My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, February 10, 2012

WASANII WAKALI KUSHIRIKI SHOO DAR LIVE JUMAPILI

Mwana FA akielezea jinsi atakavyofanya makamuzi ya nguvu.

Ambwene Yessayah ‘AY’ akiumwagia sifa ukumbi wa Dar Live ambao baada ya kuuona aligundua kuwa una hadhi ya kimataifa.

Chegge akielezea jinsi atakavyofunika katika shoo hiyo 'bab kubwa'.

Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Fella, akithibitisha kushiriki katika onyesho hilo.

Sehemu ya wanahabari wakiwa makini kwenye mkutano huo.

WASANII wakali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mwana FA, Ambwene Yesaya (AY), Kundi la TMK Wanaume Family na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ kwa pamoja wanatarajiwa kuangusha bonge la shoo siku ya Jumapili ijayo ndani ya Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam huko Mbagala. Akizungumza na wanahabari mchana huu, mratibu wa burudani katika ukumbi huo, Juma Mbizo, alisema maandalizi yote kuhusiana na tamasha hilo yamekamilika.

No comments:

Post a Comment

New