My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, September 25, 2012

Afueni kwa wanafunzi wa Kenya



Wanafunzi darasani Kenya 

Shule za umma nchini Kenya zimefungua hii leo baada ya wiki tatu za mgomo wa walimu.
Walimu hao hatimaye waliweza kuafikia makubaliano na serikali kuhusu matakwa yao ya nyongeza ya mishahara.
Serikali ilitishia kuwafuta kazi walimu hao Ijumaa wiki jana wakati walipokataa pendekezo la asilimia 4 ya mishahara ambalo serikali ilitoa.
Lakini makubaliano hatimaye yaliafikiwa mwishoni mwa wiki ya nyongeza ya asilimia arobaini.
Sasa mwalimu atakayepokea mshahara mdogo zaidi kuliko wote atalipwa dola 140 huku mwenye kulipwa mshahara mkubwa akipata dola 1,700 .
Sekta ya umma nchini Kenya imekumbwa na migomo katika wiki chache zilizopita. Hospitali za umma ambazo pia zilishuhudia mgomo wa madaktari, zinawahudumia tu wagonjwa walio katika hali ya dharura.
Vyuo vikuu vya umma navyo vilifungua siku ya Jumatatu baada ya wahadhiri ambao pia walikuwa wanagoma kurejea kazini.
Kupanda kwa gharama ya maisha na mkakati duni wa serikali kuweza kushughulikia matatizo ya wananchi hususan swala la mishahara ndio mojawapo ya sababu ya kutokea kwa migomo hii.
Walimu hao 200,000 walitaka nyongeza ya asilimia miamoja hadi miatatu .
Kulingana na makubaliano hayo yaliyotiwa saini na waziri wa fedha Njeru Githae na chama cha kitaifa cha walimu, marupurupu ya walimu pia yataongezeka hasa kwa wale wanaofanya kazi katika mazingira magumu na wale wanaowahudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Mitihani ya mwisho wa kidato cha nne na darasa la nane ilitaakhirishwa kwa wiki tatu ili kuwawezesha wanafunzi kuajindaa vilivyo.

No comments:

Post a Comment

New