My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, January 19, 2012

GLOBAL Lulu aachwa na ndege Dar

Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Na Shakoor Jongo
MUIGIZAJI kinda Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliachwa na ndege baada ya kuchelewa kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Sakata hilo la aina yake lilitokea, Januari 11, mwaka huu, uwanjani hapo, ambapo Lulu alikuwa na safari ya kwenda mapumzikoni katika Visiwa vya Comoro.
Ilielezwa kuwa, kilichomponza msanii huyo ni kutokufuata muda, kwani tiketi yake ilimwonesha alitakiwa kufika uwanjani hapo saa 8:00 mchana na muda wa safari ulikuwa ni saa 10:00, lakini yeye akafika muda wa kuondoka, hivyo akaachwa.
Lulu alipopatikana, alifunguka: “Ni kweli nilichelewa kufika uwanjani nikaachwa, nilikuwa na rafiki yangu Baby Candy, lakini nimeamua kuja huku Moshi kupumzika baada ya kushindwa kwenda Comoro.”

No comments:

Post a Comment

New