My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, March 19, 2012

Neema kwa Watanzania - Mstari wa Head Line

Head Line – Palm Reading Lesson
Leo Nimewaleteeni mstari uitwao Head Line. Kikubwa katika kuuchambua mstari huu leo ni kuwapa siri ya jinsi ya kupambana na changamoto za maisha bila nguvu nyingi ila kwa kuujua tu mstari huu.
Wale ambao mstari huu kiganjani mwao ni mfupi nawasihi sana wasifanye kazi zinazotumia akili nyingi. Badala yake wafanye kazi zinazohitaji nguvu zaidi ya akili kwa kuwa ndivyo MUNGU alivyowaandikia riziki yao. Ndio maana wapo watu ambao hutamka wazi kuwa hawazipendi kazi zao na wala hawaoni tija kuendelea nazo na alama ya wazi kuwa ndio wao hao wenye Head Line fupi utawaona wana ndita za paji la uso kama dalili kuwa hawa si watu wa masihara na hawapendi kweli masihara yasiyo na msingi.
Tuje kwa wale ambao wanafanya kazi zinazohitaji nguvu zaidi ya akili halafu wakijiangalia viganjani mwao wanaona mstari huu ni mrefu na umenyooka, halafu wana alama ya wazi kwa yeyote kuwajua. Alama hiyo ni ndita za nyuma ya shingo zinazoashiria wao ni watu wa masihara na utani sana basi wajue wameingilia kazi zisizo zao na ninawasihi sana waache kazi hizo kwani kuyafikia malengo yao maishani itakuwa ndoto ya mchanaaaa!. Hawazifurahii kazi zao hizo na kufanikiwa maishani itabaki kuwa story tu. Wao wanatakiwa wafanye kazi zinazohitaji akili zaidi kuliko nguvu na watafanikiwa katika muda mfupi sana. Nitatoa mifano miwili inayowahusu watu muhimu na maarufu sana hapa duniani wenye tofauti hizi mbili ili kila mtu aamini katika hili.

1. Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete.
Siku moja baada ya kuijua tu taaluma hii nilianza kumtafuta mdau wa fani hii hapa Tanzania aweze kunipa mawazo tofauti na pengine ushauri tu na nikaambulia kuambiwa alikuwa Marehemu Mzee Profesa Vulata pale Mwananyamala Dar Es Salaam ndiye aliyekuwa Palm Reader pekee. Nikaona basi kumbe hakuna mdau hivyo kama mwananchi mzalendo ni vema kuchukua majukumu kitaaluma ya nchi nzima ikiwemo jukumu la ulinzi wa nchi kupitia fani halafu mengine baadaye. Watu wasiojua mambo ya fani hii huwa wananibeza lakini hawajui kuwa wanatakiwa kuwa na mawazo chanya na kunisaidia kwa kuwa namlinda Mheshimiwa Rais kimya-kimya bila mtu kujua nafanyaje kwa kuwa nilipompekua tu nilimkuta ana mstari wa majanga. Hivyo nilivuta pumzi kwa kuiona hatari mbele ya rais wetu ambaye ndiye dereva wa basi tulilopanda basi nikaona kumbe nawajibika kumlinda hata ikibidi asijue kinachofanyika kwa maslahi ya nchi yetu na mpaka leo kuna mambo nafanya kama ishara njema ya kumrusha katika mashimo ya mabalaa na misala inayomwandama kutokana na mstari huo alionao ambao nakumbuka tulishauongelea katika makala ya kwanza.

Hivyo matatizo na majanga kumtokea Mheshimiwa Rais wetu hilo nawaomba wenye shaka nalo waliondoe, watulie kabisa kwa kuwa ulinzi toka JIWE KUU LA PEMBENI upo makini, umedhibitiwa, na “hataanguka tena jukwaani” hivyo mnaomwombea mabaya msahau na mkatafute kazi nyingine.
Lakini, sikuishia kumwangalia mstari wa majanga tu niione misala yake, bali niliutupia macho pia mstari wa Head Line huu tunaouzungumzia leo. Hapo niliruka kwa furaha almanusura nimshtue anishike wizi. Nilimkuta ana mstari huu wa Head Line mreeeefu halafu umenyooooka kwa madaha kuashiria “ Fikra zake ni sahihi na zenye mwonekano chanya” Upo Hapo? Mungu alimpa mstari huu kwa vile tayari anao ule wa “Misala” ili aweze kuyamaliza kiutu-uzima bila jasho na wasioamini watakumbuka alivyoahidi kumaliza zogo la siasa Zanzibar ndoa ya mkeka tayari, Majambazi siku zao kuhasabika kweli nchi imepoa, migomo ya wanafunzi, Madakitari, waalimu n.k., Mabadiliko ya tabia nchi kama ukame wa maji baadaye chakula na hata sasa mdororo wa uchumi duniani, na hata suala gumu la katiba atalimaliza kwa madaha mno….Waliomchimbia mkwala kuwa 2015 bila katiba mpya hapatatosha imekula kwao kwa kuwa misala ni lazima akutane nayo katika maisha yake ili uwezo wake wa kutumia akili katika masualamazito udhihirike. Hii inaonyesha bwana mkubwa huyu amechagua kazi sahihi inayotumia akili zaidi ya nguvu kama Mungu alivyomjaalia. Hivyo washindani wake wajiandae kweli, na wale wenye fursa ya kumsogelea wampekue waone ninachoeleza mimi nisiyemkaribia hata siku moja ndio waelewe ninachoongea hapa. Na kwa wale wasio na fursa ya japo kumsogelea tu basi wamwangalie ndita za nyuma ya shingo zinazoashiria kuwa Rais ni mmoja wale wenye masihara na utani mwingi hivyo hata zile ndita anazolazimisha kwenye paji la uso huwa hazidumu maana haishiwi vicheko mdomoni vinavyozifuta ndita zake na anabaki na zile za nyuma ya shingo daima .

