My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, February 14, 2012

MAZISHI YA MUGABE YATIKISA

Mwandishi Wetu na Mitandao
UTABIRI wa Kiongozi wa Kanisa la Synagogue nchini Nigeria, TB Joshua kwamba Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe hana miezi miwili kabla ya kifo chake, umeamsha mtikisiko kuhusu mazishi ya kiongozi huyo mkongwe barani Afrika.
Tangu TB Joshua alipotoa utabiri wake kwenye kanisa lake, leo ni siku ya tisa, hivyo siku 60, alizomtabiria Mugabe, zimebaki 51.
TB Joshua alisema kuwa Mugabe hawezi kumaliza siku 60 akiwa hai, akaeleza kwamba hesabu hiyo inaanzia pale alipotangaza utabiri wake.
Ingawa utabiri wa TB Joshua umelaaniwa mno na Wazimbabwe wanaoamini katika huduma za Mugabe, tamko lake limeibua mchuano wa vyombo vya habari vya kimataifa kuhusu namna watakavyoripoti kifo na mazishi ya kiongozi huyo.
Habari zinasema kuwa mashirika makubwa ya habari ya Al-Jazeera, SABC, BBC na CNN, kila kimoja kinawania kununua haki ya kuwa chombo cha kwanza kutangaza habari ya kifo cha Mugabe.
Hata hivyo, inaelezwa kwamba ni ngumu kwa mashirika hayo kupata haki hiyo, kwani idhini inatoka ndani ya familia ya Mugabe na kila mwanafamilia anamuogopa kiongozi huyo kwa sababu itaonekana amesadiki kifo chake.
Mugabe, alianza kuiongoza Zimbabwe tangu mwaka 1980, hivyo ana miaka 32 madarakani, wakati Februari 21, mwaka huu akitarajiwa kutimiza umri wa miaka 88.
Kwa muda mrefu, Mugabe amekuwa akiripotiwa kusumbuliwa na maradhi yanayotokana na uzee.
Zipo taarifa kuwa Chama chake cha Zanu-PF kinajipanga bila kumshirikisha Mugabe kuhusu namna ya kumzika kifahari kiongozi huyo kwa kuanzia kumtengenezea jeneza la thamani pamoja na kaburi lenye hadhi kubwa kama muasisi wa Taifa la Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment

New