My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, February 17, 2012

Wema Bwana!

Musa Mateja
WEMA Isaac Sepetu amefungua ukurasa mwingine, amezua mjadala wa kimapenzi juu yake baada ya kusambaa kwa picha zake tata za kimahaba akiwa na kidume ambaye jina lake halikupatikana.
Tukio hilo lilichukua nafasi katika mtandao wa BBM wikiendi iliyopita ambapo mara tu baada ya Wema kutundika picha hizo kwenye ukurasa wake bila kusema chochote, marafiki zake walianza kuzishambulia kwa kuzitolea maoni.
Picha hizo zilizomuonesha Wema akimbusu jamaa huyo shavuni ziligeuka gumzo pale baadhi ya watu walipodai kuwa huenda ndiye ‘bwana’ke’ mpya baada ya kuachana na mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’.
“Wema bwana! Hebu angalia hilo busu, linaonesha hisia kabisa,” ilisomeka sehemu ya maoni hayo.
“Huyu Wema ‘anaanzaga’ hivihivi kama ilivyokuwa kwa Diamond,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni hayo huku ikiungwa mkono na wengi.
“Jamani mwacheni shosti wangu, hata yeye ana hisia zake kwa sababu naye ni binadamu,” ilisomeka sehemu nyingine iliyokuwa ikimtetea Wema.
Hata hivyo, baada ya kuona maswali yanakuwa mengi, Wema alizichomoa picha hizo na kuwaacha watu na viulizo.
Ili kuondoa utata juu ya picha hizo, Amani lilifanya jitihada za kumpata Wema anayetisha katika filamu za Kibongo lakini ziligonga mwamba huku rafiki wa karibu akitonya kwamba hayupo nchini ametimkia Dubai kwa majukumu binafsi.

No comments:

Post a Comment

New