My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, January 19, 2012

Kanumba afanyiwa ‘umafia’

Steven Kanumba.

Na Joseph Shaluwa
HANDSOME boy anayefurukuta kwenye tasnia ya filamu Bongo, Steven Kanumba amefanyiwa uhuni na watoto wa mjini kwa kutumia jina lake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Risasi Mchanganyiko limegundua.
Mwandishi wetu alishuhudia watu wanne tofauti wanaotumia jina la ‘Steven Kanumba’ katika kurasa zao za mtandao huo unaojizoea umaarufu kila kukicha.
Watatu kati yao, hawajaweka maelezo yao ya kutosha, zaidi ya jinsia, umri na picha ambazo ni za Kanumba.
Mtumiaji wa nne, licha ya kutumia jina la Kanumba, ameweka picha ya staa wa filamu ya Titanic, Leonard Dicaprio, huku kwenye albamu yake kukisheheni wasanii mbalimbali wa filamu Bongo, akiwemo Rose Ndauka.
Aidha, ameandika kwamba anaishi Boston, Massachusetts, lakini ni mzaliwa wa Dar es Salaam, Tanzania.
Marafiki wa watu hao, wamekuwa wakitoa maoni ya kuwapongeza, wakiamini kwamba wanayechati naye ni Kanumba kumbe ni changa la macho.
Wengine wamekwenda mbali zaidi na kuonesha wazi dalili za kutaka kuanzisha uhusiano wa mapenzi, sehemu nyingine Kanumba feki, ndiye aliyejipendekeza kwa wasichana wanaotoa maoni ya kusifia kwenye picha zake.

KANUMBA HALISI
Akizungumzia suala hilo, kwa njia ya simu, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam alisema kuwa anafahamu juu ya watu hao, lakini anawatahadharisha mashabiki wake kuacha kuwaamini.
“Kaka ni kweli kuna hao jamaa, yaani hata mimi mwenyewe nilipotaka kufungua akaunti kwenye ukurasa huo, nilikuta jina langu linatumika na watu wengine. Sikuwa na jinsi, zaidi ya kubadili jina.
“Ikanilazimu nifungue kwa jina la Kanumba Steve, maana hata Kanumba Steven nalo pia linatumika. Najua ni kwa nini wanafanya hivyo, wanataka kutapeli watu au kupata wasichana kirahisi.
“Ukweli ni vigumu sana kuzuia hilo moja kwa moja, lakini kuna mmoja niliweza kum-block, ila ninachoweza kuwaambia mashabiki wangu, wasimuamini mtu yeyote kwenye facebook, twitter au mtandao mwingine wowote, maana watu wanaweza kufanya watakavyo kwa sababu picha zangu zipo kila mahali.
“Watu wanajua profile yangu, hivyo wanaweza kujifanya ni mimi. Mtu asifanye biashara yoyote kwenye mtandao hadi awe ameonana na mimi mwenyewe au kuwasiliana nami kwenye namba zangu official,” alisema Kanumba.

AFAGILIA WALK OF FAME
Katika hatua nyingine, Kanumba ameifagilia Kampuni ya Global Publishers Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Amani, Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na gazeti hili la Risasi kwa kuandaa tuzo za Tanzania Walk of Fame.
“Sisifii kwa sababu nami nimeshinda, ila ni ukweli kwamba Global wanawajali sana wasanii wa Tanzania. Hizi si tuzo za kwanza, nakumbuka kuna Risasi Award, Ijumaa Sexiest Girl, Ijumaa Sexiest Bachelor, Mkali wa Kuchekesha na nyingine nyingi,” alisema.

No comments:

Post a Comment

New