa CCM ni chama cha kawaida tu na unaweza kuwepo mbadala wa chama hicho. Ni wakati pia kwa wapinzani kuongeza nguvu ya kusukuma hoja ya kuandikwa Katiba Mpya itakayowashirikisha wananchi katika hatua zote.

Na mpambano ule wa Dodoma, katika hali inayoweza hata kumstajabisha Lowassa mwenyewe, umempa sio tu ushindi Lowassa na kundi lake, bali pia, Lowassa ametoka kwenye vikao vile akiwa, walau kwa wakati huu, na nguvu nyingi zaidi za kisiasa ndani ya chama hicho . Inaonekana ’ jeshi la Lowassa’ ni kubwa, limesambaa na lina nguvu za kimikakati. Ndio, Edward Lowassa amenufaika sana kisiasa na vikao vya chama chake kule Dodoma.

Na mwananchi wa kawaida anasemaje?

Namwuliza , Andrew, kijana dereva wa teksi hapa Iringa; “ Unasemaje kuhusu yaliyotokea Dodoma CCM?”
”Lowassa hayumo!” Ananijibu.
”Una maana gani?” Namwuliza.
”Tuliambiwa Lowassa ni fisadi kumbe hayumo.”

Dereva wa teksi anaonyesha kufurahi kuujua ukweli. Swali ni hili; Je, aliousikia dereva wa teksi ni ukweli kamili? Hivyo basi, waliomwaminisha dereva wa teksi kuwa Lowassa ni fisadi wana mtihani wa kuja na ushahidi wa kumtia hatiani mtuhumiwa ili nao waaminike.

Na katika hili nayakumbuka maandiko ya mwanafasihi Kezilahabi: “ Siku hiyo ikifika utaona ishara itakayokuongoza. Utakapofika pale ambapo kila binadamu lazima afike utajua hukukosea; kwani njia ya kwenda huko inajulikana kwa wote na inakwenda moja kwa moja bila kupinda.

Huna haja ya kusoma kitabu chochote kupata maelezo ya kwenda huko wala hakuna haja ya kusikiliza mahubiri. Hakuna utalaamu unaohitajika maana utajikuta umefika. Utakapofika utamkuta amekaa peke yake akiwatazama wale wengine . Hao wengine utawatambua maana ni ndugu zako wote.

Wengi kati yao ndio wale waliokuwa askari wa mwanga. Wale ambao hutaweza kuwatambua atakumbulisha kwao na wewe utachukua nafasi yako. Usistuke utakaposikia majina yao; maana, wengi kati yao wana majina makubwa. Utawakuta wanafanya jambo fulani. Wewe pia fanya kama wao bila kuuliza bila manung’uniko na usikate tamaa. Kwa sasa hivi subiri ishara” ( E. Kezilahabi, Nagona)

Ni kina nani wamejeruhiwa Dodoma?

Nape Nnauye hawezi kuwa mwana- CCM mwenye furaha kwa wakati huu. Nahofia kuna hesabu za kisiasa alizozichanganya vibaya sana. Kama mwenezi wa chama alijichanganya sana kwenye kuilezea kwa umma dhana ya ’ Kujivua Gamba’ . Badala ya kuonekan kuwa ni mkakati wa mabadiliko ya jumla kwa CCM Nape aliitumia dhana hiyo kuwahukumu WanaCCM wenzake . Hivyo basi, kuonekana zaidi kuwa ni mbinu ya kutaka kuondokana nao ili kupisha njia kwa watu wa kundi lake. Na hapo ndio kwenye tatizo la msingi kwa Nape. Kwamba anaonekana kuwa na kundi lake kuelekea 2015.

Kujichanganya kwa Nape kimsingi kumewapa fursa akina Lowassa na wenzake kupanga mashambulizi na kuyatekeleza kwa mafanikio makubwa. Na kama kuna mtu aliyejeruhiwa vibaya kwenye vikao vya Dodoma ni Nape Moses Nnauye. Ana lazima ya kujipanga na kurudisha mashambulizi ili kulinda heshima yake na hata taswira yake kwa jamii. Hivyo hivyo kwa Samwel Sitta na wenzake. Dakika 45 za kuongea peke yake kwenye ITV hazikumwongezea nguvu Samwel Sitta na kundi lake na labda kinyume chake.

Je, ina maana vita ndani ya CCM ndio imekoma?
Hapana, huu ni mwanzo tu, vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya CCM vitaendelea na moto wake kuongezeka. Mwakani kuna uchaguzi wa ndani ya chama hicho. Tulichokiona Dodoma ni ’ rasha-rasha’ tu. Kutoka Dodoma makundi yanayohasiamiana ndani ya CCM yatazidi kupambana mikoani, wilayani na hata kwenye kata. Watazidi kupambana pia kupitia vyombo vya habari. Yote ni katika kuhakikisha wanajipanga kushika nafasi muhimu kwenye uchaguzi ujao wa chama chao, nafasi zitakazohakikisha wagombea wao wanapata tiketi za kuwania urais na hatimaye kushika dola.

Na Lowassa na wenzake wana kibarua kigumu cha kuwabadilisha WaTanzania kutoka kile walichoaminishwa kabla . Ni kibarua kigumu kama vile kumwambia mtu kuwa rangi nyekundu si nyekundu tena bali ni nyeupe. Kwamba alichokuwa akiamini mtu huyo siku zote kuwa ndicho, sicho. Ni watu hawa hawa ambao hawakupata tabu jana kujibu swali la je, fisadi mkuu ni nani? Na anayefuatia….?

Je, uchaguzi wa ndani ya CCM ukimalizika mwakani ndio mwisho wa vita?

Hapana, kundi litakaloibuka na ushindi wa jumla litahamishia mapambano yake kwa wapinzani wa chama na mgombea wao Urais walio nje ya chama chao. Kwa ilivyo sasa mashambuzi yanaweza kuelekea kwa Chadema. Hiki ni chama chenye nguvu na ushawishi mkubwa kwa wananchi kwa sasa.

Hivi ni Lowassa tu aliyeibuka mshindi kule Dodoma?
Hapana, kuna MwanaCCM mwingine aliyetoka Dodoma kimya kimya huku kikapu chake kikiwa kimejaa mavuno. Ni Fredrick Tluway Sumaye. Msomaji lishike jina hili. Huyu bwana hadi wakati huu anazicheza karata zake vizuri sana. Yaelekea mafunzo yake ya Uongozi aliyoyapata kule Havard Marekani yanamsaidia.
Si tulimsikia Sumaye kule Dodoma akisimama na kumtetea ’ majeruhi’ mwenzake Lowassa bila kutamka kuwa naye, Sumaye ni ’ majeruhi’ wa ’ Siasa uchwara’ kama anavyoziita Rostam Aziz. Sumaye ana mitaji ya kisiasa anayowekeza.

Je, ni kweli Lowassa ana nguvu na ushawishi mkubwa kisiasa?

