My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, February 5, 2012

WAZIRI MKUU MIZENGO PINGA KUTUA IRINGA LEO KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA CCM

Mhe.Mizengo Pinda

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda leo anataraji kuwasili mjini Iringa kwa ajili ya sherehe za kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi (CCM).

Waziri Pinda ambaye ni mlezi wa CCM mkoa wa Iringa mchana wa leo atakuwa na mkutano mkubwa wa wana CCM katika kata ya Kihesa jimbo la Iringa mjini na jioni ataondoka kuelekea wilaya Mufindi kwa ajili ya matembezi ya mshikamano kesho asubuhi katika kata ya Igowole wilaya ya Mufindi pamoja na kuwahutubia wana CCM na wananchi wa wilaya ya Mufindi.

CCM mkoa wa Iringa imewaomba wana CCM mkoani hapa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya mlezi huyo wa CCM mkoa pia katika kusherekea sherehe hiyo kubwa kwa CCM nchini.

No comments:

Post a Comment

New