My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, June 7, 2012

MADA

DAWA YA MBU ALIYEKUAMBUKIZA MALARIA SIO KUMPIGA BUNDUKI,NI EXPEL TU..
HASIRA HASARA
Idadi ya chuki na hasira unazobeba moyoni mwako kutokana na vile wapenzi wako wa zamani walivyokufanyia vitu ambavyo unadhani hukustahili kufanyiwa,aidha kwa kupigwa kibuti bila kutegemea,au mpenzi kuchukua kipusa kipya na kukutosa kwa kashfa,au kuwa cheated pale ulipopenda sana,kutakufanya uwe kilema wa kupenda siku za usoni.

Kamwe usipende kuingia mahusiano mapya bila kusamehe kile kilichotokea ...kwenye past relationship,ukifanya hivyo,utakuwa kama mtu aliyegongwa na nyoka,hata akiona mkanda mweusi anashtuka.

Utajikuta unaishi kwa dalili,ukiona wingu kidogo unahisi kuna el nino inakuja kumbe ni watu tu wamechoma takataka nyumba ya Jirani....

Jifunze kusamehe waliokutekenya moyo na kuuacha unacheka wenyewe,lasivyo utajikuta unalalamika kwamba huwezi kupenda tena kumbe kosa ni la kwako umeshindwa kuachilia visasi vya Past.Dawa ya mbu aliyekusababishia Malaria kamwe sio kumpiga na bunduki kwa hasira,nunua Expel tu kwa Mangi unampulizia kidogo tu.

No comments:

Post a Comment

New