My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, November 7, 2011

Hannibal Gaddafi akijirusha

Hannibal Gaddafi akijirusha na mwanamke aliyetajwa kuwa ni mkewe.

Sifael Paul na Mitandao
PICHA zinazomuonesha mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya aliyeuawa na majeshi ya baraza la mpito la nchi hiyo (NTC), hivi karibuni, Muammar Gaddafi, Hannibal Gaddafi akijirusha na mwanamke aliyetajwa kuwa ni mkewe, Aline ufukweni, zimesambaa katika vyombo vya habari vya magharibi.

Habari kutoka mtandaoni zinadai kuwa zipo baadhi ya picha za Hannibal ambazo zilipigwa wakati tayari machafuko ya kumuondoa baba yake madarakani yakiwa yameshaanza.


...Wakizidi kujivinjari ufukweni.

Picha hizo zinamuonesha Hannibal akiwa kwenye boti binafsi katikati ya bahari mbali na nchi aliyouawa baba yake, Libya huku wakiweka pozi za ‘kimalavidavi’ kitandani na ufukweni.

Kusambaa kwa picha hizo za kimahaba zinazomuonesha Hannibal ambaye inasadikiwa alitorokea nchini Algeria na mama na dada yake baada ya hali kuwa mbaya ni mwendelezo wa chokochoko za kuiandama familia ya Gaddafi ili ionekane ilikuwa ikitumbua rasilimali za umma.

HALI IKOJE LIBYA KWA SASA?
Hali haijatulia nchini Libya kwani vilio dhidi ya vitendo vya ufirauni na mauaji ya kikatili ya Gaddafi bado vinaendelea kwa waliokuwa wakimuunga mkono kiongozi huyo.

Hannibal Gaddafi.

No comments:

Post a Comment

New