Nikijibu hapana nitaongopa. Edward Lowassa ni mwanasiasa mahiri na mwenye ushawishi mkubwa ndani na hata nje ya chama chake. Wanaomjua Lowassa wanasema ana vitu viwili vikubwa; authority na humbleness. Kwamba ana uwezo wa kushawishi na kufanya vitu vifanyike na pia ni mnyenyekevu. Hilo la mwisho kuna wanaosema Lowassa anaweza kuongea na mtu mdogo sana, lakini atahakikisha hajibu simu ya mtu mwingine mpaka amalize mazungumzo na anayeongea nae.

Nikiwa Bagamoyo kwenye mkutano wa masuala ya elimu juma la jana kuna hoja ilizuka juu ya shule za sekondari za kata. Kikundi cha majadiliano nilichokuwamo kiliwajumuisha watendaji wa elimu kutoka Wilaya mbali mbali za Tanzania.
Swali likaulizwa; ” Ilikuaje sekondari za kata zikajengwa kwa kasi vile?”
”Ni Lowassa!” Alijibu mmoja wa washiriki.

Alifanyaje? Akauliza mwingine.
”Waliokuwa wakiratibu michango ya elfu kumi kumi kutoka kwa Watumishi walitwambia; Lowassa anataka tumpelekee orodha ya ambao hawakulipa michango hiyo, si orodha ya waliyolipa. Ni kwa njia hiyo kila mmoja wetu akachangia na shule zikajengwa. Ni nani anayetaka jina lake lifikishwe kwa Lowassa?” Alimalizia kwa kuuliza mmoja wa wanakikundi cha majadiliano.

Na kwa yaliyotokea Dodoma kuna watakaoshika tama na kusema, kumbe, Edward Lowassa hajamalizwa kisiasa! Je, akina Mwakyembe hawakufahamu, kuwa simba humwui kwa risasi ya kumpapasa masikioni?
Kama ni mchezo wa ngumi, basi, kwa mpinzani wa Lowassa, akubali, kuwa kummaliza Lowassa , awe tayari kucheza raundi zote 12.

Naam, tutayaona mengi mengine huko twendako, tuombe uhai.

Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Chadema Ikulu

HUJAFA hujaumbika! Ni habari mbaya inayogusa ‘kapo’ ya Wema Isaac Sepetu na Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ baada ya mnyange huyo kupoteza uzao wao kufuatia mimba yake ya takribani miezi miwili kuchoropoka, Ijumaa Wikienda linairusha hewani ‘laivu’ bila chenga.

TUJIKUMBUSHE SIKU YA FURAHA
Wiki kadhaa zilizopita, huku akiwa na furaha, Wema ambaye ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo, alisimama mbele ya kamera za video za gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko na kuthibitisha kuwa ana ujauzito wa mwezi mmoja na nusu baada ya kutoka kwenye vipimo (pregnancy test).

“Ni jambo la furaha sana, ni muda muafaka kwangu kupata mtoto,” alinukuliwa Wema akiwa hachezi mbali na ubuyu, ndimu na maembe mabichi.

CHANZO
Wiki mbili baadaye, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lilipokea simu kutoka kwa chanzo chake na mazungumzo yalikuwa hivi;
Chanzo: Ijumaa Wikienda mna habari?

Wikienda: Habari tunazo nyingi tu, soma magazeti ya Global Publishers, lakini kama una ya kwako, nayo ni muhimu ukitupatia tutairusha hewani.

Chanzo: Kwa taarifa yenu, mimba ya Wema imechoropoka na hapa tunapozungumza yupo hoi kitandani, anaumwa.
Wikienda: Una uhakika? Amelazwa hospitali gani?

Chanzo: Kwani nilishawahi kuwadanganya? Yupo nyumbani anakoishi na Diamond, Sinza-Madukani, Dar. Sitaki mahojiano zaidi, fuatilieni mtajua ukweli na tafadhali naomba msinitaje.

IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada ya maelezo hayo, Ijumaa Wikienda lilizama mzigoni na kujikusanyia data zilizokaribia kwenye ukweli kutoka kwa watu wa karibu na wapenzi hao.

Hata hivyo, timu ya Ijumaa Wikienda ilipotaka kumuweka Wema kwenye ‘tageti’, alisafiri na Diamond kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya shoo na mapumziko mafupi.

AREJEA BONGO, AWEKWA ‘MTUKATI’ Aliporejea Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita, Ijumaa Wikienda lilimuweka ‘mtukati’ na kumtaka kuonesha kibendi kilipoyeyukia. Alifunguka huku akijua kuwa akibisha, aibu itamfika kwani hana tena kile kitumbo kilichogeuka kero kwa mastaa wenzake kufuatia kutema mate ovyo.

Alisema: “Ilikuwa Jumatatu ileee (wiki mbili zilizopita), nilikuwa katika hali mbaya na baadaye niligundua kuwa mimba yangu inachoropoka. Nilikimbilia ‘famasi’ ya Primar na kumweleza mtaalamu hali yangu.
“Aliniambia mimba yangu imechoropoka hivyo nilipatiwa dawa kwa ajili ya kusafisha kizazi.

MUNGU HAKUPANGA AZAE?
“Ukweli niliumia sana, lakini nilijua Mungu hakupanga nizae wakati huu, najua amenipangia muda muafaka.
“Nahisi chanzo ni vipigo vya ‘toto yangu’ (Diamond Platinum Baby), lakini pia nahisi ni kwa sababu ya matumizi ya pombe kali.

DIAMOND ALIA KAMA MTOTO MDOGO
“Nilipomjulisha Diamond juu ya kupoteza kiumbe chake tumboni, alijisikia vibaya sana, alilia kwa uchungu kama mtoto mdogo.
“Kwa sasa niko fiti kabisa na namuomba Mungu nishike ujauzito mwingine kwani natamani kupata mtoto kuliko kitu kingine chochote.”

DIAMOND VIPI?
Diamond alikiri kumtandika Wema kutokana na kushindwa kuzuia hasira hasa mwanadada huyo anapomkosea, lakini hakuweza kuzungumzia kuchoropoka kwa ujauzito huo.
“Hata makofi muda mwingine yanafunza,” alisema Diamond.

ATHARI YA VIPIGO NA
POMBE KALI KWA MJAMZITO
Diamond na wanaume wengine wanapaswa kujua kuwa kasumba ya mwanaume kumpiga mwanamke ni ya kizamani na mke hapigwi makofi bali kwa upande wa khanga.

Pia Wema na wanawake wengine wanatakiwa kujua kuwa kunywa pombe wakati wa ujauzito ni sawa na kumpiga mwanao nyundo akiwa hai na kumuua.

NENO LA WIKIENDA
Kwetu sisi Wema na Diamond anayefanya vizuri kimuziki ni vijana watafutaji ambao ni mfano wa kuigwa kwani hawapendi kubweteka hivyo tunawapa pole kwa kupoteza uzao wao wa kwanza.

