My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, January 14, 2013

Jaji wa kesi ya Tanesco, Dowans sasa asifiwa


Mitambo ya Dowans

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Fredrick Werema na Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, wamemmwagia sifa kedekede Jaji Emilian Mushi kutokana na hukumu ya kesi kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans, dhidi ya Shirika la Umeme (Tanesco).
Katika hotuba zao za kumuaga Jaji Mushi aliyestaafu hivi karibuni, Jaji Werema na Jaji Jundu walirejea hukumu za kesi kadhaa alizozitoa Jaji Mushi kama kielelezo cha umakini, ujasiri, uadilifu na weledi wake, ikiwamo hukumu hiyo ya Dowans.
Msimamo huo wa Jaji Werema na Jundu umekuja wakati Tanesco ikihaha kukata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyosajiri tuzo ya Dowans, iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC).
AG Werema
Katika hotuba yake ya kumuaga Jaji Mushi, Werema alisema kuwa Jaji Mushi katika utendaji wa shughuli zake alikuwa akitenda bila kufungamana na upande wowote, pasipo hofu wala upendeleo, nia mbaya au kuathiriwa na hali yoyote. Akizungumzia kesi ya Dowans, Werema alisema kuwa Jaji Mushi amethibitisha kuwa ni mtafiti, mtu wa kutafakari na mchambuzi wa sheria, huku akiifananisha na chuo cha sheria za usuluhishi wa migogoro ya kibiashara.
“Wale wanaotamani kuwa wataalamu katika usuluhishi, anawashauri kusoma hukumu yake katika shauri la Madai namba 8/2011 linalohusiana na usuluhishi baina ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Dowans Tanzania Ltd ya Tanzania dhidi ya Tanesco.”, alisema Jaji Werema.
Jaji Jundu
Kwa upande wake Jaji Kiongozi, Jundu, akizungumzia hukumu ya Dowans alisema kuwa ni mfano wa jinsi Jaji Mushi alivyokuwa akisisitiza hukumu zinazozingatia ushahidi na ukweli, na kwamba alikuwa mwangalifu, mwadililifu, mweledi, mtenda haki bila upendeleo.
Alisema kuwa katika hukumu hiyo Jaji Mushi alizingatia sana ukweli na ushahidi, pamoja na sheria zinazohusiana na masuala ya usuluhisi..
Kwa upande wake Jaji Mushi pia aliitaja kesi ya Dowans kuwa ni miongoni mwa kesi ambazo hatazisahau katika maisha yake ya ujaji kutokana na changamoto mbalimbali alizokabiliwa.
Alisema miongoni mwa changamoto aliyoipata katika kesi hiyo ni jinsi ya kuwianisha uamuzi wa ICC na kulinganisha na sheria zinazotumika hapa nchini, pamoja na msukumo wa kisiasa katika shauri hilo.
Novemba 15, 2010 ICC, chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen akisaidiwa na wasuluhishi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker, iliiamuru Tanesco iilipe Dowans fidia ya Sh94 bilioni kwa kuvunja mkataba baina yake na kampuni hiyo kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment

New