My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, September 1, 2013

dhana-mbaya-zinazowarudisha-watu-wengi

Watu wengi wana mitazamo mibaya wanayodhani ni sahihi lakini sio kweli, tafakari haya mambo niliyooredhesha hapo chini. Kudhani hivyo kama watu wengine wanavyofikiri kunaweza kukufanya usifanye mambo yako kwa kiuhalisia zaidi na kukupelekea usipate matunda mazuri kama unavyotegemea. 
1. Kuwa busy ni kufanya kazi nyingi kwa siku.
-Kutingwa na mambo mengi  hakumaanishi ndio unafanya kazi  kwa tija. Watu wengi hudhani kuwa busy sana ndio kupata mafanikio lakini hebu fikiria hili ‘’You Might Be Busy For Nothing Instead Of Something.’’ Ninachomaanisha hapa ni kwamba sio lazima ukiwa busy ndio kuwa utafanikiwa au kupata matokeo mazuri, unachotakiwa ni kujipanga vyema na kujua nini unafanya. Jishughulishe kwa malengo kwa kujua zao la kazi zako ni nini.

2. Kuwa jasiri ni kutoogopa.
-Ni muhimu uwe jasiri lakini sio kila kitu ni cha kukiwekea kifua mbele pasipo kufikiri. Tumeona watu wengi wameumia kwenye mambo ya hatari au hata kuharibu mambo mbalimbali katika maisha yao kama kuvunjika kwa mahusiano kwaajili ya kukomalia mambo yasiyo ya msingi, kuhatarisha maisha kwa kujifanya huogopi hata kama ni kitu hatari na mambo mengine ya kukuletea hasara. Kuwa imara na mwenye msimamo kwenye mambo mazuri na yenye faida pia ogopa vya kuogopwa na sio kila kitu ni cha kuogopa. ''Fear fear, and not everything have to be feared.''

3. Kuwa shupavu ni kuvumilia pasipo kuumia.
-Kuna mambo mengine ambayo yakikuumiza lazima uonyeshe kuwa umeumia. Tena haswa sisi wanaume mara nyingi huwa tunajifanya hatujaumia hata kama ni kweli tumeumizwa. Kuonyesha kuwa umepatwa na maswahibu haimaanishi kuwa wewe ni bwege au ni mnyonge bali wakati mwingine ina maanisha kuwa wewe ni shupavu kwa kukubali matatizo yaliyokukumba. Ukijisikia kulia ni vyema ukalia ukayamaliza kuliko kukaa nayo moyoni na kuteseka nayo bila sababu. Siku zote kuwa mkweli kwa furaha na majonzi yako kwa kueleza chochote kilichopo ndani mwako. ''Be open to your happiness and sadness.''

4. Kuamua kuwa utajisikia furaha pale tu utakapofanikiwa kupata vitu fulani kwa watu wengine.
-Huwezi kukimbia matatizo, na si vyema uwe mpweke na mwenye majonzi wakati wote kwa sababu ya matatizo. Usihuzunike leo ukitegemea utakapopata kesho kitu fulani ndio utafurahi. Ukifanya hivyo utakuwa unajidhulumu maisha yako, kuwa na furaha kulingana na hali yako au chochote ulichonacho hata kama ni kidogo. Muhimu hapo ni kuwa mvumilivu, mtafutaji na mwenye imani kuwa utafanikiwa utakacho.

5. Kuamini umechelewa kwa kila jambo unaloona sio wakati wake.
-Kuna msemo unaosema ‘’It’s Never Too Late’’ nami naamini hivyo kwasababu kwa kila jambo unalokosea leo kuna nafasi nyingine ya wewe kurekebisha mambo yako na kuyaweka vizuri kama unavyotaka. Hebu fikiri kama ungekuwa na siku ya leo tu pasipo kuwa na kesho ungefanya nini? Lakini kwa bahati nzuri una kila sababu ya kuona hujachelewa kufanya mambo yako kwasababu kama umeshindwa leo basi jiandae vizuri kesho utaweza. JipangeWeka nia na Tekeleza utakalo.

6. Kutegemea kuwa utajisikia amani pale muda mzuri utakapowadia.
-Kama huna amani sasa hivi usitegemee utakuwa mwenye amani hapo baadae. Amani huletwa na wewe mwenyewe kwa kutuliza moyo wako. Usifanye muda kukupangia amani yako bali kuwa na imani mambo yatakuwa vizuri tu maana hata ukifikiri vibaya utajiumiza bure pasipo kuwa na maana. Hakuna muda mzuri wala mbaya bali kuna hali nzuri na hali mbaya, na kiukweli  kabisa hakuna hali ya kudumu, kama una hali mbaya leo haitadumu milele ikiwa utaamua kubadilisha mambo. Muda mzuri utawadia iwapo utaamua kubadilsha hali yako kwa kutatua shida zako. Ufumbuzi wa shida zako ndio amani na furaha yako na sio muda kama watu wanavyodhani.
- See more at: http://www.kamotta.blogspot.com/2013/07/dhana-mbaya-zinazowarudisha-watu-wengi.html#.UiJ2YL_4JSp

No comments:

Post a Comment

New