My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, February 21, 2012

UJUE 'HEART LINE' KATIKA KIGANJA CHAKO

Hallow,
Wiki jana niliandika kuhusu usomaji wa viganja "Palm Reading" Na nilianza na watu wenye mstari wa majanga unaojulikana kama "Fate Line" Nashukuru ujumbe ulieleweka kwa wengi na nashukuru kwa kuitikia kwenu kuokoa maisha kupitia sanaa hii ya kisayansi.
Leo nimekuja na watu wengine ambao mstari wa heart line unaovigawa vidole na kiganja umejikunja ukaingia kati ya kidole cha shahada na kidole cha kati.
Watu hawa kwanza ni watanashati na wanawake ni warembo na wacheshi sana. kama ulifungua ile link niliyokupa ushuhudie wameelezwa kuwa "they fall in love easly" ikimaanisha kutapeliwa, kudanganywa, kuzulumiwa, na vitu kama hivyo ni kitu cha kawaida kwao.
Ni kawaida kabisa kila ukutanapo na mtu wa aina hii kukupa mikakati mipya ya maisha yake kwa kuwa ile aliyokusimulia mwaka jana imefeli kuzaa matunda.
Wanawake mimba zinaharibika, wapenzi wanawakimbia kila kukicha,ndoa zinavunjika, kazi mbaya kila siku kwa kuwa kila likitokea tatizo yeye ndiye anayetolewa sadaka. Biashara zinaanza vizuri hazichukui muda zinakufa na mambo kama hayo.

Wanaume wanabaki kuoa kila kukicha maana wamekimbiwa, kazi na biashara mpya kila siku maana mipango hainyooki n. k. Kifupi hawa watu wanakuwa ngazi za kuwanufaisha wengine.

Mbaya zaidi utakuta kuwa hata waathirika wa UKIMWI wengi ni hawa wenye mstari huu kwa kuwa wamebadili wapenzi mpaka wamekalia migongo kwa kuchoka.

Hatari ni nyingi ukiacha UKIMWI na maisha mabovu kila kukicha. Jiangalie vizuri kama mstari huo katika kiganja chako umeingia kati ya shahada na kidole kati basi basi nitafute nikuokoe na majanga haya kabla huja "fall in love easly" na kuingizwa mkenge tena. Kwa wale wanaodhani kuwa huu ni UCHAWI napenda kuwatuliza kuwa huu sio uchawi bali ni elimu tu ya kawaida inayohitaji macho mazima kuona, akili ya kawaida kusoma, na kiganja cha kusomwa tu basi. Wazungu wao wapo mbele katika taaluma hii na kama huamini basi fungua hiyo link hapo chini uone.

http://www.wikihow.com/Read-Palms

No comments:

Post a Comment

New