My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, March 29, 2016

JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA.!



1. #Mathayo.
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali kwa kutetea kanisa. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.

2. #Simoni_Zelote (Mkananayo)
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishowe akafariki.

3. #Filipo
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.

4. #Yohana (nduguye Yakobo)
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na  alitolewa akiwa mzima kabisa. 

Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.

5. #Simoni (Petro)
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisulubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya "X". Petro mwenyewe aliomba asulubiwa kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18)

6.#Yakobo (wa Alfayo)
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe.  Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga na mawe mpaka akafa.

7. #Yakobo (mwana wa Zebedayo nduguye Yohana)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa lakini alichinjwa huko Yerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).

8. #Batholomayo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo. Alipigwa fimbo nyingi zilizochubua ngozi yake na kutengeneza vidonda. Kisha akawekewa chumvi ktk vidonda hivyo, na kuanikwa juani hadi mauti ilipomfika.

9. #Andrea
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la "X" miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri sana saa kama hii"

10. #Tomaso
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko.

11. #Yuda (Thadayo)
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

12. #Yuda (Iskariote)
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha. Alinunua shamba kwa zile fedha alizomuuza nazo Yesu. Lakini alijinyongea kwenye shamba hilohilo. Kamba aliyojinyongea ilikatika na akaanguka na tumbo lake kupasuka na matumbo kutoka nje. Shamba lile likaitwa "Akel Dama" yani Shamba la damu (Matendo 1:18-19).

NOTE:
13. #Mathia
Ni Mwanafunzi aliyechaguliwa kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (msaliti). Alipigiwa kura na wanafunzi 11 wa Yesu baada ya kifo cha Yuda (Matendo 1:26). Huyu alipigwa na mawe  hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

14. #Paulo
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka 65 (A.D). 

Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.

NB: Si muhimu kujua ni namna gani mitume walikufa, ila ni muhimu kujua kuwa mitume wote walikufa wakitetea imani yao. Walikua tayari kuchukiwa na kufa vifo vya mateso kwa ajili ya kumtetea na kumshuhudia Kristo.

Biblia imesema, "Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka." Mathayo Mtakatifu 10:23


No comments:

Post a Comment

New