My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, November 20, 2012

kuna mada ndogo ndogo hapa

1. Msichana akitaka kukutafutia sababu ya kukukataa wala hatumii nguvu,ana full of option,na majibu yao makuu ni haya yafuatayo:
1.We kwanza mweusi na mi mweusi mtoto atakuwa so dark,mi napenda wanaume weupe ili mtoto atoke mzuri..Anaongea kwa kujiamini utadhani kwenye kutunga mimba huwa anamsadidia Mungu kukoroga kopo la rangi ya mtoto...
2.We sio type yangu,sasa sijui type ipi anataka Nokia au Samsung
3.Am not ready,moyo wangu umepasuka...moyo upasuke bado unatembea??Tairi lenyewe likipasuka watu wanaziba pancha...
Kuwa Mwanaume shida,tunapambana na majibu unaweza kumzaba vibao mtu na Love inaisha hapohapo!



 2. Kutokuwa na Trust kwa mpenzi wako ni Kansa mbaya sana,itakumaliza! Kama humuamini unaendelea kuwa naye wa kazi gani??
Mpenzi anaaga anaenda harusini,kiroho kinakusimama,kila muda unampigia simu,asipopokea umenuna,sasa ulitaka aende kutoa zawadi kwa maharusi simu sikioni??
Anatoka Outing usiku,hulali,kila baada ya robo saa unampigia,eti uko na nani hapo,kama kweli uko salama hebu nibusu kwa nguvu,au sema I love you kwa nguvu...Huo ni Wazimu!
Nyie ndo mnakufaga na Presha za kushuka,Huwezi kumpenda mtu usiyemuamini,thats a big lie...
Big up kwa wote mnaowaamini wapenzi wenu,kama wako wako tu,na kama sio wako sio,acheni ukukumaji



3. Ni heri uishi kwenye nyumba ndogo sana lakini ni ya kwako na imetokana na jasho lako,kuliko kujisikia fahari kukaa kwenye nyumba kubwa ya kupanga ambayo si yako..
Ni heri uwe na Msichana wa kawaida,mwenye upendo wa kweli ambaye unammiliki peke yako kuliko kuwa na demu mkali,shape hinhaa,lakini ana wamiliki wengi kama Hisa za Facebook New York Stock Exchange..
Ni heri uwe na Mwanaume wa kawaida mwenye hela za kawaida tu za kubadilishia mboga,lakini mwenye upendo wa dhati kwako kuliko kuwa na Mwanaume tajiri lakini jeuri na anayedhani pesa ni kila kitu kwake,utakuwa mtumwa



4. Akiringa huna haja ya kumbembeleza,kama ni udongo wote mmeumbwa kwa udongo asijifanye kuact kama ameumbwa special na utomvu wa mpapai....
One who loves you will listen and not cause drama for you to get hurt.Be strong and show him/her that you can manage yourself without him/her...Machozi yako ndio power yake ya kuendelea kukunyanyasa.Kujishusha kwako ndio mtaji wake kukuona wewe kama kinyago na takataka.Dont let anyone treat you lesser than what God made you to be.WAKE UP



5. 'baby come home',baby utaniletea chocolate?'babe nimekumiss'..
Kabisa mtu na akili zako unaandika status ya namna hii..Sijui ndo mahaba mapya au mapenzi ya kichina,si umtumie message???mpaka marafiki 5000 na dunia nzima wajue umemmiss babe kwenye wall?
Mapenzi ya simu ya kichina haya,Vibration ina kelele mpaka inafyeka nyasi...wape wiki 8 tu,'love sucks,''being single is better,''never mind i'll find someone lke you,Chinese love doesnt last long



6. Nyie wanawake,kuna baadhi yenu huwa mnajitafutia kuachwa nyie wenyewe!Mwanaume sio ATM ya Umoja Switch,unamtangazia shida zako zoteeeee mpaka anajuta kwanini alikutongoza.Yaani unadate na mtu anakutumia msg,Babe naomba unisaidie kitu kimoja,unajua Baba ameishiwa hela kabisa hapa home hapaeleweki please nisaidie hela'
Khaa!sasa mimi nilikutongoza wewe au nilitongoza ukoo wenu mzima???Babako kuishiwa hela mimi inanihusu nini??Mwambie akadai mafao ya Wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki!Kesho utasema unaomba hela shangazi anunue cherehani...Girls muwe serious,Mizinga kwa sasa ni adui namba moja wa mapenzi!!


7. Mapenzi ya Facebook
DAY 1-Mamboo
DAY 2-Mambo Dear.
DAY 3-Umeamkaje Baby
DAY 4-Babe kuna kitu ntakuomba
DAY 5-Baby can you help me with 200,000,nna shida ntakurudishia kabla ya Ijumaa..Mwanafunzi huyo,na hamjawahi kuonana...Laki 2,airudishe ndani ya mwezi,hata UPATU haizai fasta hivi..Ukijitusu umeumia.Unauchuna
DAY 6-Babe ulipata meseji yangu?Unapiga kimya
DAY 7-Nishagundua we Mwanaume suruali,hata laki 2 huna...We unayo??Ulidhani Mi Mwanaume Sketi???
Mnaonana humu,Mnapendana humu,Mnaachana humuhumu,tena kwa Kashfa..Yeu bora urudi tu,maana watoto wetu hawana wa kuwalea,wanaume na wanawake wote akili kushney



8. Miaka michache nyuma,Wanaume walikuwa wanalalamika sana vibomu vya kuombwa vocha,vocha ilikuwa gharama inayokera sana na kuboa maana kila siku iendayo kwa Mungu ni vocha..
Kumbe bora ingebakia Vocha,maana ina afadhali...Siku hizi,unapigwa mzinga hadi Simu yako inazimika kwanza maana haiamini kilichoandikwa..''Baby naomba laki8 ninunue iPhone simu yangu imeibiwa..dah,laki8 ni mshahara wa Walinzi 5 wa KK security wenye wake na watoto!Mama zao wenyewe wanaisikia tu iPhone wanajua ni Aina mpya ya Kitenge cha Wax...Balaa,hatuhemi,hatujengi,Love has become Article of Oenstation,kui-afford ni ngumu,come on DIVAS give us a break!



9. Mimi sikukatazi KUVAA MINI SKIRT,ila kabla hujaivaa ebu waulizee hata MAJIRANI kama kweli unaMGUU wa mini SKIRT coz wengine wanaovaa mpaka unawaonea huruma,au jiangalie basi hata kwenye KIOO KUBWA...!!      

No comments:

Post a Comment

New