2. Roman Abromovich Mmiliki wa Chelsea FC.
Huyu Jamaa ana mstari wa Life Line mfupi, wenye mikato mingi kati yake. Wenye ujanja wa kumfungua kiganja wafanye hivyo wataona hili. Hii ni ishara kuwa jamaa kwanza si mtu wa kufanya kazi zinazotumia akili ila zile zinazotumia nguvu zaidi kitu kinachomfanya kwanza asijue anakosea wapi kupata makombe na mataji ya ligi za Uingereza na Ulaya pia. Halafu pia inamfanya awe na kiburi cha umatemate (fedha) kuiongoza klabu kwa nguvu ya pesa na sio akili tofauti na nilivyomsoma Rais Kikwete hapo juu kitu ambacho kinaashiria hatachukua muda mrefu eidha kuibinafsisha timu iendeshwe kitija, au kuiuza kabisa kwa wamiliki wengine kwa kuwa hana kipaji cha uongozi ila Mungu amemjalia kutumia nguvu tu na sio akili. Yeye ana kipaji cha kazi za nguvu zaidi ya akili ndio maana ndita za paji la uso haziishi. Ukimletea masikhara anaweza akaku...

Mbaya zaidi, Mstari huohuo wa Head Line sio mfupi tu, bali pia una vistari vidogovidogo viiingi vimeuganda kuashiria kuwa jamaa ana maamuzi ya kushtukiza – shtukiza daima. Kama ningeweza kuwa karibu naye nadhani ningemsaidia kuinusuru Chelsea FC. Hapo naomba kama wewe unayenisoma una tabia hiyo hebu jiangalie kiganjani utaona hili. Hivyo hapa wale waliokuwa wanahoji uwezo wangu wa kumsoma mtu kiganja nawaomba waelewe kuwa naweza kusoma kiganja hata cha mtu nisiyemjua, na nitakachohitaji ni kujua baadhi tu ya tabia na nyendo zake. Hivyo si Mheshimiwa Rais, wala Bw. Abromovich ambaye amewahi kunipa kiganja chake nimsome ila ni umaarufu wao tu umenifanya niweze kujua viganjani mwao wamepewa karama gani na Mungu.

Narudia tena. Palm Reading sio uchawi hivyo sina kabisa uwezo wa kumroga mtu. Wengine wamehisi labda wakikutana na mimi naweza kuwafanyia utapeli pia. Hapa napenda kuwasisitizia kuwa Palm Reading ni kama kuendesha baiskeli tu na kuwa tapeli, mwongo, mwizi katika fani hii ni kitu kingine kipya na inategemea taswira ya mtu na wale wote walioonana na mimi nina imani kubwa watakuwa mbele kunielezea namna nilivyowapa msaada sahihi wa nini cha kufanya katika maisha. Hivyo nawaomba mzidi kujitokeza kwa wingi zaidi kuja kujua mlipokwama na nini mfanye kujikwamua katika maisha, kazi, biashara, ndoa na mahusiano pia.

Kwa kuwa huu si uchawi na wala si utapeli. Ni fursa adimu sana ya kujua hatma ya maisha yako kwa kukisoma tu kiganja chako na kujua kila kitu kinachojiri. Hii itakusaidia kuondoa hofu za maisha na kujua namna ya kujirekebisha pale ulipokosea ili ufanikiwe mambo yako.

Kama una tatizo, swali, au maoni basi usisite kunipigia simu siku na saa yoyote. Lakini pia kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa ni 19% ya Watanzania ndio wanaojua computer na wenye uwezo wa kunisoma hapa basi kumbe nikuombe ndugu yangu unifikishie salamu hizi kwa wote uwajuao ili na wao wayasikie haya maajabu.

Wiki ijayo tutakuja na mstari wa maisha au Life Line. Mstari huu ni huo nusu-mwezi unaokizunguka kidole-gumba hapo kiganjani.

No comments:

Post a Comment

New