My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, April 9, 2014

TAHADHARI NA MTANDAO WA UTAPELI UNAOJIITA TCRA FOUNDATION

                             JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                               MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAHADHARI NA MTANDAO WA UTAPELI UNAOJIITA TCRA FOUNDATION

Mamlaka ya Mawasiliano imebaini kuwa kuna mtandao wa matapeli wanaotumia jina la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutumia tovuti inayojiita “TCRA Foundation” na inayodanganya kutoa mikopo kwa maendeleo kwa watu.

Tovuti inayotumika ni http://tcra-foundation.wix.com/tcrafoundation. 
Mtandao huu umetengenezwa wa kutumia picha zilizopo kwenye mitandao mbalimbali  zikiwaonyesha Raisi Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Makawe Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Prof. John Nkoma.

Aidha mtandao huu unadai kuwa Mamlaka kwa kushirikiana na Kampuni za Simu za Vodacom na Tigo pamoja na Benki ya CRDB na NMB zinashirikiana kuendesha Foundation hiyo.

Mamlaka ya Mawasiliano inawatahadharisha wananchi kuwa haina “Foundation” yoyote ya kutoa misaada ya fedha. Mtandao huu unatumika kuwalaghai wananchi na kuwaibia fedha zao kwa kuwataka watume fedha za kujiunga na mtandaqo huo kwa number za simu za Tigo na Vodacom zinazoonesha kusajiliwa kwa jina la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Sio kweli na ni wizi na udanganyifu.

Mamlaka ya Mawasiliano inawataka wananchi kuwa na tahadhari na watu hawa ambao hutumia mitandao ya Mawasiliano ya simu na intaneti kufanya utapeli. Usitume fedha wala kujiunga na mitandao ya namna hii.

Aidha Mamlaka ya Mawasiliano inawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa wanapobaini utapeli wa namna hii kwa kutoa taarifa kwa Mamlaka kwa vyombo vingine vya usalama ikiwa watahisi au kuwa na taarifa za watu wanaojihusisha na udanganyifu huu katika mitandao ya Mawasiliano ili kuzuia vitendo hivi vilivyoshamiri katika siku za hivi karibuni.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
9 Aprili 2014

No comments:

Post a Comment

New