My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, October 31, 2011

Bi harusi mtarajiwa


Na Musa Mateja

PICHA za Bi Harusi mtarajiwa ambaye ni modo sexy Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack’ hivi karibuni zimenaswa akiwa katika mapozi ya kimahaba na mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Martin.

Picha hizo ambazo zipo kwenye mtandao zinawaonesha wawili hao wakijiachia kwenye Ufukwe wa Mbalamwezi uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, mazingira yaliyosababisha baadhi ya watu kuhoji juu ya ukaribu wao huo.

“Mh! Huyu si ndiyo anatarajiwa kuolewa hivi karibuni? Sasa huyu mwanaume ni nani tena, au ndiyo mchumba wake?” alihoji mdau mmoja baada ya kuziona picha hizo.

Katika kujua uhusiano uliopo kati ya wawili hao, mwandishi wetu alimtafuta Jack kupitia simu yake ya mkononi lakini hakuweza kupatikana mara moja.

Martin alipopatikana alisema: “Picha hizo tulizipiga siku tuliyokuwa tunaandaa matangazo flani hivi, ila hazina maana yoyote mbaya, Jack ni mshikaji wangu wa kawaida tu.”

Jack ambaye ni Miss Ilala namba 3, 2005 anatarajiwa kuolewa hivi karibuni ambapo vikao vya harusi vimeshaanza.


No comments:

Post a Comment

New