My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, February 5, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI SHEREHE ZA MKESHA WA MAULID MNAZI MMOJA DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja katika shamrashamra za mkesha wa sherehe za Maulid, jijini Dar es Salaam jana Februari 04, 2012 usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, wakati wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es Salaam, Muzamil Chaki, akiimba Qaswaida jukwaani kutoa burudani wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku Februari 04, 2012.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es Salaam, Muzamil Chaki, baada ya muumini huyo kumaliza kutoa burudani ya Qaswaida jukwaani, wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku Februari 04, 2012.

No comments:

Post a Comment

New