My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, February 17, 2012

Mama: Ray C rudi nyumbani

Na Shakoor Jongo
MAMA wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ aitwaye Magreth amemtaka mwanaye huyo ambaye kwa sasa anaishi jijini Nairobi, Kenya arudi Bongo.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Ray C aliyeomba hifadhi ya jina lake, mama huyo hajakifurahia kitendo cha mwanaye kwenda kuweka kambi Kenya na kwamba kila siku amekuwa akiomba arejee nyumbani ili awe karibu naye.
“Mama yake anataka Ray C arudi Bongo kuja kufanya shughuli zake za kimuziki, anafurahi kumuona mara kwa mara na mwenyewe anasema atafurahi zaidi kama atakuja kumuimbia Mungu,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kupata ‘nyiuz’ hizo mwandishi wetu alifanya jitihada za kumsaka mama wa Ray C lakini ilikuwa vigumu kumpata.
Hata hivyo, mwanzoni mwa wiki hii mama huyo alisikika akizungumza katika Kipindi cha Amplifaya kinachorushwa hewani na Mtangazaji Millard Ayo kupitia Radio Clouds ambapo alikiri kutaka mwanaye arudi nyumbani.
Alisema yeye hajampa Ray C baraka za kwenda kuishi Kenya hivyo anamsihi kama anamsikia arudi Tanzania aje amuimbie Mungu.
Ray C kwa sasa anaishi na kufanya shughuli zake za kimuziki nchini Kenya na juzikati alizindua bendi yake.

No comments:

Post a Comment

New