Mimba ya wema yachoropoka

HUJAFA hujaumbika! Ni habari mbaya inayogusa ‘kapo’ ya Wema Isaac Sepetu na Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ baada ya mnyange huyo kupoteza uzao wao kufuatia mimba yake ya takribani miezi miwili kuchoropoka, Ijumaa Wikienda linairusha hewani ‘laivu’ bila chenga.

TUJIKUMBUSHE SIKU YA FURAHA
Wiki kadhaa zilizopita, huku akiwa na furaha, Wema ambaye ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo, alisimama mbele ya kamera za video za gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko na kuthibitisha kuwa ana ujauzito wa mwezi mmoja na nusu baada ya kutoka kwenye vipimo (pregnancy test).

“Ni jambo la furaha sana, ni muda muafaka kwangu kupata mtoto,” alinukuliwa Wema akiwa hachezi mbali na ubuyu, ndimu na maembe mabichi.

CHANZO
Wiki mbili baadaye, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lilipokea simu kutoka kwa chanzo chake na mazungumzo yalikuwa hivi;
Chanzo: Ijumaa Wikienda mna habari?

Wikienda: Habari tunazo nyingi tu, soma magazeti ya Global Publishers, lakini kama una ya kwako, nayo ni muhimu ukitupatia tutairusha hewani.

Chanzo: Kwa taarifa yenu, mimba ya Wema imechoropoka na hapa tunapozungumza yupo hoi kitandani, anaumwa.
Wikienda: Una uhakika? Amelazwa hospitali gani?

Chanzo: Kwani nilishawahi kuwadanganya? Yupo nyumbani anakoishi na Diamond, Sinza-Madukani, Dar. Sitaki mahojiano zaidi, fuatilieni mtajua ukweli na tafadhali naomba msinitaje.

IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada ya maelezo hayo, Ijumaa Wikienda lilizama mzigoni na kujikusanyia data zilizokaribia kwenye ukweli kutoka kwa watu wa karibu na wapenzi hao.

Hata hivyo, timu ya Ijumaa Wikienda ilipotaka kumuweka Wema kwenye ‘tageti’, alisafiri na Diamond kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya shoo na mapumziko mafupi.

AREJEA BONGO, AWEKWA ‘MTUKATI’ Aliporejea Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita, Ijumaa Wikienda lilimuweka ‘mtukati’ na kumtaka kuonesha kibendi kilipoyeyukia. Alifunguka huku akijua kuwa akibisha, aibu itamfika kwani hana tena kile kitumbo kilichogeuka kero kwa mastaa wenzake kufuatia kutema mate ovyo.

Alisema: “Ilikuwa Jumatatu ileee (wiki mbili zilizopita), nilikuwa katika hali mbaya na baadaye niligundua kuwa mimba yangu inachoropoka. Nilikimbilia ‘famasi’ ya Primar na kumweleza mtaalamu hali yangu.
“Aliniambia mimba yangu imechoropoka hivyo nilipatiwa dawa kwa ajili ya kusafisha kizazi.

MUNGU HAKUPANGA AZAE?
“Ukweli niliumia sana, lakini nilijua Mungu hakupanga nizae wakati huu, najua amenipangia muda muafaka.
“Nahisi chanzo ni vipigo vya ‘toto yangu’ (Diamond Platinum Baby), lakini pia nahisi ni kwa sababu ya matumizi ya pombe kali.

DIAMOND ALIA KAMA MTOTO MDOGO
“Nilipomjulisha Diamond juu ya kupoteza kiumbe chake tumboni, alijisikia vibaya sana, alilia kwa uchungu kama mtoto mdogo.
“Kwa sasa niko fiti kabisa na namuomba Mungu nishike ujauzito mwingine kwani natamani kupata mtoto kuliko kitu kingine chochote.”

DIAMOND VIPI?
Diamond alikiri kumtandika Wema kutokana na kushindwa kuzuia hasira hasa mwanadada huyo anapomkosea, lakini hakuweza kuzungumzia kuchoropoka kwa ujauzito huo.
“Hata makofi muda mwingine yanafunza,” alisema Diamond.

ATHARI YA VIPIGO NA
POMBE KALI KWA MJAMZITO
Diamond na wanaume wengine wanapaswa kujua kuwa kasumba ya mwanaume kumpiga mwanamke ni ya kizamani na mke hapigwi makofi bali kwa upande wa khanga.

Pia Wema na wanawake wengine wanatakiwa kujua kuwa kunywa pombe wakati wa ujauzito ni sawa na kumpiga mwanao nyundo akiwa hai na kumuua.

NENO LA WIKIENDA
Kwetu sisi Wema na Diamond anayefanya vizuri kimuziki ni vijana watafutaji ambao ni mfano wa kuigwa kwani hawapendi kubweteka hivyo tunawapa pole kwa kupoteza uzao wao wa kwanza.

Jk akutana na Chadema

Rais JK akiagana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Ikulu mara baada ya mazunguzo jana.

Leo wanakutana tena kuendelea na mazungumzo yao

...akiagana na Mhe. Tundu Lissu

....akiagana na Mhe. John Mnyika

...akiagana na Prof. Adabballah Safari

..Mhe. Lissu akisepa taratibu kutoka Ikulu

...mambo yalivyokuwa ndani wakati wakipata chai na juisi...ilikuwa kirafiki zaidi.

PICHA: Hisani ya Ikulu

************************************************************************

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe

wa Serikali yake leo, Jumapili, Novemba 27,

2011, amekutana na kufanya mazungumzo

na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na

Maendeleo (CHADEMA).



Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika

Ikulu, Dar Es Salaam, yamefanyika katika

mazingira ya urafiki na ujumbe wa CHADEMA

umewasilisha mapendekezo yake kuhusu

mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya

Tanzania. Serikali imepokea mapendekezo

Hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana

kukutana tena asubuhi ya kesho, Jumatatu,

Novemba 28, 2011, ili kuipa nafasi Serikali

iweze kutafakari mapendekezo hayo.

Lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa

Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa

kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya

sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na

amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa

ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.



Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu

umuhimu wa kutunga Katibu Mpya kama

Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa

wakati wa salamu zake za mwaka mpya

Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba

ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa

miaka mingine 50 ijayo.



Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Rais

aliwahakikishia wajumbe hao wa CHADEMA

wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho,

Mheshimiwa Freeman Mbowe kuwa ni dhamira

yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa

Tanzania inapata Katiba mpya.



Katika mkutano huo, pande zote mbili

zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana

kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba

Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na

kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na

umoja wa kitaifa.



Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa

mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia

misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa

la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo

vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa

misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa

misingi ya maeneo.



