My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, February 9, 2012

NANI KAWADUNGA?

Maimartha Jesse.

Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’.

Shamsa Ford.

Zamaradi Mketema.

Judith Wambura ‘Jide’.

Na Musa Mateja
TUNAWEZA kusema mwaka 2012 ni wa mimba kwa mastaa wa Kibongo, kwani kwa jumla wanafika watano wenye vibendi, wengine ni wa leo au kesho kujifungua, Amani lina ripoti kamili.
Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, mastaa hao karibu wote wanahesabu siku kwa vile wamebakiza muda mchache, wengine wameanza kununua nepi na bebi shoo.
HAWA HAPA
Mastaa hao ni Shamsa Ford, Judith Wambura ‘Jide’, Maimartha Jesse, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na Zamaradi Mketema.
NANI KAWADUNGA?
Hata hivyo, swali linaloulizwa na mashabiki wao limebaki kuwa nani wahusika wa mimba hizo kwa kila mmoja.
Shamsa Ford; jamaa anayetajwa kwa jina la Dickson ndiye anadaiwa kumdunga ujauzito staa huyo wa muvi za Kibongo huku Jide ambaye ni mwanamuziki mkubwa Bongo akijulikana ni mke wa mtangazaji Gardner G. Habash.
Maimartha yeye alifunga ndoa ya siri hivi karibuni na Raymond Mushi ambaye hataki picha yake ionekane kwenye vyombo vya habari, ikidaiwa anafanya kazi sehemu nyeti katika nchi hii.
Mcheza sinema Thea ni mke wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’ kwa hiyo hakuna shaka kuwa, mimba inabaki kuwa ‘kitanda hakizai haramu’.

VIPI ZAMARADI?
Kazi iko kwa Mtangazaji wa Kipindi cha Take-One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema ambaye mpaka sasa, baba wa mtoto wake mtarajiwa, hataki kumwanika licha ya kwamba, jina lake linajulikana na wengi kwa sababu ni mtu mwenye cheo.

WAHOFIA KUJIFUNGUA KWA ‘KISU’
Aidha, habari za kusikitisha ni kwamba, baadhi ya mastaa hao wenye ‘vibendi’ wanahofia endapo watajifungua kwa njia ya upasuaji (kisu).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Amani, mastaa hao walisema wanamuomba Mungu kwa nguvu zote ili awaondelee shetani wa kisu siku ikifika.
Shamsa: “Namuomba Mungu anijalie nijifungue kawaida, siyo kwa upasuaji kwa sababu naogopa sana kupasuliwa na kutokana na maombi yangu naamini atanijalia.”
Zamaradi: “Mimba yangu ni kubwa sana na ninatarajia kujifungua siku si nyingi ila sitaki kuzungumzia chochote kwa sasa hadi nitakapojifungua.”
Thea: “Mimba hii ina miezi mingi ila haijafikia kujifungua na nitafurahi sana kama nitapata mtoto wa kike ingawa hayo yote ni mipango ya Mungu likiwemo la njia ya kujifungua.”
Kwa upande wao Maimartha na Jide hawakupatikana hewani kuzungumzia ishu hii.

No comments:

Post a Comment

New