My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, November 2, 2011

Dini ya Jacqueline Wolper utata

Na Imelda Mtema
DINI ya msanii maarufu wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ‘Amber Rose wa Bongo’ (pichani) imezua utata baada ya kutoa kauli ambayo imewaacha njia panda mashabiki wake.

Utata huo umekuja kufuatia hivi karibuni Risasi Mchanganyiko kuzama getho kwa msanii huyo ambaye anafahamika ni muumini mzuri wa dini ya Kikristo na kukutana na mazingira ya Kiislamu na Kikristo.

Paparazi wetu alishuhudia mwanadada huyo akiwa amepamba aya za Quran ukutani sebuleni kwake, huku mezani kukiwa na Biblia.

Alipoulizwa alisema: “Mimi sioni kama kuna tatizo kwa sababu ninachojua Mungu tunayemuabudu ni mmoja siku zote, ndiyo maana naamini hakuna tatizo lolote mimi kwenda msikitini au kanisani.”

Akasema kuwa, katika jamii tunayoishi haoni sababu ya kujibagua kwa dini kwani zote ni sawa hivyo asionekane mtu wa ajabu kuamini dini mbili.

Kauli ya msanii huyo imewafanya baadhi ya mashabiki wake kumchukulia tofauti kwani ni staa wa kwanza Bongo kutangaza kuuamini ukristo na uislam kwa wakati mmoja.

No comments:

Post a Comment

New