IMETOLEWA NA:

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

NOVEMBA 27, 2011

DAR ES SALAAM

Tuesday, November 8, 2011

Mkurugenzi wa mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano (kushoto), akiwa ameshikilia na kuelezea moja ya kipeperushi kinachoonyesha namna ya kuupigia kura mlima Kilimanjaro ili uweze kuingia kwenye maajabu saba ya Dunia. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bw. Geofrey Tengeneza. Ili kupiga Kura Bure mteja wa Airtel Tuma neno KILI kwenda namba 15771.
Mkurugenzi wa mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano, akiwa ameshikilia simu huku akitoa maelekezo namna ya kuupigia kura mlima Kilimanjaro kura BURE kupitia Airtel ili uweze kuingia kwenye maajabu saba ya Dunia hadi tarehe 11 novemba…

Mkurugenzi wa mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano (kushoto), akiwa ameshikilia na kuelezea moja ya kipeperushi kinachoonyesha namna ya kuupigia kura mlima Kilimanjaro ili uweze kuingia kwenye maajabu saba ya Dunia. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bw. Geofrey Tengeneza. Ili kupiga Kura Bure mteja wa Airtel Tuma neno KILI kwenda namba 15771.
Mkurugenzi wa mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano, akiwa ameshikilia simu huku akitoa maelekezo namna ya kuupigia kura mlima Kilimanjaro kura BURE kupitia Airtel ili uweze kuingia kwenye maajabu saba ya Dunia hadi tarehe 11 novemba 2011.

Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Tengeneza, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari. Kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano wakati wa hafla fupi ya kutangaza Ofa kwa wateja wa Airtel kupigia kura mlima Kilimanjaro bure. Tuma KILI kwenda 15771 sasa.


Lulu Basi


Na Waandishi Wetu
MATUKIO yenye sura za aibu kwa kinda anayewika katika Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ yamezidi na sasa baadhi ya wasanii wenzake wamemshukia na kusema basi, imetosha, Risasi Mchanganyiko pekee limeshikilia mkoba wenye mafaili yote.

Baadhi ya wasanii wa kike waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la majina yao kutochorwa gazetini, Ijumaa iliyopita katika Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Saalam, walisema wamechoshwa na vituko vya msanii huyo na lazima wamkomeshe.

Wasanii wa filamu walikuwa viwanjani hapo katika mechi ya mpira wa miguu iliyochezwa kati ya Timu ya Bongo Movie na wafanyabiashara maarufu, ambapo kama kawaida Lulu alifanya vibweka.


Awali, waandishi wetu walimshuhudia msanii huyo akiwa kimya kama amemwagiwa maji ya baridi wakati akifuatilia mechi hiyo lakini kama vile asingeinuka na kucheza ngoma zilizokuwa zikipigwa katika viwanja hivyo.

Baadaye, ghafla Lulu alisimama na kuanza kucheza katika mitindo mbalimbali ambayo ilionekana dhahiri kuwa na nia ya kuwatega wanaume, baada ya Bongo Movie kupachika bao kwa wafanyabiashara hao.

“Huyu mtoto tumemvumilia tumechoka, kila siku anatutia aibu. Hebu ona anavyocheza...ngoma za namna gani zinachezwa vile? Ona anavyoonesha makalio, yaani huyu Lulu huyu! Dawa yake inachemka,” alisema staa mmoja wa sinema mwenye jina kubwa.

Matukio ya Lulu kulewa na kufanya vituko katika shughuli mbalimbali hayajaanza leo, lakini hata yanaporipotiwa ni kama anaambiwa aendelee kufanya vibweka, hapa chini ni baadhi ya matukio yaliyopo katika makabrasha ya Risasi Mchanganyiko;

SEPTEMBA, 2010 BILICANAS
Kamera za mapaparazi wa Risasi Mchanganyiko, zilimnasa msanii huyu laivu bila chenga ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta, Dar akiwa amelewa chakari huku akijiachia hovyo na hivyo mwili wake kubaki nje.

Habari hii iliandikwa na moja ya magazeti ya Global lakini Lulu hakukoma, aliendelea kama kawa na tabia yake hiyo.

AGOSTI 2011, MOSHI
Katika msafara wa wasanii wa Klabu ya Bongo Movie, Moshi, Kilimanjaro kulipokuwa na Tamasha la Kuelekea Miaka 50 ya Uhuru, lililochukua nafasi katika Viwanja vya Hugo mjini humo paparazi wetu alikuwemo.

Kama kawaida, msanii huyo alitia kinyaa baada ya kucheza katika mtindo usiokubalika hadi kujiangusha chini, aidha alikuwa amelewa tilalila kama kawaida yake (angalia picha ukurasa wa mbele).

SEPTEMBA 2011, LAMADA
Mafaili yetu yanaonesha kwamba tarehe hiyo Lulu alifanya kihoja kama hicho katika Viwanja vya Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar, lakini safari hii alikwenda mbali zaidi na kula denda na msanii mwenzake Soud Ally ‘Akhui’.

Ilikuwa ni hafla fupi ya ‘birthday’ ya msanii anayekuja juu kwenye soko la filamu Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, ambapo Lulu alitakiwa kutoa fedha au kumchagua mwanaume na kula naye denda hadharani, akachangua denda!

OKTOBA 2011, GYMKHANA
Maktaba ya Risasi Mchanganyiko inafunga ripoti yake kwa tukio lililotokea Ijumaa iliyopita, Oktoba 28, mwaka huu ambapo kila timu ya Bongo Movie ilipopachika bao, alianza kucheza katika mitindo ya aibu (kama picha zinavyoonekana ukurasa wa mbele).

AUNDIWA ZENGWE
Uamuzi uliofikiwa na baadhi ya wasanii wa kike waliozungumza na waandishi wetu Gymkhana, umeamua kumuundia zengwe ili kukomesha tabia yake hiyo mbaya.

“Kwa sababu tumeshagundua kwamba kila anapokwenda kwenye shughuli za kisanii anaharibu, tutazungumza na uongozi ili kuona kama wanaweza kumfungia kuhudhuria kwenye hafla yoyote ya msanii au inayohusu Bongo Movie.

“Hilo likishindikana, basi bado kuna sababu ya kuongea na uongozi na kuwaambia kwamba kama Lulu akiingia kwenye sherehe zetu basi asinywe pombe kabisa, maana haziwezi. Acha tukazungumze na viongozi wetu halafu tutawajulisha,” alisema mmoja wa wasanii hao.

Lulu ni msichana mdogo ambaye bado ana nafasi ya kubadilika. Ni vyema akatambua thamani yake kama msanii na kuchukua hatua za makusudi haraka.

Ukosefu usingizi una athiri afya yako

UNAWEZA kuwa makini sana na kila kitu unachochokula au unachokunywa kwa lengo la kulinda afya yako, lakini kama wakati wa kulala hupati usingizi, hali hiyo inaweza kuathiri afya yako.

Halikadhalika, kama mahali unapolala (kitandani au jamvini) na mazingira yake hayaendani na mahitaji ya mwili wako, huwezi kuwa na afya njema pia.

Mahali tunapolala pamoja na suala la kupata usingizi ni kitu muhimu sana kama kilivyo chakula. Utakumbuka kwamba karibu nusu ya maisha yetu tunayamalizia kitandani. Kama mtu ukijaaliwa kuishi duniani kwa muda wa miaka 60, kwa mfano, miaka 20 au 25 utakuwa umeitumia kwa kulala.

