My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, October 18, 2011

Imani yako inapaswa iambatane na matendo

Imani nayo inapaswa iambatane na matendo ambayo yanaashiria kupiga hatua kuelekea mafanikioni kwani imani yako ndiyo itakayokufikisha kwenye kile unachokihitaji.

Hata kama wewe ni muumini mzuri wa dini, lakini kama imani yako ni ndogo, si rahisi kujibiwa maombi yako kwani unakuwa huamini kama kweli inawezekana.

Mpenzi msomaji, jitahidi sana kufanya kazi kwa bidii kubwa, jitahidi sana kuwa mwaminifu, kuwa mkweli katika mambo yako ya kimaongezi na kitendaji na juu ya hayo, basi jitahidi sana kuwa na imani kuwa hakuna kinachoshindikana hapa chini ya jua endapo tu utaamua kukifuatilia maishani.

Amini kuwa Mungu yupo na hashindwi kitu endapo kama utamuamini na kupanua imani yako kwake.

Uamuzi wa maisha mazuri ya kesho uko mkononi mwako, kama unaishi maisha ya taabu na mateso kwa sasa basi kuna mahali ulikosea huko nyuma. Huo ni ukweli mtupu.

Hakuna mtu anayeweza kukumulia maisha yako ya kesho isipokuwa wewe mwenyewe. Achana na tabia ya utegemezi kwa wengine na badala yake sasa anza kupigana wewe kama wewe.

No comments:

Post a Comment

New