My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, February 2, 2012

ONYESHO LA MAVAZI LA LADY IN RED KUTIKISA DAR FEBRUARI 10

Meneja wa Kinywaji cha Redd’s, Victoria Kimaro (kushoto), akizungumza na waandishi (hawako pichani) katika mgahawa wa Nyumbani Lounge. Wengine ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous, na Katibu wa Kikale Youth Care Group, Maulid Mlawa.

Kimaro, Idarous na Mlawa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanamitindo.

ONYESHO la mavazi lijulikano kama Lady In Red 2012 linatarajiwa kufanyika Februari 10, mwaka huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya Fabak Fashions kwa kushirikiana na Kikale Youth Group itawahusisha wanamitindo zaidi ya 30 kutoka Tanzania ambapo wasanii tofauti akiwamo Chiddy Benzi, watakuwepo siku hiyo kusindikiza onyesho hilo la mavazi.

No comments:

Post a Comment

New