Unapolala, usingizi hufanyakazi ya kurejesha nguvu ya ubongo na mwili iliyopotea wakati wa mchana. Usingizi hurejesha upya nishati ya mwili na ubongo inayokuwezesha kupata akili ya kuainisha matatizo na kuyapatia ufumbuzi. Vile vile hukuwezesha kuamka asubuhi ukiwa na nguvu mpya ya kupambana na masuala mengine ya siku hiyo.

KWA NINI USIPATE USINGIZI?
Kama usingizi ndiyo muhimu kiasi hicho, kwa nini mtu usilale na kupata usingizi? Kuna sababu kadhaa zinazoweza kukufanya usipate usingizi, kuanzia chakula unachokula hadi mahali unapolala. Lakini habari njema ni kwamba kasoro zote unaweza kuzirekebisha na kupata usingizi mnono.

Kama una matatizo wakati wa kulala, kama vile kukosa usingizi, kuamka usiku mara kwa mara, kujisikia mchovu unapoamka asubuhi, au unahitaji kuboresha usingizi wako, kuna mambo mengi ya kufanya, yakiwemo haya yafuatayo:
HAKIKISHA unalala muda ule ule kila siku na muda mzuri ni saa 4:00 usiku.

JIEPUSHE kula vyakula muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, hususan vitafunwa (snacks) vitokanavyo na nafaka na vyenye sukari. Badala yake kula vyakula vyepesi vya kuongeza protini mwilini, kama vile maziwa, n.k.

HAKIKISHA chumba unacholala kisiwe na baridi au joto sana. Wastani mzuri wa kiwango cha joto kinachokubalika kiafya ni nyuzi joto kati ya 18 na 21.

EPUKA kunywa kahawa au chai muda mfupi kabla ya kulala, vinywaji hivi huathiri usingizi kwa kiasi kikubwa.
HAKIKISHA unafanya mazoezi mara kwa mara, lakini siyo muda mfupi kabla ya kulala. Fanya mazoezi mapema na upate muda mrefu wa kupumzika kabla ya kupanda kitandani.

MWISHO kitanda, shuka na mto unaolalilia, hakikisha una ubora unaotakiwa. Shuka ya kujifunika na mto uliotengenezwa kutokana na pamba halisi (cotton wool) ni bora zaidi kuliko zilizotengenezwa kwa malighafi zingine, kama ‘polyester’, ‘synthetics’ n.k., ambazo zinadaiwa kuwa na kemikali zenye madhara kiafya.


Kafara Nzito


Na Luqman Maloto
VIONGOZI wakuu wa Dini ya Shetani, Freemasons, wamefanya kafara nzito kuadhimisha kukamatwa, kuteswa kisha kuuawa kwa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi.

Vyanzo vimesema kuwa ni kawaida kwa Freemasons kufanya sherehe yenye mrengo wa kafara kila mara, mpango wao unapofanikiwa sehemu yoyote ile.

Kwa mujibu wa mitandao kadhaa inayojihusisha na utoaji wa habari za jamii ya Freemasons, kafara ambayo hufanywa ni ile ya mnyama hususan mbuzi mwenye pembe zinazofanana na zile za jini anayeitwa Lucifer (jini mkuu) ambaye huabudiwa na wafuasi wa Dini ya…

Na Luqman Maloto
VIONGOZI wakuu wa Dini ya Shetani, Freemasons, wamefanya kafara nzito kuadhimisha kukamatwa, kuteswa kisha kuuawa kwa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi.

Vyanzo vimesema kuwa ni kawaida kwa Freemasons kufanya sherehe yenye mrengo wa kafara kila mara, mpango wao unapofanikiwa sehemu yoyote ile.

Kwa mujibu wa mitandao kadhaa inayojihusisha na utoaji wa habari za jamii ya Freemasons, kafara ambayo hufanywa ni ile ya mnyama hususan mbuzi mwenye pembe zinazofanana na zile za jini anayeitwa Lucifer (jini mkuu) ambaye huabudiwa na wafuasi wa Dini ya Shetani.

Mnyama huyo huchinjwa kisha damu na kichwa chake huhifadhiwa kwenye chombo chochote chenye muundo wa ndoo ili pembe zitokeze kwa juu na kutengeneza alama maarufu ya Freemasons ambayo wafuasi wake huitumia kwa njia ya vidole kutoa salamu.

Habari zinasema Freemasons walifanya kafara hiyo usiku wa manane kwenye hekalu moja kubwa lililojengwa kwenye eneo la jangwa lililopo ndani ya Jiji la Misrata, Libya.

Inabainishwa kuwa viongozi mbalimbali wakubwa kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi ambao wana vyeo vikubwa ndani ya jamii ya Freemasons, walihudhuria kafara hiyo.

MKAKATI HATARI
Habari zinabainisha kuwa Freemasons ipo kwenye mkakati thabiti wa kuitawala dunia kabla ya Desemba 2012.
Kutokana na mkakati huo, imebainishwa kuwa Freemasons wamekuwa wakiratibu sera zao kwa kuangusha utawala wa nchi mbalimbali ambao viongozi wake wameshindwa kuendana na matakwa yake.

Inaelezwa kuwa Gaddafi alikuwa kiongozi mwenye mrengo wa Kiislam japo alikuwa haweki wazi kwenye utawala wake na kwamba alikuwa anapingana vikali na Freemasons.

Kwa mujibu wa mnajimu msomi, Maalim Hassan Yahya Hussein, Jeshi la Kujihami la Umoja wa Nchi za Magharibi (Nato), hutekeleza mipango ya Freemasons kama lilivyofanya Libya kumng’oa Gaddafi.

Maalim Hassan ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mnajimu maarufu barani Afrika, marehemu Sheikh Yahya Hussein, alisema kuwa dhumuni kuu la Freemasons ni kuzipiga vita dini za Kiislam na Kikristo.

“Ipo wazi kuwa wao lengo lao ni kuitawala dunia, kwa hiyo wanahakikisha hilo linawezekana kwa kudhoofisha Uislam na Ukristo ili ufe kisha Shetani ashinde hapa duniani,” alisema Maalim Hassan ambaye ni mrithi wa kazi za unajimu za marehemu Sheikh Yahya.

Aliongeza: “Mkakati mkubwa zaidi ni kuhakikisha dunia inaabudu Dini ya Shetani, wanataka kila mtu awe chini ya mamlaka ya jini mkuu (Lucifer). Dunia nzima itawaliwe na serikali moja na iwe na sarafu moja.”

Kauli ya Maalim Hassan inashabihiana na ile iliyopo kwenye maandiko kwamba zama za Dini ya Shetani kuishika dunia, kutakuwa na mfumo ambao utazuia mtu yeyote kupata huduma za kijamii mpaka awe mwanachama na atatambulika kwa chapa 666.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Freemasons wanatumia njia mbalimbali kuhakikisha ulimwengu mzima hakuna anayeamini dini za Mungu na wanapambana kuhakikisha hata Yesu (Nabii Isa) atakaporejea akute hakuna aliye tayari kukombolewa.

