My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, November 2, 2011

Jumba la filamu kuzinduliwa Dar

Na Mwandishi Wetu
IJUMAA ya Novemba 4, mwaka huu itakuwa ni siku ya maendeleo katika tasnia ya filamu za Kibongo kwa kufanyika uzinduzi wa jengo la kibiashara la Quality Center lililopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Meneja maendeleo na biashara wa jengo hilo, Sarah Pima amesema ndani ya jengo lao kutakuwa na ukumbi wa kuonesha filamu za Kibongo.

“Hapa hatutachagua filamu pamoja na zile za nje, pia tutaonesha za Kibongo kwa watu watakaokuwa wakifika kupata mahitaji mbalimbali,”alisema Sarah.

Jengo hilo la kibiashara ni kubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na lina huduma za kibenki, michezo mbalimbali ya watoto, sehemu za kuuzia vinywaji, vyakula vya kiasili, supermarket na nguo, pia lina kumbi nne za filamu.


No comments:

Post a Comment

New