My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, January 20, 2012

THEA:Kwa hili Monalisa ni mnafiki jamani

Na Brighton Masalu
MSANII wa filamu Bongo, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ (pichani) amemtuhumu mwigizaji mwenzake, Yvone Cherry Ngatwika ‘Monalisa’ kuwa ni mnafiki kwani anafufua bifu lililoisha.
Akizungumza na Ijumaa juzi maeneo ya Mwananyamala ‘A’ jijini Dar, Thea alisema kuwa amefikia hatua ya kusema hivyo kufuatia mwenzake huyo kulitonya gazeti damu moja na hili (Ijumaa Wikienda) kwamba bifu lao la nyuma halijafutika.
Thea ambaye ni mke wa msanii, Michael Sangu ‘Mike’ alikiri kuwahi kutokea kwa bifu kati yao lakini akasema walishasuluhishwa na kumaliza tofauti hizo, lakini anashangaa kusikia Mona analiendeleza.
“Ni kweli tulikuwa na bifu la muda mrefu, lakini tuliitwa tukasuluhishwa yakaisha na kila mmoja akawa na heshima kwa mwenzake. Nashangaa hivi karibuni Monalisa anasema kuwa bifu hilo bado ni bichi, huu kwangu ni unafiki,” alisema Thea.

No comments:

Post a Comment

New