My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, October 27, 2011

KIFO CHA GADDAFI

Luqman Maloto na Mitandao

ALIYEKUWA Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi ameuawa, mambo mengi yanazungumzwa kuzunguka kifo chake lakini imefichuka kuwa Dini ya Shetani, Freemasons ndiyo mhusika mkuu.

Gazeti hili limetonywa kuwa Jeshi la Kujihami la Nchi za Magharibi (Nato), ni moja kati ya silaha za Freemasons kuelekea kutimiza mkakati wake wa siri wa kuitawala dunia.

Imeelezwa kuwa Gaddafi hakuwa mfuasi wa Freemasons na utawala wake ulikuwa kikwazo cha mafanikio ya Dini ya Shetani kuitawala dunia.

imebainika kuwa dini za Shetani ‘Jamii za Siri’ zipo za aina tatu: Freemasons, Illuminati na Skull & Bones, huku kila moja ikiwa na mkakati wa siri wa kuhakikisha inaitawala dunia.

Habari zaidi zinaeleza kuwa mpaka sasa, Freemasons ndiyo jamii ya siri yenye nguvu kuliko nyingine na ndiyo inayodaiwa kushika mamlaka ya mataifa makubwa ya Marekani, Uingereza, Ufaransa na mengineyo.

Shabaha ya Freemasons na dini nyingine za Shetani kama zinavyofafanuliwa na wachambuzi pamoja na maandiko matakatifu ni kwamba wanataka kuitawala dunia kabla ya ujio wa Yesu (Nabii Isa).

Kwa mujibu wa mnajimu msomi, Maalim Hassan Yahya Hussein, Nato ni shirika linalofanya kazi chini ya Freemasons na hutekeleza maagizo ya jamii hiyo ya siri.

Maalim Hassan ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mnajimu maarufu barani Afrika, Sheikh Yahya Hussein, alisema kuwa msingi wa Nato ni kutekeleza sera na mipango ya Freemasons.

“Wanataka kuitawala dunia. Katika nchi za Marekani, Uingereza na nyingine za magharibi, huwezi kuwa kiongozi bila kuwa Freemason. Muungano wa nchi hizo, ni genge la viongozi wa Freemasons,” alisema Maalim Hassan ambaye ni mrithi wa kazi za Sheikh Yahya na kuongeza:

“Mkakati mkubwa zaidi ni kuhakikisha dunia yote inaabudu Dini ya Shetani. Freemasons, wanataka kila mtu awe chini ya mamlaka ya Jini Mkuu, Lucifer. Dunia nzima itawaliwe na serikali moja, pia kuwe na sarafu moja.”

Kwa mujibu wa maandiko matakatifu, zama za Dini ya Shetani kuishika dunia, kutakuwa na mfumo kwamba ili mtu apate huduma za kijamii ni lazima awe mfuasi wa imani hiyo na atatambulika kwa chapa yenye namba 666.


Japo sakata la Gaddafi linatazamwa kisiasa zaidi, habari zinasema kuwa Freemasons wamedhamiria kuwaondosha viongozi wote wasiotii mamlaka yao na kuhakikisha kwamba kabla ya Desemba 21, 2012, watawala wa nchi zote duniani wawe waumini wa dini yao.


Inaelezwa kuwa watawala mbalimbali wataendelea kuangushwa na Nato itatekeleza mipango hiyo mpaka dunia nzima itakapoelekea kwenye imani hiyo.

KIFO CHA GADDAFI
Gaddafi, aliuawa kwa risasi Alhamisi iliyopita (Oktoba 20, 2011) baada ya kukamatwa na wapiganaji wa NTC waliokuwa wanasaidiwa na vikosi vya Nato.

Inaelezwa kuwa Gaddafi na timu yake, wakiwa kwenye magari ya kifahari, walikuwa wanahama kutoka Jiji la Sirte kuelekea mpakani waliposhambuliwa na ndege za Nato, walipokimbilia mtaroni kujificha ndipo walipokutana na wapiganaji wa NTC.

Hata hivyo, yapo madai kuwa walitaka kutorokea nje ya nchi, ingawa taarifa nyingine zinaeleza kwamba Gaddafi aligoma kuondoka na kusisitiza anangoja kufa kwenye ardhi aliyozaliwa.

Wakati mashambulizi yanaanza ilikuwa saa 2:30 asubuhi (saa za Libya) lakini Gaddafi alikamatwa akiwa hai saa 8:00 mchana, ndani ya mtaro kabla ya kumtesa na kumuua.

MWENDELEZO MBAYA
Kabla ya Libya, mapinduzi yalianzia Tunisia, yakafuata Misri, vile vile yanaendelea kutikisa kwenye mataifa mbalimbali ya Kiarabu.

Habari zinaeleza kuwa mapinduzi hayo yana mkono wa Freemasons ili kuua nguvu ya Dini za Kiislamu na Kikristo.
Inabainishwa pia kwamba katika mapinduzi hayo kila kiongozi anayefuata baada ya utawala uliopo kuanguka, ni lazima awe Freemasons.

Inafichuliwa kuwa Mwenyekiti wa NTC, Mustafa Mohammed Abdul Jalil ni Freemasons ndiyo maana amepewa nafasi ya kuongoza Libya.

No comments:

Post a Comment

New