My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, August 24, 2012

LL COOL J AMDHIBITI MVAMIZI KATIKA NYUMBA YAKE HADI POLICE WALIPOWASILI




Mvamiaji katika nyumba ya mwigizaji na mwanamuziki, LL COOL J, jina kamili (James Todd Smith), hatimaye alijikuta na majeraha kwa kibano kikali kilichopelekea kuvunjika pua, taya na mbavu kutoka kwa LL cool J mwenye umri wa miaka 44. Mvamiaji huyo Jonathan A Kirby kwenye umri wa miaka 56 alikutwa na COOL J jikoni saa za asubuhi ya Jumatano 22/08/2012 bila ukaribisho hivyo akaambulia kibano hicho kutoka kwa mwanajeshi huyu wa zamani katika jeshi la majini la Marekani na kuwekwa chini ya ulinzi hadi polisi walipowasili huku akiwa na maumivu makali ya kichapo alichokipokea. Akitoa maelezo kwa askari polisi, LL COOL J alisema chanzo cha uvamizi huo hakitambui ila aliomba askari kumpeleka Jonathan hospitali kwa kuwa alikuwa amemnawa ipasavyo, aling´amua Frank Preciado ambaye ni msemaji wa idara ya jeshi polisi jimbo la Los Angeles (LAPD). Askari polisi walipofika katika nyumba ya LL walikuta mtuhumiwa amepumzishwa chini ya ulinzi na walichofanya ni kumfunga pingu na kumuwahisha kwenye huduma ya afya huku wakichukuwa maelezo kutoka kwa Star huyo jasiri ambaye hakuwa na jeraha hata moja. Akiulizwa kama alichofanya star huyu ni sahihi, msemaji huyu wa jeshi la polisi alijibu kuwa ingawa mvamizi huyu hakuwa na silaha ila kwa sababu za usalama haswa kwa mtoto wa kike wa LL COOL J na ndugu waliokuwemo ndani ya nyumba, ilimlazimu kufanya kila awezavyo kuhakikisha usalama kwa familia yake, hata hivyo familia ya J imewashukuru na kuwaomba radhi majirani kwa usumbufu. Habari zaidi zinatonya kwamba mvamizi huyu ameshakamatwa mara kadhaa kufuatia tuhuma za wizi na uvunjaji wa sheria ikiwa ni pamoja na kwenda jela kwa miaka mitano kwa makosa ya ujambazi miaka ya 1990, na aliwahi kukaa mahabusu kwa makosa ya udokozi 2005. Aidha jambarika hili limedaiwa kulipa faini ya $1.1 milioni au kwenda jela maisha.

No comments:

Post a Comment

New