My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, April 28, 2017

UTAFITI: Usafi wa kinywa, kinga kwa ugonjwa wa ini

Imeelezwa kuwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa ini wanaweza kuepuka kifo cha mapema kutokana na ugonjwa huo kwa kusafisha kinywa vizuri hasa kusugua meno na fizi.

Kwa mujibu wa stori iliyochapishwa na Daily Mail April 20, 2017, fizi ambazo hazisafishwi vizuri huzalisha bacteria ambao husafiri hadi kwenye ini na huweza kusababisha kifo kwa mtu anayeugua ugonjwa wa ini ambao unatajwa kuwa ni moja kati ya sababu kubwa za vifo ukikamata nafasi ya tano katika nchi za England na Wales.

Wanasaynsi kutoka Aarhus University Hospital, Denmark, walifanya utafiti kwa watu 184 ambao walikuwa wanaugua ugonjwa wa ini ambapo 44% kati yao walikuwa pia na ugonjwa wa fizi uliosababisha vifo vyao huku mmoja wa watafiti hao Dr Lea Ladegaard Gronkjaer, alisema: “Ugonjwa wa fizi unaweza kuwa chanzo cha kuhifadhi bacteria ambao husababisha uvimbe na matatizo mengine katika ini.”

Ingawa matokeo ya utafiti huo yanashawishi, baadhi ya wataalamu wanaonya kuwa uchunguzi zaidi unahitajika kujua athari na kuimarisha usafi kwa wagonjwa wa ini.

Professor Philip Newsome, Mtaalamu wa Ini, University of Birmingham, alisema: “Utafiti huu umeonesha uhusiano baina ya ugonjwa wa fizi na hatari ya kifo kwa wagonjwa wa ini – tafiti zaidi zinahitajika kujua kama utunzaji wa fizi unaweza kuwa kinga kwa ugonjwa wa ini.”

Yajue Mambo 6 yanayosababisha Mbu kukung'ata

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), malaria ni ugonjwa wa pili unaoua watu wengi zaidi ukikadiriwa kusababisha vifo zaidi ya 429,000 kwa mwaka 2016 duniani kote, ambapo zaidi ya 90% ya vifo hivyo vimetokea Afrika.

Licha ya vifo vingi vinavyosababishwa na malaria, lakini kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Kupambana na Magonjwa ya Binadamu (NIAID), mbu anayesababisha malaria huchagua mtu wa kumng’ata ambapo huwa na sababu maalum.

Hizi hapa ndizo sababu zinazopelekea mtu kung’atwa na mbu:

1: Kutoa hewa chafu

Kutoa hewa chafu (Carbondioxide) ni miongoni mwa sababu inayopelekea mbu kukung’ata ambapo kwa mujibu wa Dr. Anandasankar wa Chuo Kikuu cha California,  mbu ana uwezo wa kunusa harufu ya hewa chafu hata akiwa mbali .Watu wanaoathirika zaidi na sababu hii ni watu wanene kwa kuwa ndiyo hutoa hewa chafu inayosabishwa na kuzalishwa kwa acid inayotokana na unene.

2: Kunywa pombe 

Kwa mujibu wa Shirika la Kupambana na Magonjwa ya Binadamu (NIAID), mtu anayekunywa sana pombe yuko hatarini kupatwa na magonjwa yanayosababishwa na mbu. Hii ni kwa sababu mbu huvutika na damu ya mtu aliyelewa kutokana na virutubisho vinavyopatikana kwenye pombe

3: Kufanya mazoezi kupita kiasi

Utafiti huu unaonesha kuwa mbu jike huvutika zaidi na damu ya mtu anayefanya mazoezi kupita kiasi. Hii ni kwa sababu mtu anayefanya mazoezi kupita kiasi hutoa asidi inayoitwa Lactic ambayo hutumiwa na mbu kupata nguvu.

4: Watu wenye kundi O la damu

Watu wenye damu group O hung’atwa na mbu zaidi ukilinganisha na watu wa group A. Mbu hutegemea protini kuzalisha mayai, hivyo watu wenye damu group O huzalisha protini nyingi ukilinganisha na watu wa makundi mengine ya damu.

5: Kuvaa nguo ya rangi nyeusi

Ripoti zinaonesha kuwa watu wanaopenda kuvaa nguo za rangi nyeusi hung’atwa na mbu mara mbili zaidi ya mtu aliyevaa nguo ya rangi nyingine. Hii inasababishwa na mbu kuweza kuona rangi nyeusi kwa haraka ukilinganisha na rangi zingine.

6: Mama mjamzito 

Wanawake wajawazito huathirika zaidi na magonjwa yanayosababishwa na mbu kama malaria, Zika, Dengue na homa ya manjano ukilinganisha na watu wengine. Hii ni kutokana na kundi hili la binadamu huzalisha hormon nyingi na kutoa hewa yenye carbondioxide kuliko watu wengine.

New