Katika kuhakikisha wanapambana na nguvu ya Yesu, Freemasons wamekuwa wakitumia damu ndiyo maana hutoa kafara kwa kuchinja mnyama hasa mbuzi au kondoo wenye pembe kwa imani kwamba huwaongezea nguvu ya kuishika dunia.

Kutokana na tishio la Freemasons, viongozi wa kidini hususan wale wa Mashariki ya Kati, wamekuwa wakiwataka Waislam na Wakristo kwa imani zao, kufunga na kusali ili Dini ya Shetani isipate mafanikio inayoyataka.

SAKATA LA USHOGA
Habari zinasema kuwa Serikali ya Uingereza imekuwa ya kwanza kutumiwa na Freemasons katika kuhakikisha nchi zote zinazounda Jumuiya ya Madola zinapitisha sheria zinazokinzana na maandiko matakatifu yanayoaminiwa na waumini wa Dini za Kiislam na Kikristo.

Ushoga na usagaji ni vitendo ambavyo vinakemewa na dini hizo lakini hivi sasa, Freemasons wanadaiwa kuchochea mabadiliko ili watu wanaojihusisha na hulka hizo wawe huru kikatiba duniani.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alitangaza kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola ili apate misaada inabidi kwanza aruhusu ndoa za jinsi moja (ushoga na usagaji) kwenye katiba ya nchi yake.

Tanzania ikiwa moja ya wanachama wa Jumuiya ya Madola, inapitiwa kwenye rungu hili, ingawa Balozi wa Uingereza nchini, Diana Corner alisema nchi yetu haihusiki.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alishatoa tamko kwamba Tanzania haipo tayari kuruhusu ndoa za mashoga na wasagaji kisha akaonya kuwa kauli ya Cameron inaweza kuivunja Jumuiya ya Madola.

SIYO FREEMASONS PEKE YAKE
Mbali na Freemasons, dini nyingine zenye mrengo wa Shetani ni Illuminati na Skull & Bones ambazo zinavuma zaidi Marekani.

VIGOGO WA FREEMASONS
Viongozi wanaotajwa kuwa vigogo wa jamii hiyo ni marais wa 43 na 44 wa Marekani, Barack Obama na George Bush, Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy ambao wanaonesha alama za vidole ukurasa wa kwanza. Yupo pia Cameron na wengine wengi.


Mbio za Mwenge zaingia Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya (kulia), akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro,baada ya mwenge huo kumaliza mbio zake mkoani Rukwa, katika hafla iliyofanyika jana, kijiji cha Mkutano wilayani Mbozi.
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo (kulia), akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini,Evance Balama, baada ya mwenge huo kumaliza mbio zake wil;ayani Mbozi.Makabidhiano hayo yalifanyika Songwe Viwandani mkoani Mbeya.Mwenge huo mkaoni Mbeya utafungua miradi yenye thamani ya sh.bilioni 2.6 na Wilayani Mbozi umefungua miradi mitatu ya sh.milioni 156.
Askari wa kutuliza ghasia na skauti wakiulinda mwenge wa uhuru baada ya kuwasili viwanja vya Bomani wilayani Mbozi.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa,Mtumwa Rashid Halfan, kutoka kaskazini Unguja,akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa Kiume wa Sekondari ya Mwalimu Jk.Nyerere iliyopo Tunduma wilayani Mbozi mkoani Mbeya.

sherehe za siku ya kuzaliwa mwanzilishi wa dini ya Sikh Guru Singh Sabha,

Wafuasi wa dini ya Sikh wakiwa katika sherehe hiyo.

salam,

MAELFU ya wafuasi wa dini ya Sikh walijitokeza siku ya Jumapili tarehe 6 Novemba 2011 katika mji wa Southall, Middlesex UK ili kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa dini yao Guru Nanak aliyezaliwa mwaka 1469 nchini Pakistan.

Muasisi wa Dini ya Sikh

Wakati akiwa na umri wa miaka 30 alipotea kwa hali ya miujiza kwa muda wa siku tatu. Alipo rejea alianza kuhubiri, kufundisha na kuandika dini ya Sikh wakati wa maisha yake yote. Pia Guru Nanak alisafiri dunia nzima kuitangaza na kujadili dini hii kwa waumini wengine kama waislamu pamoja na Wahindu.

Kwa miaka zaidi ya 550 wafuasi wa dini hii wamekuwa na desturi hii ya kusherehekea siku moja kabla ya kuzaliwa kwake Guru Nanak kwa kuandaa maandamano haya makubwa ya Sherehe hii ambayo hufanyika India pamoja na baadhi ya sehemu za nchi ya Uingereza.

Kwa kawaida sherehe hizi huongozwa na wafuasi wakuu watano wanaojulikana kama "Panj Piare" wakiambatana na waimbaji, wanamuziki na timu ya wacheza Upanga (Martial Arts) kuelekea hekaluni kwao "Gurdwara" Sri Guru Singh Sabha, hapa Southall hekalu lao ndio kubwa kuliko yote katika bara la ulaya.

Sherehe hizi huanza mapema asubuhi kwa kuimba, kuomba kwa pamoja. Baadae chakula cha kitamaduni kinachojulikana kama "Langar" hutolewa bure kwa kila mtu.

Maandamano ya Southall yanaitwa Nagar Kirtan,

Asanteni,

Mbowe, Slaa, Lissu Ni mkesha wa siku 7

Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiwa katika viwanja vya NMC jijini Arusha jana.
-Ni baada ya Lema kubakia tena mahabusu
-Jiji la Arusha larindima, umati wajaa NMC
MAELFU ya wakazi wa Jiji la Arusha, jana walikubali kunyeshewa mvua katika mkutano wa hadhara ambapo viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walitangaza mkesha wa ukombozi hadi hapo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, atakapopewa dhamana.

Aidha, wamesema mkesha wa aina hiyo utaendelea kwa mikoa ya Mwanza, Mbeya na Kilimanjaro huku mkoa wa Dar es Salaam ukijiandaa kwa harakati hizo.

Akitangaza kuwepo kwa mkesha huo huku mvua ikinyesha, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa alisema: “Uwanja huu utakuwa mali ya wakazi wa Arusha, na sisi hatutatoka hapa mpaka Lema atakapotoka mahabusu.”

Mvua ilianza kunyesha majira ya saa 9:30 alasiri hivi hadi saa 11:00 jioni, lakini haikuwafanya mamia kwa maelfu ya wafuasi hao wa Chadema kukimbia eneo hilo.

Mkesha huo ulitangazwa saa chache baada ya harakati za kumtoa Lema kwa kumwekea dhamana, ili atoke mahabusu kukwama baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusema anatakiwa apelekwe mahakamani hapo, Novemba 14, mwaka huu, saa 2: 30 asubuhi.

