My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, February 10, 2012

Rehema Fabian aanguka, alazwa kwa presha

Na Gladness Mallya.

MREMBO aliyepata umaarufu kupitia ushiriki wake kwenye Shindano la Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian amedondoka ghafla kwa presha na kukimbizwa hospitalini.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, Rehema alikutwa na hali hiyo kutokana na presha kushuka alipokuwa ‘akishuti’ filamu (haikutajwa) katika Barabara ya Sam Nujoma maeneo ya Mlimani City, Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii.
“Baada ya kudondoka tulihisi ana ugonjwa wa kuzimia ovyo lakini tulipomkimbiza Hospitali ya Kinondoni (Dar es Salaam), tuliambiwa ni presha ilikuwa imeshuka ‘so’ alilazwa kwa saa kadhaa, akatundikiwa ‘dripu’ mbili hadi aliporejea kwenye hali ya kawaida,” kilisema chanzo chetu.
Akizungumza na paparazi wetu muda mfupi baada ya kuruhusiwa, Rehema alisema aliishiwa nguvu ghafla na hakujua kilichofuata hadi alipozinduka na kujikuta akiwa katundikiwa dripu.
“Huwa nina tatizo la presha kushuka, lakini nina muda mrefu kwa hiyo nilifikiri limekwisha lakini kumbe tatizo liko palepale, namshukuru Mungu, naendelea na dozi,” alisema Rehema ambaye amekuwa akiripotiwa kuumwa mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

New