My Web

Emmanuel

CONTACT

Saturday, April 18, 2020

Maono ya kuzingatia

Wapendwa wana wa Mungu nawasalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo,Ningependa nitumie muda huu kushare nanyi hili jambo la muhimu nililopata ufunuo ktk siku tatu hizi na nimepewa ruhusa kwa kibali cha Yesu kuleta kwenu. 

Sasa atakaelichukua kwa kumaanisha atafaidika nalo.

Nilipelekwa katikamlima mmoja mrefu sana nikawa naiona dunia yote kwa chini na watu wake wote.

Kwa kweli lilikuwa jambo la kustaajabisha sana nikaona watoto wadogo na wazee kwa vijana wakiugulia maumivu na wengine wakipoteza maisha.

Nikamuuliza yule mzee niliekuwa nae alikuwa anang'aa mwili wote na mavazi yake meupe kama theluji nikamuuliza nn maana ya haya yote akaniambia subiri hujaona yote nikashuhudia

Nikapelekwa ktk nchi nyingi watu wanakufa wengine wameachwa kwa sababu ya kukosa watu wa kuwazika nikawa nashangaa tu,

Nikapelekwa katika jumba moja kubwa nikakuta watu wamevalia suti nyeusi wapo katika kikao kizito na muongozaji wa kile kikao alikuwa na pembe mbili na sura yake kama beberu lakini akiwa anaongea kwa ukali sana nikamuuliza yule mzeehiki kikao ni cha nini?

Akanieleza hawa ni wakuuu wa nchi zote wamekutana hapa kujadili mstakabali wa mataifa yao kuhusu vifo vinavyowakabili na ni kiongozi wa nchi moja tu ambae hayupo hapo nae ni wa nchi yako. Na kikao hiki kimemkasirisha sana Mungu ila pamoja na kiongozi wako kutokuwepo hapa hakufanyi nchi yako watu wake kutokufa na nitakueleza kwa nini.....

jasho jingi likaanza kunitoka baada ya kuona watu wa nchi yangu wakifa ila sio kwa wingi kama nchi zingine nikamuuliza yule mzee kwa nini haya yote yanatukia,akanijibu watu wamejitenga na Mungu na kwa nchi yako kuna Neema ipo ila watu wa nchi yako wasipoomba kwa kumaanisha Neema hiyo itatoweka na watu wengi watakufa ,akaniambia  lango la nchi yako li wazi bado halijafungwa.

Nikamuuliza nitalifungaje akacheka sana akaniambia Omba kuhusu Rais wako asije badili mawazo akaenda katika kile kikao na ombea Taifa lako na ardhi ya Taifa lako wakati huu Neema bado ipo ili kuzuia maagano yote yanayoendelea ktk kile kikao yasipenye kuja ktk ardhi ya nchi yako,ungana na wanamaombi wote walio tayari katika kuiombea nchi yako..... Fungeni mipaka yote ya nchi kwa Damu ya Yesu na mzuie maagano yote ya kishetani kuingia ktk ardhi ya nchi yako 

maagano hayo ni ya kiuchumi magonjwa na mafarakano. 

Akanishusha katika ule mlima akanikumbusha, "Usiache kumuombea Rais wako Mungu amfunike na asahau kabisa kuhusu kuhudhuria kile kikao".

WAPENDWA, kwa uaminifu nitaingia kwenye maombi ya kufunga kwa siku saba kavu kuanzia kesho na mambo ya kuombea ni kuhusu Taifa langu na ardhi yake pia kumuombea Rais wetu aendelee kushikilia msimamo wake wa kumlilia Mungu na asihudhurie kikao chochote cha marais watakaoitwa kwenye vikao vya siri.

Wapendwa atakae guswa katika hili aungane na mimi ktk maombi haya hata unashindwa kufunga omba nami japo masaa mawili ili tuiponye nchi na janga hili linalotukabili.

NAWABARIKIWOTE KWA JINA LA YESU NA NINAWATANGAZIA KWA KILA FAMILIA ITAKAYOMLILIA MUNGU HAITAKUFA NA JANGA HILI LA CORONA.

#SHARE HII MARA NYINGI ZAIDI, UTAKUWA UMEFANYA HUDUMA KUBWA SANA.....NAMI NIMESHARE TOKA KWA MWINGINE KUUNGANA NA MWONAJI WA MAONO HAYA MAZITO YA NCHI YETU PENDWA.

Usalama  wa Tanzania na watanzania.....hususani dunia yote, upo KWENYE KUJITENGA NA UOVU PAMOJA NA KUOMBA.

No comments:

Post a Comment

New