My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, August 12, 2012

RAIS KIKWETE AONANA NA RAIS MPYA WA GHANA, ATEMBELEA MASHAMBA YA MANANASI




 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiagana na Rais John Dramani 
Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini  Accra jana Agosti 11, 2012 
baada ya  kumtembelea na  kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi 
hiyo Marehemu John Evans Atta Mills aliyezikwa juzi.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na Rais John Dramani 
 Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini  Accra jana Agosti 11, 2012  
 wakati alipomtembelea kiongozi huyo mpya wa Ghana na  kumpa pole ya msiba 
wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama mananasi yakitayarishwa kwa ajili ya 
kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha  Bomarts Farms Ltd 
 katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra jana Agosti 11, 2012.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa mananasi yanayolimwa  
kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shamba la Bomarts Farms Ltd katika kijiji cha 
Dobro katika eneo la Nsawam  nje kidogo ya jiji la Accra jana Agosti 11, 2012. Kulia 
kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya 
bluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo, Mhe. Kwesi Ahwol.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya  mananasi katika 
shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya jiji la Accra. Kulia kwake ni 
Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd, Bw Emmanuel B. Koranteng ambaye 
amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka 27. Mwalimu Nyerere aliwahi 
kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka ya 1980 kujionea ukulima 
huo wa matunda.

(PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment

New