My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, September 1, 2013

Pata sababu kumi (10) za wewe kuwa jasiri



Sababu kumi (10) za wewe kuwa jasiri.


Kuwa jasiri ni ule uwezo wa mtu kutenda jambo fulani pasi na uoga. Ujasiri humfanya mtu kutekeleza na kufanikisha mambo yake.

UJASIRI + NIA + KUTEKELEZA = MAFANIKIO.

''This is Jules founder of The Confidence Garden, she is a coach, speaker, trainer and author here explaining to you how to build and gain confidence.''



 Kama mtu atakosa ujasiri ni vigumu kwake kufanikiwa labda angalau afanye jitihada za kufanya jambo alilokusudia ili afanikiwe. Hii ni sawa na mu anayetaka kufika mahali fulani, mtu huyo hawezi fika anapokusudia mpaka aondoke na kwenda mwenyewe anapopataka.
Kwa kuwa kukosa ujasiri kunamfanya mtu ashindwe kutenda na kufanikiwa atakalo zifuatazo ni sababu za wewe kuwa jasiri ambazo zitakupelekea wewe kufanikiwa.

1. Ujasiri humfanya mtu atekeleza mambo yake.
Watu jasiri hutenda na kufanikisha watakalo, hawaoni aibu kufanya mambo yao ikiwa wapo sahihi na lile wafanyalo.

 2. Ujasiri humfanya mtu kujisimamia mambo yake mwenyewe bila uoga.
Kwa kuwa na ujasiri unaweza kusimama kidete kwa lile unaloona ni sahihi na unapaswa ni kulisimamia. Lahasha ukiwa jasiri huwezi kudhuliumiwa au kuonewa kwa kuwa utasimamia haki yako.

3. Ujasiri humfanya mtu aweze kusema hapana.
Neno HAPANA, ni rahisi kwa mtu mwenye ujasiri kusema SITAKI pale panapobidi kukataa.


 4. Ujasiri humfanya mtu aweze kusema ndiyo.
-Neno NDIYO pia hutumika na mtu jasiri pale anapokubaliana na jambo fulani au penye fursa kila inapojitokeza. Mtu jasiri haoni aibu kusema’’ NDIYO’’ pale anapotaka kitu chochote.


 5. Ujasiri humfanya mtu kutokuwa na uoga.
-Kukosa ujasiri kunaweza kumfanya mtu ashindwe au kufeli mtihani wowote wa maisha. Mtu kuogopa kushindwa , mtu kufikiri hawezi kufanya jambo lolote akafanikiwa ni sababu kubwa ya watu wengi kushindwa kufanikiwa . Uoga huondolewa kwa mtu kuwa jasiri.

6. Ujasiri humfanya mtu ajiamini.
-Kujiamini ni silaha kubwa ya kukusaidia kutenda mambo yanayokuletea mafanikio. Henry Fordmwanzilishi wa kampuni Ford Motors alisema ‘’Whether You Think You Can, Or You Think You Can’t - You’re Right.’’


 7. Ujasiri humfanya mtu ajiwekee malengo ya juu kimafanikio.
-Watu jasiri hujiamini na kutegemea matokeo makubwa kwa kuwa wanajiamini kwa yale wanayoyafanya. Hata wewe ukijiwekea mategemeo makubwa na kuweka jitihada nyingi kwa kitu unachotaka kufanikiwa utapata kile kikubwa ulichotegemea.

8. Ujasiri humfanya  mtu kutenda mambo makubwa kuvuka mipaka ya uwezo wake.
-Ujasiri hukufanya ujue mipaka  ya  uwezo wako na kutenda mambo kwa kadri unavyoweza. ‘’You’re Stronger Than You Think, By Stretching Your Limits You Can Increase Them To Your Maximam Level.”


 9. Ujasiri humfanya mtu ajiamini kuwa atashinda.
-Mtu jasiri huamini kuwa atashinda , huu ni ukweli kuwa washindi hutegemea kufanikiwa kwa kuwa wamejianda kushinda na hupata ushindi kwasababu wanastahili kupata walichokusudia. Matokeo mazuri hutegemea ulichopanda. Hakuna ushindi au mafanikio ya kubahatisha kama una ndoto za kufanikiwa anza leo kujiwekea malengo.


10. Ujasiri humfanya mtu aulize maswali au ajieleze anachotaka.
-Ukiwa na ujasiri unaweza kujieleza mwenyewe kwa mtu/watu unachotaka na wakakusikiliza. Ukweli wa maisha ni kwamba huwezi pata chochote bila kuuliza au kuomba upewe. Mfano: Unataka kazi sharti uombe, ukitaka msaada omba usaidiwe nakadhalika. Vilevile ujasiri humfanya mtu aulize maswali pale anapotaka maelezo kuhusu kitu fulani, kwa kuuliza unajifunza, unaelewa na kupatiwa majibu ya maswali uliyouliza.

No comments:

Post a Comment

New