My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, December 10, 2012

Polisi yakiri wizi bandarini ni mtandao

  

Waziri waUchukuzi,Dk Harrison Mwakyembe

 Jamani tupo kazini, wizi uliotumika siyo wizi huu wa kawaida bali ni wizi wa mtandao, wapo walioghushi  nyaraka ndizo zimetumika  kufanikisha wizi, hivyo tunafanya uchunguzi kubaini wahusika wote,” alisema.

KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Bandari, Foturnatus Muslim amesema katika uchunguzi wa awali wamebaini  wizi uliotumika kuiba shaba na mafuta ni wa mtandao.
Akizungumza kwa simu jana,  Muslim alisema ili kuhakikisha wanafanya kazi ya kukomesha vitendo vya wizi bandarini, wanalazimika kufanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo.
“ Jamani tupo kazini, wizi uliotumika siyo wizi huu wa kawaida bali ni wizi wa mtandao, wapo walioghushi  nyaraka ndizo zimetumika  kufanikisha wizi, hivyo tunafanya uchunguzi kubaini wahusika wote,” alisema.
Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe hivi karibuni alihoji kuhusu maendeleo ya kesi ya wizi wa shaba lenye kumbukumbu namba KLB /IR/3067 /2012 na ya wizi wa mafuta yenye namba KLR 3068/2012.
Kesi hizo hadi sasa zinajumuisha washtakiwa 13.
Hata hivyo, imeeleza kuna polisi ambao wanatuhumiwa kuhusika kusimamia wizi huo, hawajaunganishwa na wenzao.  
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikaririwa na vyombo vya habari juzi akieleza kwamba upelelezi wa kubaini polisi waliohusika unaendelea.

No comments:

Post a Comment

New