Msimamo huo ulitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Richard Magessa, akijibu ombi la Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, aliyeiomba itoe hati ya kumtoa Lema mahabusu na kumleta mahakamani hapo kwa ajili ya kumwekea dhamana.

Katika barua ya mahakama hiyo yenye kumbukumbu namba RM/GC/Vol III/50 ya Novemba 7, 2011, ilisema: “Wadhamini wa mshtakiwa wafike mahakamani siku ya kutajwa kesi, 14/11/2011, saa 2:30 asubuhi kwa ajili ya utaratibu wa dhamana.”

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, Dk. Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, walifika mahakamani hapo kufuatilia taratibu za kumtoa Lema.

Hata hivyo, baada ya kupata taarifa hiyo, Mbowe, alilazimika kuwatuliza maelfu ya wananchi wa Arusha waliokusanyika nje ya viwanja vya mahakama kwamba watulie, kwa kuwa Chadema ni chama chenye nidhamu.

Alisema wameanzisha mapambano ya historia ya taifa hili, kwamba ukombozi wa Tanzania utaanzia hapa: “Tupo kwenye maombolezo kwa sababu mbunge mliyemchagua na kushinda kwa kura nyingi zaidi ya 20,000 amekuwa akinyanyaswa tangu alipochaguliwa, na hii inamaanisha kwamba ninyi mliomchagua hamna maana.”

Alisema anataka umati huo upeleke ujumbe kwa chama tawala na serikali yake kwamba hakuna mwenye hatimiliki ya nchi hii.

“Sisi sote tumezaliwa hapa, tunaishi hapa na tutakufa hapa na hakuna mwenye hatimiliki ya maisha ya mtu mwingine…tusije tukalaumiwa kwa kuchukua maamuzi haya magumu, hii inatokana na CCM yenyewe kutulazimisha kuchukua maamuzi haya,” alisema muda mfupi kabla ya kutangaza kuanza kwa mkesha.

Akitangaza utaratibu wa mkesha huo, Mbowe, alisema: “Sasa hivi hatutazungumza lugha ya Lema, tunazungumza lugha ya ukombozi.”

Alisema matatizo ya Arusha yalianza tangu uchaguzi wa Meya ambao alisema CCM iliuvurunda na kwamba Meya aliyechaguliwa ni batili.

Alisema suala hilo lilifikishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Chadema, lakini hakuna ufumbuzi wowote ambao umefikiwa hadi sasa.

“CCM wanaringa kuwa wana polisi, wana magereza, wana risasi, wana mabomu…sasa nawaambia kwamba hatuogopi mvua na tutakesha hapa tuzungumze kuhusu masuala ya ukombozi,” alisema na kuongeza: “Tumeanza mbinu mpya ya mapambano, hivyo, kama viongozi tumeamua tutakesha katika viwanja hivi hadi hapo serikali itakapoamua kutuletea mbunge wetu.”

Alisema mkesha huo hauwahusu watoto wadogo kwa kuwa ‘ngoma’ hiyo ni nzito kwao na hivyo akawataka warudi majumbani kwao kulala na kuwaacha hapo watu wakubwa.

“Hatuwezi kuendelea kujenga taifa la watu wenye woga, watu ambao wanatishwa na wenzao,” alisema na kuongeza: “Tunaposema hakuna kulala mpaka kieleweke naona watu hawatuelewi.”

Alisisitiza kuwa mkesha huo ni wa ukombozi na hawezi kuufunga mkutano huo kwa sababu wameamua kukesha kwa amani.

Aliusihi umati huo kuacha kuleta vurugu, kumpiga mtu wala kusukumana ili watu wasiowapenda wasipate sababu ya kuwajengea hoja kwamba chama hicho ni cha watu wasio na nidhamu.

“Wakitaka kutupiga, waje watupige na wakitaka kutupakia kwenye magari waje watupakie na kutupeleka kwa mahabusu, hatuogopi kabisa,” alisema.

ATULIZA HALI MAHAKAMANI

Awali, Mbowe alitumia busara ya ziada kuwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika mahakamani kumsubiri Lema.

“Makamanda naomba muwe watulivu, Chadema ni chama chenye nidhamu, kwa kuwa kesi zingine zinaendelea mahakamani hapa, naomba twende viwanja wa NMC ambako tutawaelezeni kila kitu kilichojiri….mimi kamanda wenu pamoja na Dk. Slaa na Tundu Lissu tutaongoza maandamano hayo hadi viwanja vya NMC,” alisema huku akishangiliwa na umati huo wa watu.

Mapema wakati Mbowe alipowasili mahakamani hapo, majira ya saa 8:51 mchana na kuingia ndani ya viwanja vya mahakama, kundi kubwa la wafuasi wa Chadema waliokuwa wamesimama tangu asubuhi nje ya uzio wa mahakama, waliingia ndani wakimsindikiza.

Hali hiyo iliwafanya polisi wa kutuliza ghasia waliokuwa kwenye Land Rover yenye namba za usajili PT 1178 kuendesha gari lao kwa kasi kwa lengo la kuzuia gari la Mbowe, aina ya Toyota lenye namba za usajili T968 BRH, lisisonge mbele zaidi kuelekea mahakamani.

Baada ya kuzuiwa Mbowe alishuka kwenye gari lake na baada ya kuzungumza kwa muda na askari polisi, aliwaomba wafuasi wake kwamba watoke nje ya viwanja hivyo.

“Nimekuja hapa kushughulikia suala hili la Lema, naomba msilete vurugu, Chadema ni chama chenye nidhamu, au sio makamanda, sasa nawaomba mtoke nje ya viwanja kwa kuwa kuna kesi za watu zinaendelea mahakamani hapa, tuwape utulivu ili kesi zao zipate kusikilizwa kwa haki,” alisema.

Baada ya kusema hayo wafuasi hao walitii amri hiyo na kutoka nje ambako waliendelea kusubiri hadi majira ya 9:20, walipopata taarifa ya kutakiwa kwenda viwanja vya NMC kwenye mkutano.

Aidha, maelfu ya watu waliojitokeza mahakamani hapo walikuwa na shauku ya kutaka kumwona mbunge wao akitolewa mahabusu na pia umati kama huo ulikuwepo Kisongo, kona ya kwenda magereza wakimsubiri Lema atolewe.

Watu hao wote waliokuwepo mahakamani hapo na wale waliokuwepo eneo la Kisongo nao pia walitembea kwa miguu hadi kwenye viwanja vya NMC kusikiliza mkutano ili kujua kulikoni.

MAHABUSU WAGOMA KUSHUKA KWENYE KARANDINGA

Mapema majira ya saa 4 asubuhi karandinga la polisi lililokuwa limewabeba mahabusu kusikiliza kesi zao, waligoma kuteremka kwenye gari hilo, lakini mahabusu wachache wanawake waliteremka.

Baada ya kuwasubiri kwa zaidi ya robo saa bila kuteremka, askari polisi waliowaleta waliamua kuwarejesha gerezani, pamoja na mahabusu wanawake ambao awali walishuka kwenye karandinga hilo.

