My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, July 21, 2015

MADHARA YA WANAFUNZI KUTOKUPENDA SHULE


Wanafunzi wengi wamekuwa na tabia ya kutokupenda shule. Wengi wao ukiwaliza kwa nini hutoroka masomo na kwenda kwenye makundi yasiyofaa hawajui msingi wake; pengine watakujibu kwa Kiswahili cha kisasa: “Shuleni kunaboa.” Yaani hakufurahishi.
Lakini ukweli ni kwamba mwanafuzni yo yote ambaye hapendi shule moja kwa moja anakuwa amejiingiza kwenye kundi la watu ambao hawawezi kufaulu mitihani na hivyo kujikuta akiwa mtu wa kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo watu ambao hawajasomo; moja kati ya hizo ni kutoheshimiwa, kushindwa kumudu maisha ya kisasa na kutopata nafasi ya kuajiriwa.
Hii ina maana kwamba; kabla mwanafunzi hajaanza safari ya kutafuta ufaulu katika masomo yake, ni lazima ajenge au ajengewe mazingira ya kupenda shule. Kazi hii ifanywe na mwanafunzi mwenyewe, wazazi au waalimu wake ambapo dokezo za kufanikisha jambo hili ni :
KWANZA:  Kuwepo kwa ushirikiano mzuri kati ya wazazi, waalimu na mwanafunzi. Siku hizi wanafunzi wengi wamekuwa wajeuri kwa waalimu wao na hivyo kuwafanya wakose ushirikiano wa kimasomo jambo ambalo halifai. Mwanafunzi lazima ajenge urafiki na waalimu wake, suala hili liende sambamba na uhusiano mzuri kati ya wazazi na waalimu shuleni.
PILI: Ushirikino mwema kati ya mwanafunzi na wenzake. Wanafunzi wengi wamekuwa na tabia za kugombana na wenzao mara kwa mara hivyo kuifanya shule kuwa na maadui ambao mwisho wa yote humfanya mwanafunzi asipende kwenda masomoni; ushauri wa kitaalamu ni kwamba, mwanafunzi hatakiwi kuonesha tabia mbaya kwa wenzake, ajitahidi kwa kila hali kujenga urafiki na wenzake ambao mwisho wa siku atapenda kukutana nao kila siku.
TATU: Kuichukulia shule kama njia ya kuelekea kwenye mafanikio ya kimaisha hivyo kuikosa ni sawa na kujiweka katika msingi wa maisha magumu.
Mwanafunzi; kila siku uamkapo asubuhi ichukulie elimu kuwa ni sehemu ya mafanikio yako, wazazi unaotegemea leo wanaweza kufariki lakini ukiwa na elimu yako haitakufa pamoja nao. Waswahili husema, elimu ni ufunguo wa maisha siyo wazazi.

No comments:

Post a Comment

New