My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, November 8, 2011

Lulu Basi


Na Waandishi Wetu
MATUKIO yenye sura za aibu kwa kinda anayewika katika Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ yamezidi na sasa baadhi ya wasanii wenzake wamemshukia na kusema basi, imetosha, Risasi Mchanganyiko pekee limeshikilia mkoba wenye mafaili yote.

Baadhi ya wasanii wa kike waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la majina yao kutochorwa gazetini, Ijumaa iliyopita katika Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Saalam, walisema wamechoshwa na vituko vya msanii huyo na lazima wamkomeshe.

Wasanii wa filamu walikuwa viwanjani hapo katika mechi ya mpira wa miguu iliyochezwa kati ya Timu ya Bongo Movie na wafanyabiashara maarufu, ambapo kama kawaida Lulu alifanya vibweka.


Awali, waandishi wetu walimshuhudia msanii huyo akiwa kimya kama amemwagiwa maji ya baridi wakati akifuatilia mechi hiyo lakini kama vile asingeinuka na kucheza ngoma zilizokuwa zikipigwa katika viwanja hivyo.

Baadaye, ghafla Lulu alisimama na kuanza kucheza katika mitindo mbalimbali ambayo ilionekana dhahiri kuwa na nia ya kuwatega wanaume, baada ya Bongo Movie kupachika bao kwa wafanyabiashara hao.

“Huyu mtoto tumemvumilia tumechoka, kila siku anatutia aibu. Hebu ona anavyocheza...ngoma za namna gani zinachezwa vile? Ona anavyoonesha makalio, yaani huyu Lulu huyu! Dawa yake inachemka,” alisema staa mmoja wa sinema mwenye jina kubwa.

Matukio ya Lulu kulewa na kufanya vituko katika shughuli mbalimbali hayajaanza leo, lakini hata yanaporipotiwa ni kama anaambiwa aendelee kufanya vibweka, hapa chini ni baadhi ya matukio yaliyopo katika makabrasha ya Risasi Mchanganyiko;

SEPTEMBA, 2010 BILICANAS
Kamera za mapaparazi wa Risasi Mchanganyiko, zilimnasa msanii huyu laivu bila chenga ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta, Dar akiwa amelewa chakari huku akijiachia hovyo na hivyo mwili wake kubaki nje.

Habari hii iliandikwa na moja ya magazeti ya Global lakini Lulu hakukoma, aliendelea kama kawa na tabia yake hiyo.

AGOSTI 2011, MOSHI
Katika msafara wa wasanii wa Klabu ya Bongo Movie, Moshi, Kilimanjaro kulipokuwa na Tamasha la Kuelekea Miaka 50 ya Uhuru, lililochukua nafasi katika Viwanja vya Hugo mjini humo paparazi wetu alikuwemo.

Kama kawaida, msanii huyo alitia kinyaa baada ya kucheza katika mtindo usiokubalika hadi kujiangusha chini, aidha alikuwa amelewa tilalila kama kawaida yake (angalia picha ukurasa wa mbele).

SEPTEMBA 2011, LAMADA
Mafaili yetu yanaonesha kwamba tarehe hiyo Lulu alifanya kihoja kama hicho katika Viwanja vya Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar, lakini safari hii alikwenda mbali zaidi na kula denda na msanii mwenzake Soud Ally ‘Akhui’.

Ilikuwa ni hafla fupi ya ‘birthday’ ya msanii anayekuja juu kwenye soko la filamu Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, ambapo Lulu alitakiwa kutoa fedha au kumchagua mwanaume na kula naye denda hadharani, akachangua denda!

OKTOBA 2011, GYMKHANA
Maktaba ya Risasi Mchanganyiko inafunga ripoti yake kwa tukio lililotokea Ijumaa iliyopita, Oktoba 28, mwaka huu ambapo kila timu ya Bongo Movie ilipopachika bao, alianza kucheza katika mitindo ya aibu (kama picha zinavyoonekana ukurasa wa mbele).

AUNDIWA ZENGWE
Uamuzi uliofikiwa na baadhi ya wasanii wa kike waliozungumza na waandishi wetu Gymkhana, umeamua kumuundia zengwe ili kukomesha tabia yake hiyo mbaya.

“Kwa sababu tumeshagundua kwamba kila anapokwenda kwenye shughuli za kisanii anaharibu, tutazungumza na uongozi ili kuona kama wanaweza kumfungia kuhudhuria kwenye hafla yoyote ya msanii au inayohusu Bongo Movie.

“Hilo likishindikana, basi bado kuna sababu ya kuongea na uongozi na kuwaambia kwamba kama Lulu akiingia kwenye sherehe zetu basi asinywe pombe kabisa, maana haziwezi. Acha tukazungumze na viongozi wetu halafu tutawajulisha,” alisema mmoja wa wasanii hao.

Lulu ni msichana mdogo ambaye bado ana nafasi ya kubadilika. Ni vyema akatambua thamani yake kama msanii na kuchukua hatua za makusudi haraka.

No comments:

Post a Comment

New