Wakigoma kushuka kwenye karandinga hilo, mahabusu hao walisikika wakisema kwa sauti kubwa kwamba hawashuki hadi Lema atakapoletwa mahakamani hapo.

Maneno hayo yaliwafanya polisi kuwaamuru mahabusu wa kike walioteremka kupanda kwenye gari na wote wakarudishwa gerezani Kisongo.

Umati wa watu ulizidi kufurika katika viwanja vya mahakama, lakini idadi kubwa zaidi ya watu ilibaki nje ya uzio wa mahakama ambako walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana.

Baadhi ya nyimbo walizokuwa wakiimba ni ‘Lema usiogope…usiogope magereza Lema,’ na wakati fulani ofisa mmoja wa polisi aliyekuwa kwenye gari aina ya Landrover lenye namba za usajili PT 1844 aliwaomba wafuasi hao wa Chadema kutangulia kwenye viwanja vya NMC ambako chama hicho kilipanga kufanya mkutano mkubwa wa hadhara, lakini walikataa na kisha akaambulia kuzomewa.

Watu hao walikuwa wameshika bendera na matawi ya miti wakipeperusha juu huku wakirukaruka na kuendelea kuimba nyimbo mbalimbali.

Kila lilipokuwa likipita gari la polisi, walisikika wakiimba Chadema semaaa…sema usigope semaa, Lema semaa…semaaa usiogope, semaa…sisi mapanya hatuogopi magereza, sema.

Mbwembwe za kuzunguka na pikipiki aina ya Toyo zilizokuwa na bendera za chama zilitoa burudani ya kutosha nje ya uzio wa mahakama hali ambayo iliwafanya wasichoke.

Wakati fulani majira yaa 6 hivi mchana, mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Arumeru, Nelson Nassari, alilazimika kuwatuliza vijana hao na kuwaeleza kwamba taratibu ndio zinazochelewesha kumtoa Lema, lakini aliwaeleza matumaini yake kwamba angetoka jana.

Alisema taratibu hizo zinafanywa kwa makusudi ili kuchelewesha muda wa saa 5 walioomba kufanya mkutano katika viwanja vya NMC.

Akiwatuliza alisema anatoa muda wa nusu saa na baada ya kupita muda huo kama taratibu za kupata hati ya kumtoa Lema mahabusu itachelewa, basi atawaruhusu waingie ndani ya uzio wa mahakama.

Palikuwa hapatoshi mahakamani kwa mbwembwe za vijana hao ambao walizidi kuimba nyimbo za kutiana hamasa na kila mara gari la polisi lilipokuwa likipita vijana hao walisikika wakiimba, ’polisi hatutaki unyanyasaji, hatumtaki huyo Zuberi (Zuberi Mwombeji ni Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha).

Pia walikuwa wakiimba, “Said Mwema mkanye Zuberi” na wakati mwingine walikuwa wakisikika kuimba, “Tumeyamisi mabomu ya polisi.” Nyimbo zingine ni kama “Mmetuita panya, nyie ni manyau.”

Vijana hao wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, ‘kama tatizo ni ubunge apewe Zuberi na u-OCD apewe Lema.

Hali ya mitaa mbalimbali jijini hapa ilijaa kila aina ya mbwembwe ya misafara ya pikipiki na magari yaliyokuwa na bendera za Chadema, na idadi kubwa ya watu ilikuwa tayari imefurika katika viwanja vya NMC kuanzia majira ya saa 4 asubuhi.

Watu wengi walikwenda kumsubiri Lema eneo la Kisongo wakiwa kwenye pikipiki na magari hali ambayo ilivuta umati mkubwa wa watu.

Rais Dkt Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na wageni wao Prince Charles na mkewe Duchess of Conrnwall

Rais Dkt Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na wageni wao Prince Charles na mkewe Duchess of Conrnwall katika dhifa ya kitaifa waliyowaandalia jana usiku Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisoma hotuba yake katika hafla hiyo.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akinyanyua glasi juu kuwatakia afya wageni wake na msafara wao.
Makofi baada ya hotuba ya Rais.
Prince Charles akisoma hotuba yake.
Duchess of Cornwall akimpongeza kiongozi wa bendi ya brass ya Polisi baada ya kutumbuiza vyema.

Monday, November 7, 2011

Hannibal Gaddafi akijirusha

Hannibal Gaddafi akijirusha na mwanamke aliyetajwa kuwa ni mkewe.

Sifael Paul na Mitandao
PICHA zinazomuonesha mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya aliyeuawa na majeshi ya baraza la mpito la nchi hiyo (NTC), hivi karibuni, Muammar Gaddafi, Hannibal Gaddafi akijirusha na mwanamke aliyetajwa kuwa ni mkewe, Aline ufukweni, zimesambaa katika vyombo vya habari vya magharibi.

Habari kutoka mtandaoni zinadai kuwa zipo baadhi ya picha za Hannibal ambazo zilipigwa wakati tayari machafuko ya kumuondoa baba yake madarakani yakiwa yameshaanza.


...Wakizidi kujivinjari ufukweni.

Picha hizo zinamuonesha Hannibal akiwa kwenye boti binafsi katikati ya bahari mbali na nchi aliyouawa baba yake, Libya huku wakiweka pozi za ‘kimalavidavi’ kitandani na ufukweni.

Kusambaa kwa picha hizo za kimahaba zinazomuonesha Hannibal ambaye inasadikiwa alitorokea nchini Algeria na mama na dada yake baada ya hali kuwa mbaya ni mwendelezo wa chokochoko za kuiandama familia ya Gaddafi ili ionekane ilikuwa ikitumbua rasilimali za umma.

HALI IKOJE LIBYA KWA SASA?
Hali haijatulia nchini Libya kwani vilio dhidi ya vitendo vya ufirauni na mauaji ya kikatili ya Gaddafi bado vinaendelea kwa waliokuwa wakimuunga mkono kiongozi huyo.

Hannibal Gaddafi.

Mamiss Tanzania wapata dili

Miss Tanzania namba mbili, Tracy Sospeter, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kula shavu.

Tracy na Alexia wakijisevia msosi kwenye hafla hiyo.

MREMBO aliyetwaa taji la Miss Tanzania namba mbili mwaka huu, Tracy Sospeter, na aliyetwaa taji la mshindi wa tatu, Alexia William, usiku wa kuamkia leo wamepata ‘shavu’ la kuwa mabalozi wa kampuni mpya ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Uhusiano na Masoko iitwayo Tanzania Mwandi. Warembo hao walikula shavu hilo kwenye uzinduzi wa kampuni hiyo uliofanyika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.
’Wakijisosomola’.

Sehemu ya wadau walioalikwa.

Mhariri wa Gazeti la Championi, John Joseph, akitafakari jambo. Kulia ni mmoja wa wadau wa kampuni hiyo, Damas Ndumbaro.

Wadau wakisikiliza kwa makini.
Tracy akitoa shukrani baada ya kuteuliwa na kampuni hiyo kuwa balozi wake.

New