My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, February 9, 2012

ROSE MUHANDO ALA SHAVU SONY MUSIC

Manusha Sarawan akielezea mchakato wa kumpata Rose Muhando ulivyofanyika.

Rose Muhando akielezea furaha yake ya kuchaguliwa kuwa balozi wa Sony Music.

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku (kushoto,) na wanamuziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Ally Kiba (kulia) wakisikiliza kwa umakini kwenye mkutano huo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Production, Rita Paulsen ‘Madam Rita’ (kushoto,) na mtayarishaji muziki maarufu, Master J, wakibadilisha mawazo kwenye mkutano huo.

Kampuni ya bidhaa za Sony Barani Afrika kupitia vifaa vyake vya muziki imemteua mwanamuziki wa nyimbo za Injili hapa nchini, Rose Muhando, kuwa mmoja wa mabalozi wake. Uteuzi huo umetangazwa leo na Mkurugenzi wa Mambo ya Masoko, Manusha Sarawan, katika mkutano na wanahabari uliofanyika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Manusha alisema mchakato wa kumpata balozi huyo ulishirikisha wanamuziki wakongwe zaidi ya 130 barani hapa.

No comments:

Post a Comment

New