My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, March 6, 2016

BINTI YANGU..,



Sasa nikijitazama Nimekua Mzee, Nikikutazma Usoni namkumbuka Mama yako, Nalikumbuka Tabasamu lake na ile sauti yake ya kubembeleza. Nafurahi kukuona sasa Umekua na unanipa Heshima yangu nikiwa Baba Mwema kwako.

My daughter, Kumbuka  kuanzia kesho hutakuwa ukiitwa tena jina langu. Utakuwa na furaha kuolewa na mwanaume uliyempenda. Please  Usini miss mimi kwasababu nimeshatimiza majukumu yangu. Sasa ni wakati wa kutimiza majukumu yako.

Kuanzia utoto wako, nimekulea vema kwa neema za Mungu. Ila kabla hujasema mbele ya Shekh kuwa unakubali kuolewa ningependa nikueleze kuhusu kuishi na mwanaume na maisha ya ndoa kiujumla.

Unakumbuka ulivyokua umekaribia kufanya mtihani wako wa mwisho wa kidato cha sita?

 Unakumbuka Ulikuja kwangu na nikakupa laki moja kwa ajili ya maandalizi ya mtihani?  Nakumbuka ulifurahi sana na ukaibusu Mikono yangu huku ukionesha Tabasamu la Dhati juu yangu, Sawa ingawa nilikupa mimi, lakini ukweli ni kwamba pesa ile ilikuwa sio yangu.

Najua siku zote ulikua ukijua kuwa mimi ndiye niliyekuwa nikikulipia ada. Ukweli ni kwamba mimi nilikua katika wakati mgumu, Sikua na kzi sikua na mbele wala nyuma...

Lakini mama yako alinipa pesa zake. Angeweza kukupa wewe moja kwa moja ila aliamua kunipa mimi kwanza ili nikupe, Alihitaji kuilinda Heshima yangu kama Mume kwake na Baba kwako.

Hii inamaanisha nini mwanangu, msupport mume wako! Muda mwingine atakutana na changamoto katika maisha na kukutana na ugumu wa maisha, madeni na vinginevyo ingawa ataonekana yuko sawa ila akilini mwake anayo hofu na majonzi makuu...Atahisi hutaweza kumthamini tena kwa vile mambo yamemuendea kombo. Huo ndio muda ambao itakubidi kuwa nae bega kwa bega ukimfariji na kumfanya kuwa na furaha wakati wote.

Mwanangu njia sahihi ya kumuonesha mume wako kua unampenda ni kumuheshimu, najua inaweza tokea ukabishana nae, ukakwaruzana nae ila mwisho wa siku mwache ajue kuwa heshima yako kwake iko pale pale.

Mwanangu unakumbuka siku ile nilipomkaripia vibaya sana mama yako? Alifanya nini? Alibaki kimya kabisa. Unakumbuka pia siku ile mama yako alivyonijia juu? Nilifanya nini? Nilibaki kimya kabisa!

Binti yangu jifunze kuwa Kimya muda mwingine pale mume wako atakapokuwa na hasira. Mmoja kati yenu atakapokuwa na hasira na gadhabu  mmoja lazima atulie kimya. Kama wote mtaanza kupandishiana hasira tatizo hapo ndio huibuka. Na matatizo ya ndoa ndio huanzia hapo.

Mwanangu kitu cha kwanza kujua kuhusu mume wako ni chakula anachokipenda. Kama anapenda vyakula vya aina nyingi weka katika akili yako. Usiache mpaka aombe chakula siku zote muandalie wewe, Usimpe nafasi ya kutafuta chakula akipendacho kwa jirani.

Binti yangu kuna siku mama yako alinikuta nikiwa nimemshika mwanamke mwingine mkono, hakuwa mchepuko wangu ila ni rafiki yangu nikiyepotezana nae kitambo. Mama yako aliponiona hakuanzisha ugomvi na yule mwanamke. Aliondoka kimya kimya.

Nilikuwa na hofu  kurudi nyumbani, ningemwambia nini anielewe? Lakini niliporudi nyumbani hakunisema chochote. Aliniandalia chakula mezani kama kawaida. Ila nafsini nilijiona kama nina hatia. Nikaanza kumuomba msamaha. 

Kuanzia siku ile sikukaa kumtazama mwanamke wa pembeni mara mbili. Nani anajua? Je kama mama yako angegombana na mimi siku ile, labda ningeondoka nyumbani nakuangukia katika mikono ya mwanamke yeyote tu barabarani akanipoze. 

Muda mwingine ukimya huleta ufumbuzi mkubwa kuliko ugomvi.

Mwanangu Sahau kuhusu riwaya za mapenzi ulizosoma ulipokuwa shuleni. Unakumbuka filamu za kihindi na za kimarekani? Unakumbuka filamu za kitanzania na Kinaijeria? Unakumbuka tamthiliya za kifilipino? Nyimbo za westlife na Diamond,  unazikumbuka?  Maisha ya kina Wema na Zari? Sahau kabisa hayo mambo mwanangu! Usitegemee vitu ulivyokua ukiviona huko vitakuwepo katika ndoa yako. Maisha halisi ni tofauti na hadithi za kufikirika.

Kitu cha mwisho nachotaka nikuambie... Unakumbuka jinsi ulivyozaliwa? Sijawahi kukwambia!

Nilipanga kuja kukwambia siku utakapokua tayari kuishi ndani ya uhalisia.

 Baada ya ndoa yetu mimi na mama yako mambo yalikuwa magumu. Na mama yako ilimlazimu afanye kazi mbili kusupport familia. Nami pia nilikuwa nikifanya hivyo. 

Nilikuwa nikirudi nyumbani saa moja jioni na mama yako alikuwa akirudi saa mbili usiku akiwa amechoka. Lakini tulipoenda kulala hakuninyima chakula cha usiku kitandani. Na kwa jinsi hii ndipo ulipozaliwa. Usijenge tabia ya kumyima mumeo chakula chake akipendacho cha usiku. Maana kufanya hivyo sio kumkomoa bali ni kuiharibu ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe. 

Kuwa mke mwema, na utakuwa binti yangu nitakae jivunia mpaka naingia kaburini....., Naamini Mama yako atakua anatabasamu huko Mbinguni kwa kuwa umemlindia Heshima yake hapa Duniani.

#Nakutakia Maisha Marefu ya Ndoa Binti yangu...,

No comments:

Post a Comment

New