My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, December 10, 2012

Korea Kaskazini yaahirisha urushaji roketi

Korea Kaskazini inasema kwamba imeongeza muda wa uzinduzi wa roketi yake ya masafa marefu ili kukabiliana na hitilafu za kimitambo katika injini ya roketi hiyo.
Uzinduzi huo, uliokuwa uanze leo, sasa umesogezwa na kupewa muda hadi 29 Desemba.
Jaribio la awali ili kujaribu kurusha roketi hiyo mnamo mwezi Aprili halikufaulu.
Korea Kaskazini inasisitiza kuwa roketi hiyo ni ya amani ili kutuma setilaiti angani, lakini Marekani na mataifa mengine yanasema kuwa hilo ni jaribio la kurusha kombora la masafa marefu kutoka bara moja hadi jingine.

No comments:

Post a Comment

New