My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, February 10, 2012

Shilole aifungukia stori yake ya kubakwa


Na Erick Evarist
MSANII wa filamu Bongo ambaye pia anafanya freshi kwenye muziki wa mduara, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ (pichani) amefunguka kuwa katika maisha yake ya kimapenzi hatasahau siku aliyobakwa na mwanaume ambaye kwa sasa hawezi kumuweka wazi.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Shilole alisema kuwa tukio hilo lilimfika akiwa ndiyo kwanza anaingia kwenye ulimwengu wa malavidavi ambapo mwanaume huyo alimlazimisha kufanya naye mapenzi.
“Katika maisha yangu nimepitia mitihani mingi, mmoja wapo ni huu wa kulazimishwa kufanya mapenzi bila ridhaa yangu, kwa kifupi nilibakwa. Niliumia sana hasa ukizingatia kuwa kipindi hicho nilikuwa sijawahi kabisa kufanya mambo hayo.
“Kila ninapomkumbuka yule mwanaume naumia sana, kamwe sitamsahau. Historia hii na nyingine kuhusu maisha yangu inapatikana katika filamu yangu mpya inayoitwa Shilole In Dar,” alisema Shilole.

No comments:

Post a Comment

New