My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, February 5, 2012

RAIS KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI YA MIAKA 35 YA CCM JIJINI MWANZA LEO

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza kuongoza matembezi ya mshikamano kwa ajili ya maadhimnisho ya miaka 35 ya CCM leo asubuhi. Anayempokea ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na wengine ni Spika wa Bunge Anna Makinda ambaye ni mlezi wa mkoa huo na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama. Pamoja na Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilllo.Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Philip Mangula kabla yamatembezi kuanza Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza. Kulia ni Katibu Mkuu Mstaafu Yussuf Makamba.
Rais Kikwete akimsalimia Nape Nnauye Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya matembezi hayo.
Wananchi kutroka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo tayari kushiriki matembezi hayo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi hayo kutoka kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza hadi viwanja vya Furahisha jijini Mwanza akiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa CCM. Kutoka Ofisi hiyo hadi kwenye viwanja ni umbali wa kilometa tatu.

No comments:

Post a Comment

New