My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, June 7, 2012

MADA II TAFAKARI

SI KILA MPENZI UMPATAYE ATAKUOA..WENGINE NI MITUME TU

Si kila mpenzi ajaye maishani mwako wewe unawaza ndoa tu,na asipokuoa basi unabaki unalia tu na kujihisi una mkosi.

Wapenzi wengine hutumwa tu na Mungu kwa kusudi maalum kwa muda maalum,na kusudi likiisha lazima waondoke,hata ufanye nini!

Si kila mpenzi atakuwa Mke au mume,Nimejifunza kulielewa hili na ninamshukuru Mungu kwa mengi niliyojifunza in my Past relationships.Nawashukuru ALL my past Girl...friends,kwa changamoto na elimu waliyonipatia kuhusu Love,wale mlioutesa huu moyo na kuubondabonda kama Korosho,wale mlionisulubu kisa mlijua nawapenda,mmenifundisha mengi sana,pokeeni Shukrani zangu!

Acha kulialia ukiachika,mara ooh nilimpenda tungezaa watoto wazuri weupe,hilo halikuwa kusudi la Mungu,atakupa mtu sahihi aliyekupangia na utafurahi,yule alikuja kwa kazi maalum tu.

Wake up,Learn and Move On...

No comments:

Post a Comment

New