My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, March 1, 2012

Lengo la Uingereza ni kutaka kutuingiza katika laana

David William Donald Cameron.

MUNGU ni mwema na ndiyo maana leo tunakutana tena, yatupasa sote tumshukuru kwa kutuweka hai na kuniwezesha kuwaletea machache ambayo naamini yatasaidia kujenga nchi yetu ili kusonga mbele kimaendeleo.

Leo nitazungumzia shuruti la Uingereza kwa nchi ambazo zilikuwa makoloni yake, kwamba ili waendelee kutoa misaada kwao pamoja na vigezo vingine basi ni lazima watu wake wamkatae Mungu aliyezuia ushoga na kuiteketeza Miji ya Sodoma na Gomora na nchi hizo zitunge sheria kuruhusu wanaume kwa wanaume au wanawake kwa wanawake kuoana!

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, hakusema kwa bahati mbaya, alikuwa akiwahutubia wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola huko Perth, nchini Australia hivi karibuni baada ya mkutano huo kufunguliwa na Malkia Elizabeth 11 wa Uingereza.

“Nitazuia misaada kwa nchi zote ambazo hazitatambua haki za watu wanaojihusisha na ushoga ikiwemo kuruhusu ndoa ya jinsi moja,” yalikuwa ni maneno ya hovyo ya matusi ya Bw. Cameron kwa wakuu mbalimbali wa nchi.

Ingekuwa hapa nyumbani, huyu bwana angeambiwa amekosa adabu kwa sababu kimaadili huwezi kuzungumzia nambo ya kishoga kwa watu wazima, tena wanaoongoza watu. Sikuwepo kwenye kikao hicho, lakini naamini viongozi wa Kiafrika waliokuwepo pale walijihisi kuwa wametukanwa matusi ya nguoni.

Bw. Cameron hakujua kwamba katika mikutano yote ya viongozi wakuu wa nchi ushoga siyo sehemu muhimu ya vigezo vya kuipa misaada nchi? Huyu bwana ametumwa na nani kututusi watu wa dunia ya tatu? Haelewi kuwa kutenda, kuona, kushabikia au hata kuwa na mashoga ni chukizo kwa Mungu?

Kama ushoga ni muhimu, kwa nini Cameron na washirika wake wasiipe sharti hilo Ugiriki ambayo licha ya kuwa katika bara moja, ina matatizo mazito ya kiuchumi?

Ndugu zangu, naamini hili lingekubalika, tungewachekea ipo siku wangesema ili watupe misaada watataka kuwepo na vyama vya siasa vya mashoga.

Pamoja na utetezi uliotolewa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Diane Corner, ambaye tunajua Bw. Cameron ni bosi wake, kwamba eti kigezo cha misaada siyo kimoja, ukweli ni kwamba Jumuiya ya Madola inapoteza dira na natabiri kwamba siku zijazo itakataliwa na wanachama wake ikiwa Waingereza wakiendelea na upumbavu huo.

Hii ni laana kubwa sana ambayo Bw. Cameron anataka kutuingiza, yaani anataka nchi zinazoiomba misaada zigeuke kuwa ‘Sodoma na Gomora’. Hajui kwamba Mungu aliiangamiza miji hiyo na wale wote waliokuwa wakisikia au kuona upuuzi huo hata bila kufanya tendo?

Cameron aelewe kuwa ushoga katika nchi hii ni haramu maana hata mbwa hawafanyi upuuzi huo, wana utaratibu maalum unaozingatia mpango wa Mungu katika uumbaji.

Uingereza inaanza kupenyeza makucha yake ili hatimaye ije tena kututawala Waafrika, ni ukoloni mambo leo. Mifano ya Uingereza na washirika wake kunyanyasa Waafrika ipo na wa hivi karibuni ni jinsi walivyofanya unyama kule Libya.

Wameua watu kwa kushirikisha Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO), wamebomoa miundombinu ambayo iliwachukua Walibya miaka mingi kuijenga na wakazuia akiba kubwa ya fedha zao za kigeni. Huu ni umwamba.

Ni lazima tumuambie Cameron kuwa misaada ambayo ina masharti ya kipuuzi hatuikubali. Uingereza ikiona kuwa utajiri wake unaweza kuchukua nafasi ya Mungu, tunawaomba wakae na mali zao hukohuko kwao na kamwe hatutakubali kumdharau Mungu ili kuwatetemekea wao.

Waafrika wako tayari kufa kwa umaskini kuliko kukubali misaada ya kidhalilishaji kama hiyo, tena basi ya kumdharau na kukiuka amri za Mungu.

Niwapongeze viongozi wa Kiafrika waliyoilaani Uingereza kwa tamko lake hilo la kuhimiza ushoga, hao ni Rais wa Ghana, John Atter Mills, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini, Bernard Membe.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Observer la Uingereza katika utafiti wao waliouchapisha Oktoba 2008, nchi za Ulaya baadhi ya watu wanapenda sana ushoga na ndoa za jinsi moja ambapo nchini Uingereza asilimia 55 walionesha kupenda vitendo hivyo vichafu.

Gazeti hilo limefanya utafiti na kubaini kuwa Uholanzi watu wanaotaka ushoga ni asilimia 82, nchi nyingine na asilimia katika mabano ni Sweden (71), Denmark (62), Ubelgiji (62), Luxembougr(58), Jamhuri ya Czech (52), Ufaransa (62) na Ireland (51).
Nchi ambazo raia wake waliohojiwa na kukubali kuwepo na mashoga kwa asilimia chini ya 50 ni Romania, Bulgaria, Poland, Hungary, Malta, Cyprus nakadhalika.

Dhambi hii imeathiri Kanisa Katoliki na kumfanya Papa Benedict XVI kuomba radhi kila nchi anayotembelea kutokana na madai kuwa mapadri wa kanisa hilo ‘waliwashughulikia kingono’ wavulana.

Ndugu zangu, hata Kanisa la Anglikana duniani lipo hatarini kumeguka kutokana na tawi lao la Marekani ambao ni marafiki wakubwa wa Uingereza kuruhusu ushoga.

Kiukweli Ulaya na Marekani tamaduni na maadili yao wamekoroga na sasa wanaangalia jinsi ya kutuchanganya na sisi Waafrika katika laana hiyo.

Waafrika wote tulinde maadili yetu na tukatae ushoga kwa nguvu zote kwa sababu hilo ni agizo la Mungu na tusikubali kuchezewa na kutenganishwa na Mungu kwa kisingizio cha misaada. Ni kweli misaada inakaribishwa lakini tujiulize inakuja kwa masharti gani na katika muktadha gani? Isiwe kwa sharti la wanaume kwa wanaume kuoana, ni hatari, tusiamshe hasira za Mungu.

Aidha, tuwapige vita watu wanaojihusisha na vitendo vya kishoga nchini kwa kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa sababu tunaishi nao majumbani mwetu ili kuepuka kumkasirisha Mungu.
Jipu limepasuka siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

No comments:

Post a Comment

New