My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, June 12, 2012

VYAKULA AMBAVYO SI VIZURI KUNUNUA SUPAMARKERT

NI kweli kwamba watu wengi tunapenda kununua vyakula kutoka ‘supermaket’ kutokana na ubora wa bidhaa zake na wakati mwingine hata unafuu wa bei. Lakini ni vyema kujua pia kuwa siyo vyakula vyote vilivyomo humo ni vizuri kiafya.
Katika makala ya leo, nakuletea orodha ya baadhi ya vyakula maarufu vinavyopatikana kwenye ‘supermarket’ na maduka mengine ya bidhaa za vyakula, ambavyo hununuliwa na watu wengi bila kujua madhara yanayowakabili kwa kutumia vyakula hivyo mara kwa mara.

NYANYA ZA KOPO
Nyanya kama ilivyo haina madhara, lakini namna inavyohifadhiwa ndiko kunakoiharibu na kuifanya kuwa na madhara kwa afya yako. Ili iweze kukaa kwa muda mrefu, ni lazima iwekewe kemikali na kopo la kuhifadhiwa nalo, lazima liwekewe kemikali za kulifanya lisipate kutu.
Vitu hivyo havibaki kwenye kopo wakati wa kuitoa nyanya, bali hutoka na nyanya na mwisho huingia jikoni na kuliwa. Hivyo nyanya ya kopo inaharibika na kuwa hatari kwa afya yako kutokana na kuwekewa kemikali za kuhifadhi. Katika mazingira ya kitanzania ambapo nyanya halisi zipo nyingi hadi zinaoza, huna sababu ya kula nyanya za kopo na uache nyanya halisi.
NYAMA ZA KOPO
Nyama za kopo (beef) nayo inaingia kwenye orodha ya vyakula hatari vya supermaket kutokana na kuwekewa kemilaki na chumvi nyingi ili kuifanya ikae kwa muda mrefu bila kuharibika. Ukiacha dosari hiyo, nyama nyingi za makopo, hutokana na ng’ombe wa kufugwa ambao huishi kwa kulishwa nafaka badala ya nyasi na hulishwa madawa mbalimbali ambayo huhatarisha afya ya mlaji.
Nyama bora na yenye kukidhi faida za kiafya ni ile inayotokana na ng’ombe wanaofugwa katika mazingira ya kula nyasi na mimea asilia (organic farming). Kwa mazingira ya kitanzania, huna sababu ya kununua nyama za kopo wakati nyama ipo nyingi buchani. Pia elewa kwamba hata katika nchi zilizoendelea, hivi sasa zinapiga vita ulaji wa nyama za makopo na badala yake zinahimiza ulaji wa nyama ‘fresh’ na wanaofugwa kiasili.
VIAZI, MAZIWA, SAMAKI
Imebainika kuwa kuna ‘viazi ulaya’, maziwa na samaki feki ambao wanapatikana kwa wingi katika ‘supermaket’ nyingi nchini. Imeelezwa kuwa ulimaji wa kisasa wa mazao mengi, vikiwemo viazi hutumia madawa ya kuongeza ukubwa wa mazao kwa teknolijia inayojulikana kama GMO (Genetically Modified Organisms).
Teknolojia hiyo, ambayo kwa sasa inapigwa vita sana dunia nzima, hulifanya zao kuwa kubwa na kuonekana bora kuliko kawaida kwa kutumia ‘madawa’ ambayo yana madhara kwa mlaji. Chips na crips nyingi zinazouzwa supermarket hutengenezwa kutokana viazi vinavyolimwa kwa teknolijia hiyo.
Hali hiyo haiko kwenye mazao tu, bali pia iko kwenye samaki na maziwa. Samaki tunaouziwa ni wale wa kufugwa ambao hulishwa vyakula vya kutengenezwa ili kuwafanya wazaane kwa wingi na kuwa wanene.
Halikadhalika, maziwa mengi ya paketi hutokana na ng’ombe wa kufugwa ambao nao inaelezwa kuwa hulishwa madawa ya kuwawezesha kutoa maziwa kwa wingi na hulishwa vyakula vitokanavyo na nafaka kama vile pumba na mahindi, badala ya nyasi kama ilivyo asili yake.



No comments:

Post a Comment

New